Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Unaweza kutuwekea mchanganuo hapa ni kwa vipi kila mradi ungepanuliwa kuongeza megawats ngapi?Miradi kama Nyumba ya Mungu, Kidatu, Mtera, Kihansi ilikua ipanuliwe kuogeza megawatts
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaweza kutuwekea mchanganuo hapa ni kwa vipi kila mradi ungepanuliwa kuongeza megawats ngapi?Miradi kama Nyumba ya Mungu, Kidatu, Mtera, Kihansi ilikua ipanuliwe kuogeza megawatts
Sababu zimetolewa nyingi sana na Waziri Makamba, lakini ipi ni ya kweli na ipi haina ukweli ???Mkuu hakuna cha winch wala winji ni porojo tu zile nipo eneo la mradi katika nafasi ya mfanyakazi wa JV hamna kitu &January angekuwa na akili na yule mwingine alieugua corona wangewauliza watanzania jamani eeeee ni nini kinaendelea hapa?wangewasikiliza nazani wasimamizi wa mradi wangefukuzwa kazi hapo hapo kuna madudu ya hovyo sana huku
Mkuu, ili kupata taswira ya inakokwenda ni lazima tufahamu tulikotoka ili makosa yasijirudie.
Mimi nimekuuliza maswali machache kuhusu Power-Master-Plan 2025 ili niweze kufahamu ni lini ilitengenezwa, kwa kiwango gani ilitekelezwa kabla ya 2015, fungu lake ni kiasi gani na kufahamu ni kiasi gani cha umeme kingeweza kuzalishwa mpaka 2050.
Lilikuwa ni suala dogo tu, kunipa hata chanzo ili nitakafute mwenyewe. Ntashukuru ukinasaidia kupata vyanzo ili nijifunze zaidi.....
Kumbe iliishia kwenye ngazi ya chama tu, na haikufika kwenye Interminsterial Technical Committee ???Mkuu kwa sasa imeeditiwa, wakati tunapiga kelele watu waligeuza gia angani wakaiedit..
Mimi niliiongelea kwenye makala moja ila kama siku mbili mbele nilivyoingia PDF nikakuta kitu kingine. Ila ilielekeza kuboresha miradi kama Bwawa la nyumba ya Mungu, Kidatu, Mtera e.t.c na kulikuwa na specific amounts za investment na megawatts to be expected..
Ila kwenye ilani ya CCM 2015 -2020 imeongelewa
Mkuu nakusoma vizuri kabisa, hili la kuangalia Financial Viability nimelizungumzia kule juu kwenye mradi wa Tennessee Valley Authority (TVA). Mahakama ya Juu ya Marekani (The US Supreme Court) ilizungumza kama ulivyoweka bayana hapa. Nikushukuru sana ndugu yangu kwa mchango wako mzuri ?Miradi kama hii haipimwi kwa financial viability. Kuna vigezo zaidi ya hivyo. Angalia kwenye nyanja za kiuchumi na kijamii. Kuna internal rate of return kubwa sana for time infinity.
CC: MALCOM LUMUMBA
Serikali ifungue milango tuwe na makampuni binafsi ya kuzalisha,kusafirisha na kuuza umeme.Kwenye aya za mwanzo kabisa za uzi wangu nimezungumzia GOVERNMENT MONOPOLY. Hebu naomba utueleweshe TANESCO's MONOPOLY inasababishaje tatizo la uhaba wa nishati ya umeme nchini na tutumiea mbinu ipi kulitatua tatizo.
Umeme ni huduma muhimu sana kwa uchumi na uhai wa taifa lolote katika dunia hii ya sasa. Hivyo mbali na kupata huduma hii, lazima pia tuzingatie gharama nafuu kwa wananchi. Unadhani tukiruhusu makampuni binafsi kuzalisha, kusafirisha na kuuza umeme tunaweza kupata umeme wa gharama nafuu ??? (Kama ndiyo, naomba utusaidie kutuonesha ni kipivi itakuwa hivyo)Serikali ifungue milango tuwe na makampuni binafsi ya kuzalisha,kusafirisha na kuuza umeme.
Mkuu kama hutajali hebu tuwekee hiyo yenye sura mpya.Hiyo masterplan ilieditwa na Jiwe..
Na mimi sikusave ile ya mwanzo..kwa sasa ina sura mpya
Sio kweli kwamba Nyerere aliacha Mashirika ya Serikali katika hali nzuriNinawasi wasi sana na huu mradi kuwa na tija hapo baadae maana watanzania hatuna historia ya kuendesha miradi mikubwa ,Mwl nyerere aliacha mashirika makubwa sana yakiwa na hari nzuri lakini mengi yamekufa kama si kubinafsishwa kwa hasara,moja ya kosa la serikari ni mkandarqsi alipewa kujenga mradi Mwarabu muda mwingi yeye ni kunywa kahawa na kupiga fitna mchina ambae ni sub anawakimbiza kwa kufanya kazi kwa wakati ukumbuke kila unavyoongeza muda katika miradi garama zinazidi na mbatika katika lengo,swari je serikari na tanesco wamejiandaa kikamilifu hapo baadae kuendesha mradi?je tabia ya watanzania katika usimamizi wa mali za umma umebadilika?sina hakika kama tutamudu kuendesha huu mradi na kurejesha garama hapo baadae nionavyo tutarudi kwenye kuubinafsisha tu muda ni mwalimu mzuri sana hivyo tusubili
Google tu..andika; Tanzania power system masterplan..download hizo za PDFMkuu kama hutajali hebu tuwekee hiyo yenye sura mpya.
Ni kweli umeme ni huduma muhimu hasa kwa Uchumi wa Nchi,kama ilivyo kwenye mawasiliano ya simu na intranet ambapo tumepata mafanikio katika sekta hiyo (Mawasiliano).Kwahiyo tunaweza kuanza,gharama zitaenda zinashuka,Serikali inaweza kuendelea kuweka ruzuku kwa muda.Tukiruhusu Makampuni binafsi angalau tutakuwa na uhakika na Umeme wa kutosha na wa uhakika.Umeme ni huduma muhimu sana kwa uchumi na uhai wa taifa lolote katika dunia hii ya sasa. Hivyo mbali na kupata huduma hii, lazima pia tuzingatie gharama nafuu kwa wananchi. Unadhani tukiruhusu makampuni binafsi kuzalisha, kusafirisha na kuuza umeme tunaweza kupata umeme wa gharama nafuu ??? (Kama ndiyo, naomba utusaidie kutuonesha ni kipivi itakuwa hivyo)
Nchini Marekani umeme wa Tennessee Valley Authority (TVA) ambalo ni shirika la kiserikali una gharama nafuu zaidi kuliko ule kutoka kwenye mashirika binafsi. Unadhani hili linawezekana kufanyika nchini Tanzania ???
Nakuelewa vizuri, lakini swali langu bado liko kwenye huduma nafuu ya umeme kwa mtanzania wa kawaida. Je, hili litawezekana endapo tutaruhusu mashirika binafsi kufua na kuuza umeme ??Ni kweli umeme ni huduma muhimu hasa kwa Uchumi wa Nchi,kama ilivyo kwenye mawasiliano ya simu na intranet ambapo tumepata mafanikio katika sekta hiyo (Mawasiliano).Kwahiyo tunaweza kuanza,gharama zitaenda zinashuka,Serikali inaweza kuendelea kuweka ruzuku kwa muda.Tukiruhusu Makampuni binafsi angalau tutakuwa na uhakika na Umeme wa kutosha na wa uhakika.
Bei nafuu ni Tsh ngapi?.Umeme kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya Production.Production ikiongezeka uchumi utakuwa na hivyo basi kipato cha Mwananchi kitaongezeka kuweza kumudu kulipia umeme.Nakuelewa vizuri, lakini swali langu bado liko kwenye huduma nafuu ya umeme kwa mtanzania wa kawaida. Je, hili litawezekana endapo tutaruhusu mashirika binafsi kufua na kuuza umeme ??
Kama umeme wa maji si rafiki kwa mazingira ni upi ulio rafiki?Umeandika mengi lakini umejichanganya sana.
Tafuta wataalamu wa haya masuala wakusaidie.
Kuna factors (moderating and mediating factors) nyingi umeziweka constant.
Umeme wa maji ni mzuri lakini si rafiki wa mazingira!
Umeenda mbali sana na umeangalia hili suala kwa upande moja peke yake. Karne ya 21 nishati ya umeme haitumiki kwenye uzalishaji wa kiviwanda peke yake (Industrial Production), bali hata kutoa huduma (Service Market) na Usafirishaji (Transportation). Watanzania wengi hutumia huduma ya umeme katika utoaji huduma, hivyo huwezi kutegemea uzalishaji peke yake bila kuangalia soko la huduma ambalo wananchi wengi tunajihusisha.Bei nafuu ni Tsh ngapi?.Umeme kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya Production.Production ikiongezeka uchumi utakuwa na hivyo basi kipato cha Mwananchi kitaongezeka kuweza kumudu kulipia umeme.
Acha matusi yako yatokanayo na uvivu wa kusoma. Hii kitu aliyoandika inasomeka kwa dka 15 hadi 20 tuu. Wapi shida? na hulazimishwi kusoma pia, ila kabla hujasoma na kuelewa mada usiweke mchango dhaifu hapa tafadhali.Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
Mkuu mimi ninafikiri tunaongea lugha moja,uzalishaji ni uzalishaji uwe wa bidhaa au huduma.Umeenda mbali sana na umeangalia hili suala kwa upande moja peke yake. Karne ya 21 nishati ya umeme haitumiki kwenye uzalishaji wa kiviwanda peke yake (Industrial Production), bali hata kutoa huduma (Service Market) na Usafirishaji (Transportation). Watanzania wengi hutumia huduma ya umeme katika utoaji huduma, hivyo huwezi kutegemea uzalishaji peke yake bila kuangalia soko la huduma ambalo wananchi wengi tunajihusisha.
Sasa tuje kwenye gharama: Unafuu wa gharama za umeme hutegemea sababu nyingi sana, kama upatikanaji wa rasilimali muhimu ambazo hutumika kuzalisha umeme, Aina gani ya umeme mnazalisha, Hali ya hewa, Idadi ya watu katika eneo na n.k Hivyo gharama za umeme huweza kutofautiana eneo na eneo katika nchi zilizoendelea. Mfano mwingine, huwezi kusema umeme wa nyuklia unaozalishwa kwa nyuklia unaweza kuwa gharama sawa na umeme wa gesi, makaa, maji au upepo.