Mradi wa bandari Bagamoyo pamoja na Magufuli kusema ni wakinyonyaji lakini unatekelezwa!!!

Mradi wa bandari Bagamoyo pamoja na Magufuli kusema ni wakinyonyaji lakini unatekelezwa!!!

Wadau
China anakuja kujenga kwa mkopo toka Oman.

Repayment period mpaka tupewe sisi miaka 99. Muda huu ni mrefu kuliko umri wa uhuru wetu.

Marufuku kuendesha bandari zote Tanga, Dar, Mtwara isipokuwa ni wao tu.

Kwenye industrial parks karibu na bandaro China anakuwa na mandate kumkodishia atakae na haingiliwi kujua bei gani kapata.

Tanzania ingekuwa hub ya imports kuliko exports kupitia bandari hiyo kama ingekuwa hai leo.

Sir Lanka aliumwa na Nyoka. NGOSHA katumia tahadhari kuliko kuingia kichwa-kichwa

Jihabarishe wengine walivyolizwa

Nimeangalia kipindi Azam Tv wanaonyesha namna ya huu mradi utakavyo kuwa, yaani Tanzania haitatumia hata sent tano...

Lakini Magufuli alisema huu mradi ni wakinyonyaji na haufai kutekelezwa lakini leo nimeona kwenye kipindi Azam Tv wakisema mradi utaanza kutekelezwa..

Ni kweli huu mradi wa kinyonyaji utatekelezwa?
Kwani kuna mtu muongo na asiyeaminika kama Rais Magufuli! Lengo lake ni kuipaka matope na kusitisha "mega projects" zilizoanzishwa na JK kwasababu yeye "halambi unga" kupitia miradi hiyo.

We naglia tu anavyoponda miradi ya gesi ya Mtwara na Kilwa na Umeme wa Kinyerezi.
Kama kweli mradi unaendelea basi uje na yeye "anatandaza ulimi" hapo.
 
Jamani eleweni Mtaalamu wangu Magu si kwamba anapinga miradi bali anapinga magumashi yaliyokuwa yamepachikwa ndani ya hiyo mitadi. Kama umeanza basi ni heri
Mh. Raisi hapingi miradi kwani yeye anapenda tupate maendeleo kwa haraka ila anachopinga ni ile miradi yenye magumashi na terms ambazo hazina mashiko na kama amekubali basi kutakua na vitu vimeboreshwa kwenye huo mkataba
 
Mradi unaanza lini? Kampuni gani imepewa tenda ?tukasake tonge.
 
Acheni "Poverty Mentality" Wajukuu Zetu Watakuja Kufaidi Hii Miradi Kitu Kikijengwa Hakifi Leo .

Ivi Mnafikiri Kenya, Ethiopia, Msumbiji Na Kagame Wanafrahia Mradi Kama Huu? Unajuaje Kama Hawakujipenyeza?

Katika Vitu Nitakavyomsifia Kikwete Ni Hii Bandari Na Hospital Ya Upasuaji Kiukweli

Hiyo Sio Gesi Ilichotwa Kinyemela
 
Jamani eleweni Mtaalamu wangu Magu si kwamba anapinga miradi bali anapinga magumashi yaliyokuwa yamepachikwa ndani ya hiyo mitadi. Kama umeanza basi ni heri

Aseme nini kilimfanya agomee mwanzo,na sasa amekubali kwa sababu gani. Isije ikawa alirukwa kwenye mgao mwanzo, na sasa kawekewa fresh ameamua kupitisha.
 
Huu mradi utakuwa mkubwa sana, ninacho hofia ushindani wa bandari ya bagamoyo kama wao watakuwa ndiyo wanao kuja kuiendesha wachina wanapiga kazi kweli kweli halafu ni wajanja wajanja sana, tutaweza kuja kushindana nao na bandari yetu ya Dar?

Utaogopa kushindana hadi lini
 
Aseme nini kilimfanya agomee mwanzo,na sasa amekubali kwa sababu gani. Isije ikawa alirukwa kwenye mgao mwanzo, na sasa kawekewa fresh ameamua kupitisha.
Huu ugomvi sasa, haina haja as long as mradi umeanza
 
Nimeangalia kipindi Azam Tv wanaonyesha namna ya huu mradi utakavyo kuwa, yaani Tanzania haitatumia hata sent tano...

Lakini Magufuli alisema huu mradi ni wakinyonyaji na haufai kutekelezwa lakini leo nimeona kwenye kipindi Azam Tv wakisema mradi utaanza kutekelezwa..

Ni kweli huu mradi wa kinyonyaji utatekelezwa?
Kwa hiyo ?
 
Back
Top Bottom