Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Yaani miaka 50 nchi haichukui Kodi, haiendelezi bandari nyingine, haina mamlaka ya kuhoji na kukagua vitabu vya mapato na matumizi vya mchina.
BIG NOOOOO
Hivi mlimwamini Magu kuhusu masharti ya huu mradi? Kumbe kuna watu walikuwa wanamwamini kiasi hiki?

Ukweli ni kwamba Magu ali exaggerate masharti terms za huu mradi. Tafuteni ukweli mtajua
 
Kila kitu kinazungumzika.
bandari ya bagamoyo ina Mambo mengi sana.viwanda, apartments,mahotel,n.k n.k.
Hata 50 nakataa katakata. Bandari ya Dar inalipa kodi kubwa ikitokea mradi wa Bagamoyo kukamilika Dar itakosa wateja na hela zote kwa Mchina wa Bagamoyo. Kwa hiyo tukae miaka 50 tukisubiri waachie hasara yote hii?

Kama wanataka tugawane 50/50 hapo sawa
 
Nani kakwambia ni Bandari isiyo na faida??? Kwa Unajua mradi wa Bandari ya Bagamoyo ulikuwa unahusisha mambo gani??? Au ndo tapeli wenu magufuli aliwalisha matango pori???

Hayo mambo yenye faida hawakuyaona kiasi cha kutupilia mbali? Kwa kifupi ni kuwa haukuwa na faida au impact yoyote kiuchumi, na kwa kipindi kisichojulikana.
Au wewe unaweza kutuambiwa kwa nini ulisitishwa zaidi ya sababu zilizotolewa na the late Magufuli?
 
No no no no no no no. Huo mradi utakuwa wa wachina miaka 99. Na inabidi bandari ya Dar na Tanga zisiendelezwe ili hiyo ya Bagamoyo iweze kuperform vizuri.
 
Mleta mada ulisoma masharti ya huo mkataba au kwa kuwa umeshiba visheti ndo unaamua kuropoka
Wewe ulisoma huo mkataba? Au ulilishwa matango pori na watu wanaowaza kizamani?

Je,best practice kwenye miradi ya namna hiyo iko namnagani? Kuna comparison ilifanyika?

Ule mradi ni muhimu sana kiuchumi kwa Tanzania na nchi nyingine 8 zinazotegemea Tanzania kama sehemu ya kupitishia mizigo yao.

Pamoja na nafasi yetu ya kijografia kuwa muafaka kuliko Kenya,bandari yetu inapitisha 20% tu ya mizigo kwenda nchi hizo 8! Wakati bandari ya Mombasa ikihudumia 80%

Hatuwezi kuendelea kuwaza kizamani na kutenda kizamani kwenye zama hizi. Lazima tusonge mbele na mawazo ya kijanja kwa kutekeleza miradi ambayo itatupatia competitive advantage.

Watu wanakujengea bandari ya kisasa ambayo imeunganika na industrial estates kibao kwa hela zao. Wewe hutoi hata thumuni,hata kama watakaa miaka 50,tatizo liko wapi? Wanacho chukua wenyewe ni port charges tu! Kodi zingine zote kama ushuru wa forodha unachukua wewe. Tatizo liko wapi?

Unadhani Dubai wamefanyaje kufika hapo walipo? Wangekuwa wanafikiri kizamani kama nyinyi wangefika hapo? Hebu acheni longolongo waarabu na wachina watujengee bandari yetu ya Bagamoyo.
 
Back
Top Bottom