Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Huu mradi umekaa kinyonyaji sana, labda contract wepewe watu wengine sio wachina halafu conditions za mradi zipitiwe tena upya kwa maslai mapana ya taifa.
 
Hatuwezi kujua kama aliyosema ni ya kweli.
Hakuwa mtu wa kuaminika sana katika yale aliyozungumza.
Kama aliyoyasema Hayati JPM juu ya huu mradi ni ya Hakika kwakweli HAPANA acha tuendelee na ile ya kimkakati aliyoiacha ila kama terms zitabadilishwa na kuwa win win situation hapo SAWA.
 
Yaani miaka 50 nchi haichukui Kodi, haiendelezi bandari nyingine, haina mamlaka ya kuhoji na kukagua vitabu vya mapato na matumizi vya mchina.
BIG NOOOOO
Waulize baada ya iyo miaka iyo bandari itakua kwenye hali gani wakati wanatukabidhi.....
 
Hivi unaelewa sharti moja lililopo kwenye mkataba huo ni kuwa hautaruhusiwa kukusanya kodi wala kufanya ukaguzi kwenye huo mradi mpaka pale mda uishe au mpaka wapate faida.

Sasa huo si ujinga kama siwezi kufanya ukaguzi ntajuaje kama umepata faida.
 
mkuu wachina sio watu Pakistan wanalia,congo wanalia, kenya wanalia zambia wanalia hizo sample ukipata muda jionee miladi waliyofanya huko ni dhuluma kubwa
Ila mmarekani ndio mtu
 
Sasa hapo, bandari ya dar itakufa, ni bora serikalini ipate share angalau 40%
Mkuu, mbona hilo linazungumzika ni kiasi cha kukaa chini na kuelewana - wala sidhani kama Wachina wangeshindwa kutoa gawiho kiasi na kuipatia Serikali kila mwezi including ulipaji kodi - bandari ingefanya kazi in parallel na Bagamoyo kwa kuhudumia meli zenye uzito wa kati na sio zile ambazo ni Juggernuat - kina cha Bagamoyo kinaweza kubeba Meli zenye uzito wowote Duniani unlike Dar port.
 
Ndio mambo yaleyale ya waziri kuzuiwa getini
 
HATUITAMBUI MIKATABA YOTE ILIYOKWENDA KUSAINIWA CHINA.

Hii mikataba ipelekwe bungeni, bungeni likae kama kamati na lichambue kila kipengele tena iwe LIVE!

Huu si wakati wa kufichaficha mambo
 
Ndio mambo yaleyale ya waziri kuzuiwa getini
Kamati ya bunge ya maliasili na utalii ilizuiliwa kuingia Serengeti Grumet, na yule mzungu wa Oyster bay alieikata kamati ya LAAC mpaka baadhi ya wajumbe kulazimika kuruka ukuta.

Halafu hawa kwa unyenyekevu tunawaita wawekezaji
 
Tatizo ni fikira za kiumaskini na kukosa uthubutu, hili ni tatizo la viongozi na nchi nyingi za Africa

Penye watu 10, ni asili mia 2 tu Kati ya hao ndio huwa watu wa kuona furusa na kuona inawezekana hata kusipokuwepo msaada

Lakini asilimia 8 ya watu hao akiwemo na Mleta mada, hawana uamuzi na niwatu wenye fikra za kiumaskini na kusingizia watu kwamba Kwa nini huyu anazuia watu wakuleta ajira, labuda akifa ndio nitafanikiwa,

Tanzania ni Taifa lililosheheni furusa kila utapogusa, kilichopo ni uthubutu wa kufanya, viongozi wenye kutegemea msaada hawatufai hata kidogo!!

Viongozi wenye kugawa rasilimali zetu Kwa Mali kauli tena miaka miiingi kisa ni kutengeneza ajira, hao ni masikini wa kifikra na hawana uwezo wa kusimamia
Huo sio msaada ni agreement lakn by the way bandari ni muhim ila kuwe na usawa ktk mkataba pia
 
Back
Top Bottom