Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Mkuu hakuna cha winch wala winji ni porojo tu zile nipo eneo la mradi katika nafasi ya mfanyakazi wa JV hamna kitu &January angekuwa na akili na yule mwingine alieugua corona wangewauliza watanzania jamani eeeee ni nini kinaendelea hapa?wangewasikiliza nazani wasimamizi wa mradi wangefukuzwa kazi hapo hapo kuna madudu ya hovyo sana huku
Sababu zimetolewa nyingi sana na Waziri Makamba, lakini ipi ni ya kweli na ipi haina ukweli ???
 
Mkuu kwa sasa imeeditiwa, wakati tunapiga kelele watu waligeuza gia angani wakaiedit..
Mimi niliiongelea kwenye makala moja ila kama siku mbili mbele nilivyoingia PDF nikakuta kitu kingine. Ila ilielekeza kuboresha miradi kama Bwawa la nyumba ya Mungu, Kidatu, Mtera e.t.c na kulikuwa na specific amounts za investment na megawatts to be expected..

Ila kwenye ilani ya CCM 2015 -2020 imeongelewa
Mkuu, ili kupata taswira ya inakokwenda ni lazima tufahamu tulikotoka ili makosa yasijirudie.
Mimi nimekuuliza maswali machache kuhusu Power-Master-Plan 2025 ili niweze kufahamu ni lini ilitengenezwa, kwa kiwango gani ilitekelezwa kabla ya 2015, fungu lake ni kiasi gani na kufahamu ni kiasi gani cha umeme kingeweza kuzalishwa mpaka 2050.

Lilikuwa ni suala dogo tu, kunipa hata chanzo ili nitakafute mwenyewe. Ntashukuru ukinasaidia kupata vyanzo ili nijifunze zaidi.....
 
Mkuu kwa sasa imeeditiwa, wakati tunapiga kelele watu waligeuza gia angani wakaiedit..
Mimi niliiongelea kwenye makala moja ila kama siku mbili mbele nilivyoingia PDF nikakuta kitu kingine. Ila ilielekeza kuboresha miradi kama Bwawa la nyumba ya Mungu, Kidatu, Mtera e.t.c na kulikuwa na specific amounts za investment na megawatts to be expected..

Ila kwenye ilani ya CCM 2015 -2020 imeongelewa
Kumbe iliishia kwenye ngazi ya chama tu, na haikufika kwenye Interminsterial Technical Committee ???
 
Miradi kama hii haipimwi kwa financial viability. Kuna vigezo zaidi ya hivyo. Angalia kwenye nyanja za kiuchumi na kijamii. Kuna internal rate of return kubwa sana for time infinity.

CC: MALCOM LUMUMBA
Mkuu nakusoma vizuri kabisa, hili la kuangalia Financial Viability nimelizungumzia kule juu kwenye mradi wa Tennessee Valley Authority (TVA). Mahakama ya Juu ya Marekani (The US Supreme Court) ilizungumza kama ulivyoweka bayana hapa. Nikushukuru sana ndugu yangu kwa mchango wako mzuri ?
 
Kwenye aya za mwanzo kabisa za uzi wangu nimezungumzia GOVERNMENT MONOPOLY. Hebu naomba utueleweshe TANESCO's MONOPOLY inasababishaje tatizo la uhaba wa nishati ya umeme nchini na tutumiea mbinu ipi kulitatua tatizo.
Serikali ifungue milango tuwe na makampuni binafsi ya kuzalisha,kusafirisha na kuuza umeme.
 
Serikali ifungue milango tuwe na makampuni binafsi ya kuzalisha,kusafirisha na kuuza umeme.
Umeme ni huduma muhimu sana kwa uchumi na uhai wa taifa lolote katika dunia hii ya sasa. Hivyo mbali na kupata huduma hii, lazima pia tuzingatie gharama nafuu kwa wananchi. Unadhani tukiruhusu makampuni binafsi kuzalisha, kusafirisha na kuuza umeme tunaweza kupata umeme wa gharama nafuu ??? (Kama ndiyo, naomba utusaidie kutuonesha ni kipivi itakuwa hivyo)

Nchini Marekani umeme wa Tennessee Valley Authority (TVA) ambalo ni shirika la kiserikali una gharama nafuu zaidi kuliko ule kutoka kwenye mashirika binafsi. Unadhani hili linawezekana kufanyika nchini Tanzania ???
 
Ninawasi wasi sana na huu mradi kuwa na tija hapo baadae maana watanzania hatuna historia ya kuendesha miradi mikubwa ,Mwl nyerere aliacha mashirika makubwa sana yakiwa na hari nzuri lakini mengi yamekufa kama si kubinafsishwa kwa hasara,moja ya kosa la serikari ni mkandarqsi alipewa kujenga mradi Mwarabu muda mwingi yeye ni kunywa kahawa na kupiga fitna mchina ambae ni sub anawakimbiza kwa kufanya kazi kwa wakati ukumbuke kila unavyoongeza muda katika miradi garama zinazidi na mbatika katika lengo,swari je serikari na tanesco wamejiandaa kikamilifu hapo baadae kuendesha mradi?je tabia ya watanzania katika usimamizi wa mali za umma umebadilika?sina hakika kama tutamudu kuendesha huu mradi na kurejesha garama hapo baadae nionavyo tutarudi kwenye kuubinafsisha tu muda ni mwalimu mzuri sana hivyo tusubili
Sio kweli kwamba Nyerere aliacha Mashirika ya Serikali katika hali nzuri
 
Studies zinaonyesha kuwa Mkoloni Mwingereza ndiyo waliobuni mradi wa umeme wa Stiglers Gorge mwaka 1936 na Mwl JKNyerere through taasisi ya RUBADA mwaka 1980 akafanya upembuzi yakinifu. Kwa sababu mbali mbali mradi hauku take off wakati ule umekuja kulazimishwa mwaka 2016 na Magufuli.

Hakuna upembuzi yakinifu mwingine uliofanyika zaidi ya copy and paste ili kumridhisha Jiwe ambaye akiamua la kwake ameamua. By rule of thumb inawezekana 36% ya maji yamepungua kati ya mwaka 1978 na 2016 kutokana na sababu zifuatazo;

1. Utekelezaji wa Mtera Dam pale kati ya Dodoma na Iringa

2. Utekelezaji wa Kihansi Electricity Project pale Kilombero

3. Shughuli za binadamu kwenye bonde la Usangu na bonde la Kilombero

4. Mabadiliko ya tabia nchi kusababisha mvua kupungua

5. Mito yetu kujaa matope sana

Hata ukirudi nyuma tuliaminishwa wakati Mtera inajengwa mwaka 1981 na Kihansi mwaka 1993 kuwa yalikuwa ni masuluhisho ya matatizo ya umeme Tanzania. Lakini shida ziliendelea mpaka leo.

Kama Jiwe angekuwa rational angekubali tu tuendelee na umeme wa gesi ya Mtwara. Ila akitaka ku mprove JK kuwa alikuwa wrong yeye ndiyo ana upeo. Kitu ambacho si kweli

Suala ta utunzaji wa mazingira litakuwa ni changamoto sana katika uzalishaji wa umeme. Mfano ukiangalia uzalishaji wa umeme kwa kutuma vyanzo vya maji vya miradi ya Kidatu, Mtera na Kihansi ulipungu sana ndiyo maana uzalishaji umeme kwa kutumia makapuni ya nje ambayo yakitugharimu mabilion ya fedha yakawepo.

Kutokana na sababu hizo tukaanzisha uzalishaji wa umeme wa gesi kinyerezi.
Tumefanya nini katika uzalishaji wa umeme katika bwana la Nyerere;

1. Uhamasishaji wa kutunzwa kwa vyanzo yote vinavyotirisha maji katika mto husika na kuanisha vipaumbele kwa ngazi ya kitaifa kwa kutumia mawaziri na Makatibu Wakuu Sijui kama kuna utekelezaji endelevu wenye bajeti na uratibu wenye mikakati ya utekelezaji.

2. Tutakuwa na uhakika gani kupata maji katika vyanzo hivyo vinavyotiririsha maji katika mto huo. Kwa kuhakisha vyanzo vyote vinatunzwa nabufutiliaji wa vyanzo vyote wawepo wawajibika wa maeneo kwa kufuata ukanda, tarafa, wilaya hadi mkoa.

3. Tukifanya hivyo kuanzia sasa tunweza kupata bwawa tarajiwa lenye tija na uhakika wa kina cha kutosha kuzalisha umeme wa kutosha, hivyo kupunguza bei ya umeme.
 
Umeme ni huduma muhimu sana kwa uchumi na uhai wa taifa lolote katika dunia hii ya sasa. Hivyo mbali na kupata huduma hii, lazima pia tuzingatie gharama nafuu kwa wananchi. Unadhani tukiruhusu makampuni binafsi kuzalisha, kusafirisha na kuuza umeme tunaweza kupata umeme wa gharama nafuu ??? (Kama ndiyo, naomba utusaidie kutuonesha ni kipivi itakuwa hivyo)

Nchini Marekani umeme wa Tennessee Valley Authority (TVA) ambalo ni shirika la kiserikali una gharama nafuu zaidi kuliko ule kutoka kwenye mashirika binafsi. Unadhani hili linawezekana kufanyika nchini Tanzania ???
Ni kweli umeme ni huduma muhimu hasa kwa Uchumi wa Nchi,kama ilivyo kwenye mawasiliano ya simu na intranet ambapo tumepata mafanikio katika sekta hiyo (Mawasiliano).Kwahiyo tunaweza kuanza,gharama zitaenda zinashuka,Serikali inaweza kuendelea kuweka ruzuku kwa muda.Tukiruhusu Makampuni binafsi angalau tutakuwa na uhakika na Umeme wa kutosha na wa uhakika.
 
Makamba ajawahi kuwa seriously kwenye jambo lolote
 
Ni kweli umeme ni huduma muhimu hasa kwa Uchumi wa Nchi,kama ilivyo kwenye mawasiliano ya simu na intranet ambapo tumepata mafanikio katika sekta hiyo (Mawasiliano).Kwahiyo tunaweza kuanza,gharama zitaenda zinashuka,Serikali inaweza kuendelea kuweka ruzuku kwa muda.Tukiruhusu Makampuni binafsi angalau tutakuwa na uhakika na Umeme wa kutosha na wa uhakika.
Nakuelewa vizuri, lakini swali langu bado liko kwenye huduma nafuu ya umeme kwa mtanzania wa kawaida. Je, hili litawezekana endapo tutaruhusu mashirika binafsi kufua na kuuza umeme ??
 
Nakuelewa vizuri, lakini swali langu bado liko kwenye huduma nafuu ya umeme kwa mtanzania wa kawaida. Je, hili litawezekana endapo tutaruhusu mashirika binafsi kufua na kuuza umeme ??
Bei nafuu ni Tsh ngapi?.Umeme kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya Production.Production ikiongezeka uchumi utakuwa na hivyo basi kipato cha Mwananchi kitaongezeka kuweza kumudu kulipia umeme.
 
Umeandika mengi lakini umejichanganya sana.
Tafuta wataalamu wa haya masuala wakusaidie.
Kuna factors (moderating and mediating factors) nyingi umeziweka constant.
Umeme wa maji ni mzuri lakini si rafiki wa mazingira!
Kama umeme wa maji si rafiki kwa mazingira ni upi ulio rafiki?
 
Bei nafuu ni Tsh ngapi?.Umeme kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya Production.Production ikiongezeka uchumi utakuwa na hivyo basi kipato cha Mwananchi kitaongezeka kuweza kumudu kulipia umeme.
Umeenda mbali sana na umeangalia hili suala kwa upande moja peke yake. Karne ya 21 nishati ya umeme haitumiki kwenye uzalishaji wa kiviwanda peke yake (Industrial Production), bali hata kutoa huduma (Service Market) na Usafirishaji (Transportation). Watanzania wengi hutumia huduma ya umeme katika utoaji huduma, hivyo huwezi kutegemea uzalishaji peke yake bila kuangalia soko la huduma ambalo wananchi wengi tunajihusisha.

Sasa tuje kwenye gharama: Unafuu wa gharama za umeme hutegemea sababu nyingi sana, kama upatikanaji wa rasilimali muhimu ambazo hutumika kuzalisha umeme, Aina gani ya umeme mnazalisha, Hali ya hewa, Idadi ya watu katika eneo na n.k Hivyo gharama za umeme huweza kutofautiana eneo na eneo katika nchi zilizoendelea. Mfano mwingine, huwezi kusema umeme wa nyuklia unaozalishwa kwa nyuklia unaweza kuwa gharama sawa na umeme wa gesi, makaa, maji au upepo.
 
Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
Acha matusi yako yatokanayo na uvivu wa kusoma. Hii kitu aliyoandika inasomeka kwa dka 15 hadi 20 tuu. Wapi shida? na hulazimishwi kusoma pia, ila kabla hujasoma na kuelewa mada usiweke mchango dhaifu hapa tafadhali.
 
Umeenda mbali sana na umeangalia hili suala kwa upande moja peke yake. Karne ya 21 nishati ya umeme haitumiki kwenye uzalishaji wa kiviwanda peke yake (Industrial Production), bali hata kutoa huduma (Service Market) na Usafirishaji (Transportation). Watanzania wengi hutumia huduma ya umeme katika utoaji huduma, hivyo huwezi kutegemea uzalishaji peke yake bila kuangalia soko la huduma ambalo wananchi wengi tunajihusisha.

Sasa tuje kwenye gharama: Unafuu wa gharama za umeme hutegemea sababu nyingi sana, kama upatikanaji wa rasilimali muhimu ambazo hutumika kuzalisha umeme, Aina gani ya umeme mnazalisha, Hali ya hewa, Idadi ya watu katika eneo na n.k Hivyo gharama za umeme huweza kutofautiana eneo na eneo katika nchi zilizoendelea. Mfano mwingine, huwezi kusema umeme wa nyuklia unaozalishwa kwa nyuklia unaweza kuwa gharama sawa na umeme wa gesi, makaa, maji au upepo.
Mkuu mimi ninafikiri tunaongea lugha moja,uzalishaji ni uzalishaji uwe wa bidhaa au huduma.
Labda tusaidiane,mbona kwenye sekta ya Mawasiliano tumeweza?
 
Back
Top Bottom