Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,753
Kwani tatizo liko wapi kaeni na pori lenu la Mbegani mfugie swala na chatu kama mnadhani maendeleo ya kutuletea viwanda na Bandari ya kisasa havina maana.Sema tu mkuu kama uliahidiwa Ka pasent Fulani
Huo mradi ni watu wasiojua umhimu wa nchi Yao na athari zake
J.K ni binadamu ambaye ni bingwa kwenye masuala ya diplomasia na ana heshimika sana Duniani, sasa kawaleteeni mradi mkubwa wa uwekezaji katika ujenzi na uendeshaji wa Bandari kubwa in eastern and southern Africa - nyie mlimpiga vita kwa kuwasingizia Wachina kwamba lengo lao ni kutuibia - zikapigwa propaganda lukuki kupitia vyombo vya habari nchini hasa TV na magazeti jinsi wachina walivyo kuwa wamepania kupiga mnada Taifa letu kupitia ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo! Propaganda hizo zilifanikiwa sana mpaka baadhi ya wananchi wakaingia laina na kuanza kuwasema sema wachina kwamba ni wezi, hawafai, kumbe ni ulaghai mtupu.
Propaganda hizo zenye walakini mkubwa Taifa letu likajikuta linapoteza mradi/investment ya maana kutokana na propaganda za kupikwa tu - mladi initiator ni Mh. Jakaya Kikwete basi watu wenye nia ovu wakapania kuupiga chini na kutunga adithi za kufikirika tu kuwazuga Watanzania ili wawasingizie Wachina kwamba ni wezi na walaghai, tunayasema hayo wakati mwaka jana nilimuona na kumsikia JPM akimuomba/sihi waziri mkuu wa China aliye tembelea Tanzania kwamba Serikali ya China isamehe Deni la ujenzi wa TAZARA, reli iliyo jengwa zaidi ya miaka hamsini iliyo pita kwa gharama ya matrillion ya TShillings , mpaka leo hatujawahi kuwalipa Wachina hata senti tano ya mkopo wao, vivyo hivyo mkopo wa ujenzi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki - sasa kati ya yetu na Wachina walaghai ni akina nani?
Tumekalia mantra ya kuwasema vibaya Wachina kwamba ni wezi,wezi.
Ni suala la muda tu tutajikuta tunarudi kule kule kwa Wachina kuwabembeleza waje kutukamilishia ujenzi wa reli katika sections zilizo baki za SGR tena kwa mkopo wa riba nafuu yanarudi yale yale ya ushauri/maoni ya Mh. Jakaya Kikwete.