Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Mradi wa bandari ya Bagamoyo urejeshwe haraka sana

Hivi mlimwamini Magu kuhusu masharti ya huu mradi? Kumbe kuna watu walikuwa wanamwamini kiasi hiki?

Ukweli ni kwamba Magu ali exaggerate masharti terms za huu mradi. Tafuteni ukweli mtajua

Nenda Zambia. Lakini kubwa zaidi huitaji hata kujua kilichomo ndani ya mkataba. The general principle for such economic investment is profit at any costs. So tell me Leo una mapenzi sana na wachina ehhhh
 
View attachment 1745616
Wandugu, sasa ni muda muafaka wa kurejesha ule mradi wetu mkubwa wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa maslahi mapana ya kiuchumi na kwa faida za kichumi.

Yafanyike maandalizi mapema na washirika wote wakae katika mazungumzo ili hatimae mradi uanze kazi mara moja.

Ikumbukwe mradi huu ukikamilika utakuwa ni miongoni mwa miradi mikubwa sana Afrika Mashariki na utaleta manufaa makubwa sana siyo tu kwa watanzania na watu wa ukanda wa Pwani bali pia hata nchi jirani zitanufaika.

Habari sijui za kusema mradi utaua bandari ya Dar es salam hazina mantiki kabisa kwa sasa. Tusonge mbele tujenge taifa letu.
Sikujua kwamba uwezo wako wa kufikiri ni mdogo kiasi hiki
 
Kwamba kwa muda wa miaka 99 hakuna mamlaka yoyote Tanzania inaruhusiwa kuona nini kinafanyika huko ndani ya Bandari. NO!.

Eti ukishindwa kulipa deni lao, wanachukua hiyo aridhi na Bandari zinakuwa ni mtaa mmoja wa China, kuingia pale uwe na viza n..k. Ujinga huu nani akubali?

Mleta mada usitake tuanza kilio cha kumlilia rais wetu upya.
 
Tatizo ni fikira za kiumaskini na kukosa uthubutu, hili ni tatizo la viongozi na nchi nyingi za Africa

Penye watu 10, ni asili mia 2 tu Kati ya hao ndio huwa watu wa kuona furusa na kuona inawezekana hata kusipokuwepo msaada

Lakini asilimia 8 ya watu hao akiwemo na Mleta mada, hawana uamuzi na niwatu wenye fikra za kiumaskini na kusingizia watu kwamba Kwa nini huyu anazuia watu wakuleta ajira, labuda akifa ndio nitafanikiwa,

Tanzania ni Taifa lililosheheni furusa kila utapogusa, kilichopo ni uthubutu wa kufanya, viongozi wenye kutegemea msaada hawatufai hata kidogo!!

Viongozi wenye kugawa rasilimali zetu Kwa Mali kauli tena miaka miiingi kisa ni kutengeneza ajira, hao ni masikini wa kifikra na hawana uwezo wa kusimamia
 
Yaani miaka 50 nchi haichukui Kodi, haiendelezi bandari nyingine, haina mamlaka ya kuhoji na kukagua vitabu vya mapato na matumizi vya mchina.
BIG NOOOOO
Pesa haipatikani kwa kodi tu. Kuna makato mengine mengi tu ambayo tunaweza kupata kwa gharama za huduma mbalimbali. Vilevile wafanyakazi watakaoajiriwa hapo watalipa kodi na soko la bidhaa zetu ghafi litaongezeka.
 
Acheni ufala, BAGAMOYO BANDARI HAIJENGWI.

Mimi niko TAYARI HATA boko haram au Alshabab waje TUMG'OE MTU.......!!!
 
Magufuli ameshaondoka! Tutaurudisha tu ule mradi. Kodi itakayo patikana, itatumika kuboreshea huduma mbalimbali za kijamii. Mtake msitake. Ccm ni ile ile.

Mbona gesi asili mmewapa! Iweje muwanyime hiyo Bandari

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ungenufisha Taifa letu sasa sana, nafikiri JPM for some strange reasons hakutaka Bandari mpya ijengwe pale Bagamoyo - hoja nyingi zilizo kuwa zina husu ubaya wa ujenzi wa Bandari zilikuwa zinawekwa chumvi mno zikiwa na lengo la kuhalalisha kuhujumu mradi wa Bandari ya Bagamoyo kiaina, kwa kukomoana tu.

Watu wenye akili timamu hawawezi kukataa mradi ambao ungejenga viwanda vya kisasa kuongeza ajira nyingi kwa vijana, mradi mkubwa wa kuhudumia nchi nyingi Afrika Nashariki, Afrika ya kati na kusini mwa Afrika - Wachina na wawekezaji wa Oman walitaka Bandari ya Bagamoyo ndio iwe HUB ya kusafirisha na kuingiza bidhaa nyingi Barani Afrika na ku-create employment - lakini JPM kaipiga chini kwa visingizio lukuki ili tuwaone Wachina wabaya na wezi kumbe hiyo si kweli hata kidogo, Wachina na Kikwete walikuwa na lengo zuri tu kuendeleza taifa letu kisayansi na kitekinolojia oh yes wachina walitaka kuongezea village/park ya sayansi na teknolijia sisi tunataka kuchezea shillingi kwenye tundu la choo, tunachezea a golden chance kwa kusingizia Wachina all sorts of vices as if wazungu ndio malaika.

Mama Samia fanyeni mazungumzo tena na Wachina ili mfufue tena mradi huu ambao utaleta tija kubwa kwa Taifa letu, husiwasikilize baadhi ya watu wenye chuki binafsi na Wachina, nasikia kampuni ya Oman imehamuwa kuwekeza bandari ya Lamu au Djibuti sisi huku watu wanaendeleza rivaly za kijinga - bandari hisijengwe Bagamoyo lakini International Airport ijengwe Chato, bandari na kivuko cha
Kwenda Lubondo vijengwe Chato, Wilaya ya Chato yenye population hisio zidi laki nne ijengwe Hosptali ya Rufaa kwa visingizio eti itakuwa Hospitali ya kanda ya ziwa na Bunge linakubaliana na hoja hizo za kitapeli yaani wakazi wa mkoa wa Kagera wanao fikia million sita walazimike kwenda Chato kutibiwa - mambo gani haya? Fufueni mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
 
Pesa haipatikani kwa kodi tu. Kuna makato mengine mengi tu ambayo tunaweza kupata kwa gharama za huduma mbalimbali. Vilevile wafanyakazi watakaoajiriwa hapo watalipwa kodi na soko la bidhaa zetu ghafi litaongezeka.
Yaani unatetea miaka 50 ya China kulitawala eneo letu Mbegani Bagamoyo bila kujua wanalalaje, wanaamkaje na wanafanya nini hapo, siyo??
 
Hivi mlimwamini Magu kuhusu masharti ya huu mradi? Kumbe kuna watu walikuwa wanamwamini kiasi hiki?

Ukweli ni kwamba Magu ali exaggerate masharti terms za huu mradi. Tafuteni ukweli mtajua
Tuwekee hapa huo ukweli tuujue
 
Na wewe unatetea 50 years ya mchina kushikilia eneo letu pale Mbegani, bila kujua wanalalaje, wanaamkaje, wanasafirisha vitu gani hapo, na mbaya zaidi, ni nchi yetu lakini eneo Hilo kulikanyaga ni Kwa ruksa ya J. kupitia msemaji wa serikali yake!!

Utumwa mwingine huu tunaukaribisha Kwa kujitakia
 
Hivi mlimwamini Magu kuhusu masharti ya huu mradi? Kumbe kuna watu walikuwa wanamwamini kiasi hiki?

Ukweli ni kwamba Magu ali exaggerate masharti terms za huu mradi. Tafuteni ukweli mtajua
Hii nchi imejaa mazwazwa sana kiongozi, bado kuna watu wanaamini kila kitu alichokuwa akikizungumza Jiwe ni cha KWELI
 
Back
Top Bottom