Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Kumbuka kuweka pipes infrastructure ni costly, ingawa Russia ina upper hand on that front sababu pipe tayari ipo..., kwahio the next big thing ni liquefied Natural Gas (kwahio who is one of the largest player in that sector) ?

Kwa hali ilivyo Marekani na Ulaya ni kuwa kwa njia yeyote ile lazima waachane na Urusi ili Urusi aache kibuli.

Na njia pekee ya kuachana na Urusi na kumuua Urusi ni kuacha kutegemea gesi yake. Kama wataacha kutegemea Gesi ya Urusi ni lazima sehemu wanayoweza kupata Gesi wahakikishe Gesi iyo inafika Ulaya. Na nakuhakikishia wataifikisha ulaya hata kwa kupunguza shipping cost kutoka Tanzania
 
Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.
Mumesahau kuwa Jpm alidai gesi iliuzwa kwa Mabeberu. Sasa kuhusu nani na serikali ya utawala upi iliuza hakusema. Hvyo akaki.bilia miradi inayotumia ngv nyingi na rasilimali nyingi. Akaacha gesi iliyo ardhini ambayo side effects zake ni chache. Hii africa wanasiasa ni watu wa hovyohvyo tu.
 
Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa Mkuu mbona Nchi zenye gas ni nyingi Sana hapa Duniani yaani Tanzania ni kiduchu Sana,sioni hiyo advantage.
 
Weka ushahidi kuwa sio ya Tanzania. Au upon chato huko umeshalishwa matango pori unakuja kuropoka humu
Ww ndio mlopokaji na unajipendekaza kwa watawala HAKUNA GESI YA TAIFA mikataba mibovu ambayo inalinyima taifa mapato ya gesi .hatuna uwezo wa kuiuza gesi mpaka mwekezaji abembelezwe ...usiwadanganye wananchi ww
 
Mkuu mbona Nchi zenye gas ni nyingi Sana hapa Duniani yaani Tanzania ni kiduchu Sana,sioni hiyo advantage.
Biashara duniani ni namna unavyotumia fursa inayopatikana kwako. Kuwa na Gesi ni jambo moja a kuitumia fursa ya kuwa na Gesi kufaidika kiuchumi ni jambo lingine.

Hata Marekani ana hifadhi kubwa sana ya .
mafuta na Gesi ila nchi zinazofaidika zaidi katika Biashara ya mafuta na Gesi duniani ni Qatar, Saudi Arabia na UAE.
 
Ww ndio mlopokaji na unajipendekaza kwa watawala HAKUNA GESI YA TAIFA mikataba mibovu ambayo inalinyima taifa mapato ya gesi .hatuna uwezo wa kuiuza gesi mpaka mwekezaji abembelezwe ...usiwadanganye wananchi ww
Usiongee maneno mengi sana nipe ushahidi tu kuwa Gesi sio ya Tanzania
 
Mumesahau kuwa Jpm alidai gesi iliuzwa kwa Mabeberu. Sasa kuhusu nani na serikali ya utawala upi iliuza hakusema. Hvyo akaki.bilia miradi inayotumia ngv nyingi na rasilimali nyingi. Akaacha gesi iliyo ardhini ambayo side effects zake ni chache. Hii africa wanasiasa ni watu wa hovyohvyo tu.
Jpm ndo nani hadi aaminike? Alikupa huo ushahidi kuwa Gesi imeuzwa kwa mabeberu?
 
Upo sahihi kabisa...

Mwaka 2018 niliwahi kuandika haya...

mkuuwakaya,

Nitajitahidi kueleza kwa uchache sana manake kwenye issue ya gas kuna mengi sana ya kueleza!!

Mosi; FAILURE kubwa ya JPM katika issue ya kutozingaatia vipaumbele basi ni suala la gas!

Kama kweli JPM ana lengo la kuwaondolea Watanzania umaskini basi TOP PRIORITY yake ingekuwa kwenye gas na wala sio ndege na wala sio viwanda!

Angeweka priority kwenye gas... akazuia ufisadi kwenye gas; na akajenga uchumi mzuri wa gas; hayo ya ndege na viwanda yangekuja automatically tena at advanced level!

Wakati tunaenda mwaka wa 3 sasa na bado ndo kwanza kafanikiwa kupata vindege 3 kiasi cha kutokuwa threat hata kwa FastJet; endapo angejenga na uchumi wa gas angeweza kununua hata Airbus 100 kwa mpigo na kuyatisha hata mashirika makubwa kama Ethiopia Airline!

Gas ni uchumi

Gas ni viwanda

Gas ni fimbo ya diplomasia

Gas ni fimbo ya siasa za kimataifa

Kufafanunua yote hayo kunahitaji muda!

Lakini kwa ufupi tu ni kwamba; leo ukizalisha gas na kusambaza throughout East Africa... hizo nchi zote zitakuheshimu!

Zitakuheshimu kwa sababu zitafahamu uchumi wao unategemea gas ya Tanzania!!

Yule Kagame aliyekuwa anamkejeli JK ingekuwa ukimpigia kufuli koki inayopeleka gas Rwanda; siku ya pili angepanda ndege kuja Dar kusawazisha hali!

Hiyo ndiyo gas!

Hata byproducts zinazotokana na natural gas processing ni malighafi tosha ya viwanda!

I hate to say this but to be honest hata kwenye madini alikowekeza nguvu nako ni wastage of time!

Sisemi apuuze kwenye madini bali ile nguvu aliyowekeza kwenye madini ndo angewekeza kwenye gas basi impact yake ingekuwa kubwa zaidi ya mara 10!

Ngoja nikuulize swali moja:

Hivi wazungu wakigoma kununua ile Tanzanite na Gold; alternatively tutaifanyia nini?!

Swali lingine dogo: Unaweza kunitajia nchi 3 tu duniani zinazokula bata kwa kutegemea uchumi wa madini?!

Jiulize maswali sawa na hayo upande wa gas!

Panapo majaliwa; ningependa tujadili kwa mapana na marefu; with statistics and figures na subject iwe: "A Comparative Analysis of the Gas and Mining Economy"

To sum up... JPM bado hajaiangalia gas kwa jicho pana kiasi hicho! Pamoja na madhaifu yote ya JK lakini inaelekea yeye aliiangalia gas kwa jicho pana na ndio maana ilikuwa ndiyo priority yake!

Na ngoja nikutoe shaka!

Gas tunayoizungumza hapa na aliyokuwa anaisema JK na Muhongo wake sio hii iliyoanza kupita kwenye Bomba la Gas la Mtwara!

Gas yenyewe haijachimbwa bado! Ile ya kwenye bomba is just a fraction of 57 trillion cubic feet of discovered gas reserve!!

Gas yenyewe ni ile ambayo kiwanda cha kuichakata ndo kile kilitarajiwa kujengwa pale Lindi!

Mradi wa kile kiwanda peke yake ni zaidi ya Shilling Trilioni 65... narudia; sio Bilioni 65 bali TRILIONI 65... Bajeti yetu miaka 2 na chenji inabaki!

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, kiwango hicho ni takribani mara 2 ya Market Cap ya Barrick Gold!

Barrick Gold ndio kampuni kubwa kuliko zote za uchimbaji dhahabu duniani!

Cortez na Goldstrikes ni among top 10 mines duniani na yote hiyo ipo USA na inamilikiwa na Barrick Gold Mines!

Chukua mapato yote (not faida) ya mgodi wa Cortez na Goldstrikes kwa miaka 10 ndipo labda unaweza kufikia hiyo Trilioni 65.

Hiyo ndiyo gas tunayoisema! Investment ya kiwanda cha kuichakata tu ni Bajeti yetu ya miaka 2!!

JPM bado hajaona ikiwa mradi kama huo unahitaji priority!

Aidha nikujuze lingine! Achana na simulizi za kwamba gas yote imechukuliwa na Wachina!

Makampuni yaliyofanya exploration ni ya Ulaya na America! They invested billions of T Shilling kufanya exploration! Aidha zote hizo ni gas and oil companies!

That said; there's no way pamoja na energy yote waliyotumia halafu gas yote wamwachie Mchina wakati wao hiyo ndiyo biashara yao ambayo wapo tayari hata ku-initiate War for the sake of their business... gas and oil business!!

Gas and oil business iliyozalisha:
Etihad Airways
Emirates
Qatar Airways

Hivi umeshawahi fika Qatar ukaona wa-Qatar wanavyoishi kama Wafalme?!

Ni nchi pekee duniani ambayo zaidi ya 80% ya population yake ni wageni! Ni wageni walioenda kutafuta na kufanya kazi huku wenyewe wakifanya kazi kifalme! All that is because of the fvcking gas and oil business ambayo JPM ni kama bado sio priority kwake!

Tungechimba ile gas wala tusingehitaji tena Stigler's Gorge!

Stigler's tungeiacha iendelee kuhifadhi uoto wetu!!

What about Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015 pamoja na ile ya Sheria ya Matumizi ya Mapato ya Mafuta na Gesi?!

Na kuna siku niliwahi kusema hapa kwamba, position ya Tanzania relative to Europe ni fursa kubwa sana kwa sababu Putin amekuwa akitumia sana fimbo ya gesi, na kwahiyo lau kama tungekuwa tumechangamka, basi ukanda huu wa Africa... yaani Tanzania and Mozambique ingekuwa ndo kimbilio la Europe ukiacha Middle East.
Total ametangaza ana resume uzalishaji Mozambique, Shell na Equinor wao wanachangamkia Tanzania.

Serikali wameliona hili tuwaombee likamilike na kuenda vizuri
 
Jpm ndo nani hadi aaminike? Alikupa huo ushahidi kuwa Gesi imeuzwa kwa mabeberu?
Kama haijauzwa..munakkmbilia kutumia maji ya nini Wakati wa serkalini ya Jk bungeni mlisema gesi ndy itashusha bei ya umeme mpaka viwanda vitajengwa vijijini. Watu walewale mkaja sema tena Gesi imeuzwa kwa mabeberu Mara Paa Umeme wa Hp..Rufiji....gesi kama ipo maji kwanini muyasumbue?
 
Nimekusoma ulichoandika mpaka pale uliposema nchi yetu ina siasa nzuri, huu upofu wa makusudi unaojitia unajidanganya mwenyewe, ni kama unajitekenya na kucheka peke yako.

Kuhusu hiyo LNG mtazipata wapi $30mil zinazohitajika kwenye huo mradi?

Kwa utoto ulioandika hapa, vipi kuhusu Nyerere Dam ndio pesa imeshachezewa pale kwa hiyo iachwe ipotee?

Kama hiyo ndio akili yenu, kwanini nisiamini mnataka kuanzisha mradi mpya wa LNG ili nanyi mpate nafasi ya upigaji ili kama ikitokea msipoukamilisha kama wa Nyerere Dam muwe mmeshaiba mnachotaka?

Naona umejaza uzi wako na yanayotokea ulaya kama vile hao wazungu wanatupenda sana sisi, unajidanganya tu, kwenye maslahi hakuna taifa litakalokubali kuwa nyuma ya lingine hata kama kila siku mtaenda kwao miaka kumi mfululizo.

Tusidanganyane, sharti mradi wa Nyerere Dam ukamilike kwanza kama kweli mnataka kuokoa pesa za walipakodi masikini wa Tanzania, badala ya kujitutumua na miradi mipya ya bei ghali ambayo hamuwezi kuikamilisha wenyewe, huu ujinga wa kujiona wajanja kwasababu mnakopesheka utaangamiza vizazi vya hili taifa.
Mwenzako anaongea juu ya opportunity ya Tanzania kutokana na mahusiano ya Urusi na Ulaya. Mimi namuunga mkono. Hiyo ni biashara. Zaidi nataka nijue usafirishaji wa gesi yetu kwenda Ulaya utakuaje.
 
Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.
Sahau Hilo swala kabisaa

Maana usitegemee mnyonge kunufaika hapo

Wajanja watakula na niwale tu amba wapo upande wa wenye nguvu
 
Kwa hali ilivyo Marekani na Ulaya ni kuwa kwa njia yeyote ile lazima waachane na Urusi ili Urusi aache kibuli.

Na njia pekee ya kuachana na Urusi na kumuua Urusi ni kuacha kutegemea gesi yake. Kama wataacha kutegemea Gesi ya Urusi ni lazima sehemu wanayoweza kupata Gesi wahakikishe Gesi iyo inafika Ulaya. Na nakuhakikishia wataifikisha ulaya hata kwa kupunguza shipping cost kutoka Tanzania
Sasa tumehama kwenye Point yangu ya Mwanzo..., Is it Diplomatically Correct kwa Tanzania kusema (kusema sio kuwaza) kwamba huu mgogoro ni fursa kwetu?
 
LNG si ni mradi wa kuiprocess gas’s kupata products mbali mbali zaidi zaidi ni kuisafisha na kuondoa takataka na kuivadilisja form kuwa liquid ili iweze kuwa stored kwenye mitungi kama LPG does LNG and LPG rings a bell in your head? LNG has nothing to do with uzalishaji wa umeme Tafiti kwanza kabla haujakosoa, leo hii gas ya kupikia tunaagiza nje na inakuja kwa Meli ila kwa mradi wa LNG gas itakuwa inatoka lindi kuja nyumbani kwako ikiwa kwenye mtungi
Are you sure about this? ile Gas tuliyoambiwa wakati wa Kikwete unakumbuka ilipoishia?
 
Are you sure about this? ile Gas tuliyoambiwa wakati wa Kikwete unakumbuka ilipoishia?
Uzi umejaa watu wa yule jamaa, ukweli ni kuwa gesi yote iliuzwa hatuna gesi. Hata hii ya umeme tunanunua
 
Mwenzako anaongea juu ya opportunity ya Tanzania kutokana na mahusiano ya Urusi na Ulaya. Mimi namuunga mkono. Hiyo ni biashara. Zaidi nataka nijue usafirishaji wa gesi yetu kwenda Ulaya utakuaje.
Hiyo mikataba utaionea wapi?
 
Are you sure about this? ile Gas tuliyoambiwa wakati wa Kikwete unakumbuka ilipoishia?
Kwani Gesi ya kipindi cha JK ndo LNG? Ndugu ni vizuri kuomba ueleweshwe maana unaonekana elimu yako ni ya hapa na pale
 
Back
Top Bottom