Mradi wa bandari Bagamoyo pamoja na Magufuli kusema ni wakinyonyaji lakini unatekelezwa!!!

Mradi wa bandari Bagamoyo pamoja na Magufuli kusema ni wakinyonyaji lakini unatekelezwa!!!

Katika vitu vichache ninavyoweza kukubaliana na Magufuli ni habari za kusimamisha huu mradi.

Akishindwa hili nitamuona anashindwa kitu muhimu sana.
 
Unaweza kukuta alipiga mkwara maana JK na genge lake ndio walipata 10% yao, ila kwa sasa na yeye si ajabu kapatiwa 10% yake hivyo anapitisha kimya kimya. Uzalendo hauna ubavu mbele ya 10%.
“Eti unaweza kukuta”, Kwahiyo unataka tujadili hisia zako! Umaandazi huu sasa.
 
Jukumu la bunge ni kuiweka serikari accountable ajabu nchi inaingia mikataba ya maliasili au miradi mikubwa bunge halijua terms zenyewe.

Unafanya vipi checks zako za serikari wakati hujui matendo yake na athari zake, bunge sio mahala pakujadili madarasa, sijui visima vinavyojengwa na kupitishia sheria only; serious matters of the nation are also debated too.

Mpaka sasa inaonekana hakuna mmbunge ata mmoja inaonekana anaejua serikari imesaini mikataba gani.

Civil servants wanaowanyima hizo access ya kuona maidhui ya yaliyomo kwenye hiyo mikataba hawana uhalali wa kufanya ivyo wao nao kawachagua kuendesha nchi kwa niaba ya watanzania.

Raisi ndio aliepigiwa kura na wabunge kwa niaba ya wananchi.

Ni wakati sasa wabunge kusimamia serikari kama wajibu wa sheria unavyotaka na kulazimisha kuona details za hiyo mikataba.

Huu mradi tusiojiongopee unakuja kwa sababu yetu (sio kwamba mmbaya kwa taifa) bali ukiangalia tu main investors ni Oman ambao port yao ni transit ya goods shipped to Africa from Asia na China ambao ni main suppliers wa bidhaa zao kwa Africa. Lazima kuna strategic plan yao tofauti na sisi tunavyofikiri ni zawadi.

Kwa ivyo where do we fit in this project what if China akiamua bidhaa zao zote zinazotoka maeneo ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Zambia na Malawi; zitapitia Bagamoyo what is the opportunity cost ya Dar? Au wazungu wakiona port ya Bagamoyo more efficient Bandari zetu zinaathirika vipi na mapato ya serikari in terms of mizigo inayotoka kwenda nje uwezi mlazimisha mteja atumie bandari zako by force.

Hili swala sio simple tu kama tunavyolichukulia ya kuwa kuna bandari ya bure inakuja ni lazima kujua jinsi hiyo bandari itakavyojilipa, impact yake kwa incoming and outgoing of goods kwa bandari zetu zingine, faida ya economic zone kwetu na multiplier effect zingine.

Kwa sababu hiyo bandari dalili zote zinaonyesha ni kwa strategy zao lazima tuelewe zaidi sisi tunanufaikaje in the bigger picture lazima ujue long term plan za mwenzako hili uweze kufanya risk assessment zako appropriately na kwa kutumia wataalamu wa serikari lazima mtu uwe na wasiwasi.

Sisemi kwamba labda mimi najua sana hila hata kwa elimu yangu ndogo nina uhakika naweza mgalagaza mtaalamu yeyote wa serikari including PhDs kwenye mjadala wa biashara na uchumi. Now that is a reason enough ya wajuaji zaidi kushinda watu kama mimi kutaka kuona ni kitu gani serikari inaji commit nacho na ku debate angle zote.
 
Ukishaweka maamuz hadharani........ni vyema ukiamua vinginevyo urud tena hadharani kuongea na hadhara kuwapa feed back

Ameshagundua nia zenu sio njema. Vikinoga hampongezi lakini kukiwa na utata tu mnakuja na mauzi. Kila mtu afanye kazi yake.
 
Nimeangalia kipindi Azam Tv wanaonyesha namna ya huu mradi utakavyo kuwa, yaani Tanzania haitatumia hata sent tano...

Lakini Magufuli alisema huu mradi ni wakinyonyaji na haufai kutekelezwa lakini leo nimeona kwenye kipindi Azam Tv wakisema mradi utaanza kutekelezwa..

Ni kweli huu mradi wa kinyonyaji utatekelezwa?
Unatekelezwa kwa masharti yapi ndio unaweza kusema ni wa a kinyonyaji au sio wa kinyonyaji .
 
lazima ijengwe,hata kama tutatoa pesa na sisi ikibidi tule nyasi,lazima ijengwe,kikwete oyeeeeee
 
Huu mradi utakuwa mkubwa sana, ninacho hofia ushindani wa bandari ya bagamoyo kama wao watakuwa ndiyo wanao kuja kuiendesha wachina wanapiga kazi kweli kweli halafu ni wajanja wajanja sana, tutaweza kuja kushindana nao na bandari yetu ya Dar?
Itawasaidia kuleta ushindani ushindani uchochea maendeleo na ufanisi
 
Itawasaidia kuleta ushindani ushindani uchochea maendeleo na ufanisi
Hii serikali inaweza ushindani kweli kama tumeuwa shirika la Fastjet ili tubaki sokoni na shirika moja tutaweza kuja kukimbizana na hawa wachina?
 
Hii serikali inaweza ushindani kweli kama tumeuwa shirika la Fastjet ili tubaki sokoni na shirika moja tutaweza kuja kukimbizana na hawa wachina?

Mswahili hawezi fanya chochote chenye manufaa kama hata sasa hawawezi compete na mombasa au beira ndo wataweza na wachina
 
Itawasaidia kuleta ushindani ushindani uchochea maendeleo na ufanisi
Bandari nyingi husaidia uchumi kukua mfano South Africa wana Bandari kubwa Nne Capetown, East London, port Elazabeth na Darban kila Bandari ina majukumu yake, Mfano Bandari ya Darban ni kuhudumia Nchi jirani ni Bandari ya kimataifa na Capetown ni watalii na mizigo ya ndani zaidi sanjari na Bandari zingine zao, Hata Tanzania tunaweza kuiteua Bandari ya Dsm ikatumika kwa mizigo ya nyumbani pekee na kupokea meli za mafuta na pia kusafirisha mizigo ya nyumbani sanjari na Bandari ya Tanga na Mtwara pia ijengwe Bandari ingine Lindi Taifa liwe na Bandari nyingi kubwa meli zimiminike Nchini, Hiyo Bandari ya Bagamoyo ndiyo iwe ya kimataifa ihudumie Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Congo, Uganda na hata msumbiji na hata kenya kwani Mbona watanzania hutumia Bandari ya kenya kusafirisha mizigo yao.
 
Wajenge Bandari Bagamoyo wapunguze foleni na msongamano wa magari ya mizigo Bandari ya hapo Dsm pia hata Bandari ya Zanzibar ipanuliwe ijengwe upya iwe ya kisasa ili meli kubwa zipate kutia Nanga Taifa liwe la mabandari makubwa kibao meli ziamiminika kwa wingi na kuleta maendeleo kwa kasi kubwa
 
Bandari ya Dar bado ni ndogo kuhudumia meli nyingi hadi zinapaki bahari mda mwingi hali zatakiwa zifike na kupakua ziondoke.Tukiwa na bandari ya bagamoyo itapunguza haya
 
Itawasaidia kuleta ushindani ushindani uchochea maendeleo na ufanisi
Bandari ya Dsm itabakia kuwa Bandari ya meli za mafuta na mzigo ya ndani ya Nchi hizo Bandari zingine zitakuwa za kimataifa Nchi jirani
 
Bandari ya Dar bado ni ndogo kuhudumia meli nyingi hadi zinapaki bahari mda mwingi hali zatakiwa zifike na kupakua ziondoke.Tukiwa na bandari ya bagamoyo itapunguza haya

Hii ndiyo kero sana, wamiliki wa Meli hawaipendi Bandari ya Dsm kabsa wanadai meli huchukua mda mrefu kwenye foleni majini, hata upakuaji na upakiaji wa mizigo ni slow slow sana na pia zile Meli kubwa Duniani haziwezi kutia nanga kutokana na kina kifupi cha maji, kwa kifupi Bandari ya Dsm sasa ni kabandari ka kizamani hakopo kisasa kapo kichochoroni sana.
 
Back
Top Bottom