Jukumu la bunge ni kuiweka serikari accountable ajabu nchi inaingia mikataba ya maliasili au miradi mikubwa bunge halijua terms zenyewe.
Unafanya vipi checks zako za serikari wakati hujui matendo yake na athari zake, bunge sio mahala pakujadili madarasa, sijui visima vinavyojengwa na kupitishia sheria only; serious matters of the nation are also debated too.
Mpaka sasa inaonekana hakuna mmbunge ata mmoja inaonekana anaejua serikari imesaini mikataba gani.
Civil servants wanaowanyima hizo access ya kuona maidhui ya yaliyomo kwenye hiyo mikataba hawana uhalali wa kufanya ivyo wao nao kawachagua kuendesha nchi kwa niaba ya watanzania.
Raisi ndio aliepigiwa kura na wabunge kwa niaba ya wananchi.
Ni wakati sasa wabunge kusimamia serikari kama wajibu wa sheria unavyotaka na kulazimisha kuona details za hiyo mikataba.
Huu mradi tusiojiongopee unakuja kwa sababu yetu (sio kwamba mmbaya kwa taifa) bali ukiangalia tu main investors ni Oman ambao port yao ni transit ya goods shipped to Africa from Asia na China ambao ni main suppliers wa bidhaa zao kwa Africa. Lazima kuna strategic plan yao tofauti na sisi tunavyofikiri ni zawadi.
Kwa ivyo where do we fit in this project what if China akiamua bidhaa zao zote zinazotoka maeneo ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Zambia na Malawi; zitapitia Bagamoyo what is the opportunity cost ya Dar? Au wazungu wakiona port ya Bagamoyo more efficient Bandari zetu zinaathirika vipi na mapato ya serikari in terms of mizigo inayotoka kwenda nje uwezi mlazimisha mteja atumie bandari zako by force.
Hili swala sio simple tu kama tunavyolichukulia ya kuwa kuna bandari ya bure inakuja ni lazima kujua jinsi hiyo bandari itakavyojilipa, impact yake kwa incoming and outgoing of goods kwa bandari zetu zingine, faida ya economic zone kwetu na multiplier effect zingine.
Kwa sababu hiyo bandari dalili zote zinaonyesha ni kwa strategy zao lazima tuelewe zaidi sisi tunanufaikaje in the bigger picture lazima ujue long term plan za mwenzako hili uweze kufanya risk assessment zako appropriately na kwa kutumia wataalamu wa serikari lazima mtu uwe na wasiwasi.
Sisemi kwamba labda mimi najua sana hila hata kwa elimu yangu ndogo nina uhakika naweza mgalagaza mtaalamu yeyote wa serikari including PhDs kwenye mjadala wa biashara na uchumi. Now that is a reason enough ya wajuaji zaidi kushinda watu kama mimi kutaka kuona ni kitu gani serikari inaji commit nacho na ku debate angle zote.