Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Alafu ujenzi ukiisha?

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
currency itakayokua inatumika kwenye kutolea mizigo nahuduma zote kwa hyo bandar kwa nchizote 8 itakua ni tsh itaimarisha shilingi yetu,
TRA watapata import tariffs nyingi zaid compare nasasa hiv
jumlishia na eneo tuliopo kua tumezungukwa na land locked country nyingi hata stability ya uchumi wa nchi zajiran utakua unatutegemea sis zaid.
hio bandar itakua nafaida myingi mno
 
Kuna mtu huwa anatoa hoja nzito za kujadili. Tusimpuuzee kwa misimamo yetu ya kisiasa. Huyu hapa:
 
Hiyo gesi asilia sisi tunapata nini? Kama hatupati kitu Kuna haja gani ya kuwapa na bandari?
Wabunge wako wa ccm waliupitisha mswada wa kuvuna hiyo gesi usiku wa manane kule Bungeni, tena kwa hati ya dharura! Wakati huo Rais alikuwa ni JK, na JPM alikuwa ni mmoja wa Mawaziri!

Sasa kama hampati kitu, mimi hainihusu. Maana ninacho amini ni kwamba, chini ya utawala wa ccm! Kila kitu ni ubatili, wizi na ufisadi!
 
View attachment 1745616
Wandugu, sasa ni muda muafaka wa kurejesha ule mradi wetu mkubwa wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa maslahi mapana ya kiuchumi na kwa faida za kichumi.

Yafanyike maandalizi mapema na washirika wote wakae katika mazungumzo ili hatimae mradi uanze kazi mara moja.

Ikumbukwe mradi huu ukikamilika utakuwa ni miongoni mwa miradi mikubwa sana Afrika Mashariki na utaleta manufaa makubwa sana siyo tu kwa watanzania na watu wa ukanda wa Pwani bali pia hata nchi jirani zitanufaika.

Habari sijui za kusema mradi utaua bandari ya Dar es salam hazina mantiki kabisa kwa sasa. Tusonge mbele tujenge taifa letu.

Pia soma: Kilichobadilika katika mradi wa bandari ya Bagamoyo ni miaka tu vingine vipo sana tofauti na wanavyojitapa

We mwezi tu huna jipya
 
Kila kitu kinazungumzika.
bandari ya bagamoyo ina Mambo mengi sana.viwanda, apartments,mahotel,n.k n.k.
Walikuwa wapi kipindi choote cha kuanza wakati wa jk.
Mladi ufe,mama samia ahangaike na URITHI wetu.hiyo ambayo mikataba haikuinguwa tyachane nayo.
 
Miaka 99 kwa mchina bila kulipa Kodi? Big no
Yaani miaka 50 nchi haichukui Kodi, haiendelezi bandari nyingine, haina mamlaka ya kuhoji na kukagua vitabu vya mapato na matumizi vya mchina.
BIG NOOOOO
Wanao unga mkono huo mradi ni either hamnazo au watu wa Bagamoyo tu, sasa wameingia na wagogo wa Dodoma, the rest tunasema BIG NO kwa mradi wa Bagamoyo
 
Wanao unga mkono huo mradi ni either hamnazo au watu wa Bagamoyo tu, sasa wameingia na wagogo wa Dodoma, the rest tunasema BIG NO kwa mradi wa Bagamoyo
Achana na Hio Miaka.. ati serikali Ifanye Excavation ambayo ni zaidi ya 1T

Wanahitaji Mandate ya kwamba hio Ardhi inakuwa kama yao Mazima.

Vitabu vyao vya Mapato havitakiwi Kuguswa wala kufuatiliwa.

Pia wakaweka na kifungu kwamba ikiwa Mradi Overall utakuwa na Hasara Basi Serikali Ifanye Compensation.

Unajiuliza.. Hawaruhusu Serikali ikague Mapato yao.. How would the government find out kwamba they are gaining or Losing?

Anyway... Naendelea Kupitia Ripoti yao.. Nije na Nondo zaidi.
 
Narudia, wote wanaoungamkono huo MRADI ni either HAMNAZO kichwani au ni watu wa Bagamoyo, sasa Wagogo nao wameingia. Bagamoyo residence mnataka kuingiza nchi kwenye matatizo makubwa hivyo kwasababu ya ajira za kuwapikia vitumbua Wachina????
 
Bagamoyo karibu na ulaya kuliko dar.
Walikuwa wapi kipindi choote cha kuanza wakati wa jk.
Mladi ufe,mama samia ahangaike na URITHI wetu.hiyo ambayo mikataba haikuinguwa tyachane nayo.
 
Nyinyi mlilishwa matango pori na mwendazake, mkakubali ku-swallow a line, hook and the sinker without questions asked - mna zero kwenye issue moja tu eti wachina hawati kulipa kodi for almost half a century - kuna ukweli gani kwenye madai hayo na ni kodi gani wanayo isema hapa?

Yaani Watanzania tunakubali kopoteza mradi mkubwa wa aina yake barani Afrika, mradi ambao ungehusu mpaka ujenzi wa viwanda vya kisasa pamoja na high technology village kwa ajili ya utafiti na uundaji wa mashine na products nyingi za teknolojia mpya - badala ya kuchangamukia fulsa sisi tunajiingiza kwenye malumbano yasio na tija kwa Taifa letu, wenye uhitaji ni sisi sio Wachina tukiwazenguwa wanakwenda kuwekeza kwingine kwa nini wapoteze muda wao watu ambao hawajui wanataka nini hasa - kaeni na pori lenu la Mbegani likiwa dormant tuone lita generate revenue kiasi gani likiwa halitumiki.

Watupe mkopo wa pesa tujenge wenyewe kwa kutumia wakandarasi of our choice na tuendeshe wenyewe kila hatua bila kuingiliwa!

Mkopo with zero conditions!
 
Tulitakiwa tutafutiwe huo mkataba uwekwe jamvini wadau wauchambue watoe maoni , hilo la kusema eti mkataba miaka sijui 100, sijui 99, mara 50 , na mengine meeengi aliyasema jiwe ili ku win popularity kuwa ulikuwa wa kishenzi sidhani kama ukweli ndio uko hivyo maana JK ametukanwa sana kwenye hili na hajawahi kutokeza hadharani kulisema ameishia kuambiwa anawashwawashwa tu, tungeuona ndio tungejua mbivu na mbichi, imagine mkataba haujulikani then mtu mmoja ndio anatoa madai kuwa ulikuwa wa hovyo, tusikimbilie vya kuambiwa huo mkataba uletwe wenye akili wauchambua full stop, inawezekana hata haukuwa mbaya ni Chato tu ndio ilikuwa focus ya Jiwe na sio kingine hapa nchini
 
Kwa hii comment pekee inatosha kabisa kuhitimisha huu mjadala
 
Sijamsikia Ndugai, anasema Rais alishauriwa vibaya au alidanganywa kuhusu mkataba wa ujenzi wake?. Nilimsikia Rais Magufuli alichoeleza kama hakudanganwa ndiyo kilichomo katika mkataba ule. Ndugai alipaswa kushauri nchi ikae mezani tena kukubaliana na wachina upya na kurekebisha baadhi ya makubaliano ya mradi huo.
 
Watupe mkopo wa pesa tujenge wenyewe kwa kutumia wakandarasi of our choice na tuendeshe wenyewe kila hatua bila kuingiliwa!

Mkopo with zero conditions!
MFANO UNA NYUMBA LA MITI NA UDONGO PALE KARIAKOO LINAKARIBIA KUANGUKA KABISA! HALIKUINGIZII KIPATO CHOCHOTE YAANI JUMBA LIPO LIPO TU KAMA PAGALE NA UWEZO WA KUJENGA HUNA NA WALA HAUTEGEMEI KUPATA UWEZO. THEN

ANAKUJA MHINDI AU MWARABU ANAKWAMBIA TUFANYE MKATABA WA NYUMBA YAKO HII TUNAIJENGA UPYA GHOROFA 20 NA FREMU 12 WEWE UTAPATA FREMU MBILI NA FALAT MBILI ZENYE APARTMENT 4. ZILIZOBAKI YOTE NI YA KWANGU KWA MUDA WA MIAKA 5O GOROFA LOTE LITAKUWA NI LA KWAKO PAMOJA NA FREMU ZA MADUKA

WEWE UNAMWAMBIA SITAKI MKATABA HUO KAMA VIPI NIPE MKOPO NIJENGE GOROFA LA KWANGU KWA KUTUMIA MKANDARASI WANGU!!! IVI APO UTAKUWA MZIMA KWELI? AMA ITABIDI UPIMWE AKILI? MWARABU GANI ATAKAEKUBALI HILO?
 
Kusitishwa kwa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na falsafa ya, "Quis Custodient, Ipsos Custodes."

Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulisitishwa kufuatia majadiliano yenye tija yaliyofanywa mwaka 2018. Serikali ilibaini masharti magumu yanayoweka rehani uchumi wa nchi na kuhatarisha uhuru wa nchi yetu. Kwa mantiki hii wajuvi wa mambo katika mimbali za "Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi" watang'amua na kuunga mkono zuio hilo la serikali.

Kupitia majadiliano hayo yaliyojikita katika viunga vya ujasusi wa kidola na kiuchumi, serikali ilibaini baadhi ya masharti yafuatayo ambao ni hatarishi kwa uchumi wetu;

1) Wachina walihitaji kuendesha Bandari hiyo baada ya ujenzi bila kuingiliwa, jukumu la kupanga bei liwe mikononi mwao.

2) Pia ukanda huo wa Bandari ya Bagamoyo ( Tanga-Mtwara), kusiwe na uboreshwaji wa Bandari zingine, mathalani Bandari za Tanga, Dar es Salaam, Mafia na Mtwara zibaki kama zilivyo kitu kinachohatarisha ukuaji wake na kwa namna yoyote ile zingekufa kifo cha asili.

3) Eneo lote la ujenzi wa viwanda na mji wa kisasa wachina walihitaji umiliki wa hati kwa zaidi ya miaka 33 (zaidi ya miongo mitatu). Mbaya zaidi walihitaji kama Faida yao itakuwa haijapatikana kwa miaka 33 basi hata kwa miaka 99 wangeweza kuendelea kumiliki na kukusanya kodi.

4) Wachina walihitaji pia wawe wasajili, wasimamizi wa viwanda vyote vitakavyowekezwa eneo hilo sanjari na ukusanyaji wa kodi zote zitakazolipwa eneo huska.

Sintofahamu inaongezeka pale ambapo, ni wachina hao hao ambao wangetumika kutoa tafsiri ya kimahesabu kuhusu faida au hasara kutokana na 100% ya kumiliki au kuratibu mchakato mzima wa mapato katika eneo hilo. Hapa nalazimika kukumbuka usemi wa kiratini, "Quis Custodient, Ipsos Custodes?" Kwa tafsiri isiyo rasmi ni, "Who watches the watchers?" Au "Nani atawalinda walinzi wetu," ilihali wenye mali tumewekwa kando na wageni wamepewa fursa ya kufanya wanavyotaka.

Katika viunga vya ujasusi wa kidola na kiuchumi kwa namna yoyote ile lazima wachina wangetuchakachua ili watuvune vya kutosha. Maana wao ndio wangekuwa walinzi wa 100% wa mapato yanayoingia na hata kampuni za ukaguzi ili ionekane wamepata hasara ili kupata tiketi ya kuongezewa muda wa kumiliki na kukusanya mapato.

Aina hii ya makubaliano kandamizi ndio imepelekea Bandari ya Hambantota, Sri Lanka kuchukuliwa na kumilikiwa na China kwa 99%. Pia Uwanja wa Ndege wa Mattala Rajapaksa, Sri Lanka kumilikiwa na China kwa 70%. Ikiwa ni zao la kushindwa kulipa mikopo iliyotegwa katika mtego wa falsafa za "Quis Custodient, Ipsos Custodes."

Rejea andiko lililoandikwa na Institute for Security Studies Africa mwaka 2017 lenye kichwa cha habari, "Lessons from Sri Lanka on China's 'debt-trap diplomacy."

Aidha, rejea andiko ambalo liliandikwa na The Diplomat mwaka 2017 lenye kichwa cha habari, "Sri Lanka's Debt and China's Money," sanjari na andiko la mwaka 2018 lenye kichwa cha habari, "Does Debt Pay? China and the Politics of Investment in Sri Lanka."

Nawiwa kuwaomba watanzania wenzangu kuyatafta maarifa ambayo yamefichwa katika Vitabu au maandishi ili kubaini propaganda zinazofanywa na baadhi ya watu kutetea mradi wa Bagamoyo uendelee kwa maslahi binafsi paspo kuutizama ukweli kwa maslahi mapana ya taifa.

Aidha, niipongeze serikali ya awamu ya 5 kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu katika viunga vya ujasusi wa kidola na kiuchumi. Hii ni zaidi ya tafakuri tunduizi ya kukataa makubaliano yanayotweza utu wa Taifa letu, kupoka Uhuru wa nchi na kuweka rehani uchumi wa nchi yetu kwa faida ya China.
 
Magufuli ameshaondoka! Tutaurudisha tu ule mradi. Kodi itakayo patikana, itatumika kuboreshea huduma mbalimbali za kijamii. Mtake msitake. Ccm ni ile ile.

Mbona gesi asili mmewapa! Iweje muwanyime hiyo Bandari?
Hakuna kodi
 
Kwani why mnakomaa sana na wachina .?
Kama tunaihitaji sana iyo Bandari kwanin asitafutwe basi mwekezaji yeyote kwa terms ambazo sio za kinyonyaji!?

Mmekula down payment ya Mchina eeh !???
 
BANDARI YA BAGAMOYO AKA MBEGANIZHOU YA WACHINA.

BANDARI YA BAGAMOYO HAITAJENGWA NA WACHINA KWA MKOPO
WANAJENGA MALI YAO WENYEWE
MALI YA CHINA NDANI YA TANZANIA KWA MIAKA 99
HAKUNA MTANZANIA ATARUHUSIWA KUINGIA PALE KUFANYA LOLOTE PALE MBEGANIZHOU YA BAGAMOYO..

Nilichogundua huo mradi wa bandari ya Bagamoyo ni DO OR DIE PROJECT kwa wachina na SERIKALI yao hakuna NCHI yeyote inaweza kubali MKATABA wa AJABU na wa KITAPELI WA KUTOA ARDHI YAKE NZURI NA KUBWA KIASI KILE IWE MALI YA CHINA ni TANZANIA PEKEE
KWAHIYO WACHINA WATAFANYA LOLOTE LINALOWEZEKANA KIHAKIKISHA MRADI HUO WA KIJAMBAZI UNAFANIKIWA

Swali la kizushi Makada, hivi kabla ya Bagamoyo kuwa China itapigwa kura Bungeni kupitisha au ? taratiibu zikoje? Najiuliza kama ni hivyo je wakipitisha hilo Wabunge watakuwa wamewatendea haki WANANCHI? kiasi Cha kurudi kifua mbele 2025 kuomba kura? Je Chama kina msimamo gani juu ya hii biashara kichaa?
 
Back
Top Bottom