Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.

Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi

Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi

Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.

Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.

Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi

Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana

Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.

Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?

Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
View attachment 2128208
hebu nikuulize mleta mada, huu mradi (ikiwa utakubalika kufanyika) utachukuwa muda gani kukamilika? Na nimeshindwa kusoma popte katika nakala yako panaposema mradi mzima unatagharimu kiasi gani! Na kwa muda wote huu wakati europe wanasubiri ukamilishaji wa mradi huu ni nani atakuwa suplier mkuu wa gas kwa nch hizo ulizozitaja?
 
Ulaya kuachana na Urusi ni long term plan! Kama ilivyokuwa Cold War.

Hata ukichukua miaka 5, Suala litakuwa Ulaya hawahitaji tena Gesi ya Urusi na wananunua Gesi sehemu nyingine ikiwemo Tanzania
 
Mkuu mm nimeshangaa tu kuwa jamaa anasema 30Mus$ ni hela ndefu...ila baada ya kusoma comments zako ndo nikaona umemkosoa na kusema 30billion$us...Haya Mambo sio mgeni sa a ingawa sio mfuatiliaji Sana..ila migodi ya dhahabu inagharimu zaidi ya 300mus$ kuanzishwa na watu wanaweka mpunga...ndo maana nikasema kama ni only 30m$ Wala hatuna haja ya muwekezaji. Shida ya hii nchi siasa nyingi Sana. Mm naamini wizara ya nishati na madini wakati ule wangemwacha Muhongo na wakaacha kumuingilia Leo hii tungekuwa tunaongea mengine kabisa kwenye gesi...sema nn mkuu ndo maana watu wengi wmefika sehemu wanasema acha nitafute ugali wa watoto wangu tu.
Bado hadi kesho namlilia Muhongo...

Muhongo ndie alikuwa anaifahamu hii sekta hii vizuri...
 
Uzi umejaa watu wa yule jamaa, ukweli ni kuwa gesi yote iliuzwa hatuna gesi. Hata hii ya umeme tunanunua
Walinzi wa Legacy mna matatizo sio kidogo...

Eti gesi iliuzwa... ni nani aliuziwa?!
 
Bado hadi kesho namlilia Muhongo...

Muhongo ndie alikuwa anaifahamu hii sekta hii vizuri...
Yaani acha kabisa mkuu...siku kamati ya makinikia wanasoma report yao nil
itamani niingie chini ya meza maana kilichofanyika pale ni uzandiki wa Hali ya juu Sana...niliwashangaa Sana akina Mruma na Ikingura kuja na report ya namna Ile...inakuweje watu na uelewa wao wana-quantifu gangue minerals...nilishangaa Sana...sijui Mruma alikuwa anataka uwaziri hata sijui..
 
Wosomi wetu wapo kulinda matumbo yao na sio kulinda proffessional zao kwa maana ya kulisaidia taifa. Kwa kipindi kile ilikuwa na ngumu labda kwa mwenye strong balls kama lisu kusimamia ukweli mbele ya mzalendo wa chato.
 
Magufuli aliharibu sana kwenye suala la gas.

Baada ya kugundua kuwa ameharinu, akaanza kuhangaika kutaka kuurudisha huo mradi, akagonga mwamba. Mwaka 2020, wawekezaji wakaahidi kuwa wanaweza kurudi tena Tanzania, lakini haitakuwa kabla ya miaka mitano. Lakini kimsingi ni kwamba waliona dhahiri kuwa utawala wa Magufuli siyo wa kuaminika.
Sio tuu gas ,aliharibu Bagamoyo port na uchumi in general,angekuwa hai saizi tungekuwa shimoni.
 
Bado hadi kesho namlilia Muhongo...

Muhongo ndie alikuwa anaifahamu hii sekta hii vizuri...
Yani Watanzania milioni 60 katika miaka 60 ya uhuru Muhongo peke yake ndiye tegemeo!
 
Yani Watanzania milioni 60 katika miaka 60 ya uhuru Muhongo peke yake ndiye tegemeo!
Wapo wengi ila huwezi mlinganisha Muhongo na Kalemani au Makamba...hata ukiwachanganya pamojahawafiki hata heluthi ya uelewa wa Muhongo kwenye ishu za madini na nishati mkuu...Muhongo ni level nyingine boss.
 
Angola, Equatorial Guinea, Gabon, Sudan na Nigeria wote ni wazalishaji wakubwa wa mafuta dunia ila umaskini uliokithiri kwa watu wengi haujaondoka. Sisi ni tofauti sana na Waafrika wengine?

Pia utajiri wa nchi huamiliwa zaidi na aina ya watu wake na akili zao, ndio maana unaweza kuona nchi zenye rasilimali kidogo sana kama Japan, Israel, Singapore, Belgium, Switzerland, Taiwan zimeweza kuendelea zikiwa na rasilimali chache sana
Switzerland has Human Resources never forget that and it’s the leading country in the world in democracy
 
Hivi tunaongelea nini hapa !!!!

I Qoute.... ad verbatim "Samia says Russia / Ukraine tension an Opportunity for Gas Sales"

Sasa wewe unadhani that is diplomatically ?

Je hawezi kufurahia kimya kimya na kuuza kimya kimya (though its a pipe dream) and an America has a stake to play (has plenty of natural gas as well)

Before selling anything you have to condemn the act and distance yourself from the perpetrators can Tanzania do that like Kenya??
 
Yani Watanzania milioni 60 katika miaka 60 ya uhuru Muhongo peke yake ndiye tegemeo!
Unaweza kuonesha ni wapi nimesema kati ya Watanzania 60M ni Muhongo peke yake ndie tegemeo?
 
Back
Top Bottom