Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Yale ya kusema mikataba ni ya siri yasiwepo, watuwekee hapa kila kitu labda tutaelewena, ila swala la mtu kukodi sehemu kwa miaka 99 au 50 na kutaka asihojiwe, asilipe chochote na tumwache afanye atakalo kwa miaka yote hiyo kwa kweli hata mtu asiyekuwa na akili hawezi kukubali..
hata kichaa haez kubali hata mtoto alie tyumbon hawez kubali huo upuuz!
 
Sijui nilini tutaelimika kutoka kwenye huo wehu wakushikiwa maskio kifala ivo,

kwanza ujenzi wa mradi utacost dollar billion 10, means zaid ya trillion 23 zaujenzi zitaingia kwenye mzungo wetu wahela kupitia ajira zitakazopatikana kutokana naujenzi huo, mfano manunuzi ya cement nondo navifaa vingine vyaujenzi. ajira nyingi sana itapatikana wakat waujenzi nanyingi zaid baada ya ujenzi kukamilika, serikali watakusanya kodi PAYE kwaviwanda vitakavouza material za ujenzi na zawatu wakatakaokua wameajiriwa

sawa tutakosa ushuru waforodha vip tozo nyingine ambazo tutapata zinaweza kuanyingi kias gani kwaukubwa wahio bandari??

imagine labda currency itakayokua inatumika kwenye kutolea mizigo nahuduma zote kwa hyo bandar kwa nchizote 8 itakua ni tsh itaimarisha shilingi yetu kias gani??
 
aliyekuwepo hakutaka mazungumzo.
Sababu sio kwao
Wangekuwa na nia ya win win situation kwanini wasifanye hayo kipindi kile?Waje kukubali kujadiliana baada ya kuona kitumbua kimeingia mchanga?Mchina hawezi fanya biashara ambayo kamwe haiwezi mlipa na kamwe hawezi kwambia biashara imemlipa.Atakwambia tu anakusaidia ila anapata hasara.[emoji23][emoji23]
 
Naona watu wenye vijiplot vyao huko ndio wanatetea huu mradi aisee. Kweli hapa ndio nimeamini hata kipindi cha kupigania uhuru kuna waafrika walikuwa upande wa wakoloni.
 
Miaka 99 kwa mchina bila kulipa Kodi? Big no
Hilo la miaka 99 , bila ya kulipa kodi halina ushahidi.. Yalikuwa maneno ya mwendazake... Kwa akili ya kawaida , uwekezaji wowote mkubwa .. Unahitaji muda kwa aliyewekeza kurudisha hela aliyowekeza..... Swala la kuuliza , je bandari nyingine duniani wanafanyaje? Nakumbuka pale mlimani city tu, wawezekaji wanahitaji 50 years , baada ya hapo ndio umiliki uende serikalini.. Kuna namna ya kufanya kwenye mradi wa Bagamoyo...
 
Hapana bora tuendelee na ule wa Tanga ndio unatija kubw sana hata wanaoitumia Dar port wana aafiki kuikuza ya Tanga kwa kurahisisha huduma kwa pande za Rwanda,Burundi,Congo yachini , hata Uganda pia.
 
kunduch pale hivi kwanin isiwepo bandar kubwa sana na samak wapo pale.
 
Ni yale yale tunayosema. Mama Samia anakuwa kama vile katoke nje ya serikali iliyopita! Kuwachekea wawekezaji itatu-cost! Kukataa kwa mradi wa Bagamoyo wenye masharti kibao yalioitwa "sawa ya mwenda wazimu" ni kuturudisha kulekule - kwenye deal na kupoteza raslimali zetu!
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo
Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena

Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99
 
Naona spirit ya JAkaya inalead nchi Sasa! JPM alizungukwa na wanafiki Class A
 
ndiyo maana wengine wanaamini kuwa huenda hiyo bandari na wachina ndiyo ilikuwa dhamana ya Rais kwa kijana wake baada ya kukamatwa Hong Kong na madawa!

Wala hujakosea,inawezekana Wachina bado wamemkaba mdeni wao atimize ahadi yake
 
Mawazo kama haya yataamfanya hata mama aidharau Jamii Forum
Hivi hujui kama tukimzingua tutazinguana.
Kumbuka she is the most informed person in da country.
Jengeni hoja za kueleweka
 
Back
Top Bottom