Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Ukiona hivyo, ujue KICHAA hamshirikishi VP kwenye maamz mengi ya uendeshaji wa masuala ya Taifa

Nchi haiwezi kumuachia mtu mmoja akaamua juu ya matumizi makubwa ya fedha kutekeleza mradi kama huu wa Stiegler's gorge bila kuwepo mjadala wa Taifa!! Fedha nyingi zitahitajika hivyo Rais asituburuze kujenga hili bwana kwa utashi wake ili hali kuna options nyingine bora za kuweza kufua umeme kwa bei nafuu na endelevu.

Tukumbuke kuwa tuna mabwawa ya kufua umeme ya Mtera na Nyumba Ya Mungu ambayo upatikanaji wa umeme wake unategemea kunyesha kwa mvua, na ndio maana miaka ambayo kunakuwa na ukame tunakuwa na mgao wa umeme!!! Hivyo hata tukijenga huo mradi mpya wa stiegler's gorgre nao pia utategemea kiasi cha mvua zitakazonyesha hivyo hakuna guarantee ya uzalishaji endelevu!!

Kuna vyanzo vingine vya nishati ya umeme ambavyo vingeweza kukidhi mahitaji ya nchi bila kuwa na athari zozote na kwa bei nafuu; tunaweza kufua umeme kwa kutumia upepo na pia jua au kama majirani zetu wa Kenya wanavyofua umeme wa GEOTHERMO!! Options zote hizi tunazo lakini inaelekea wakubwa bado wanataka mradi wa Stiegler's gorge utakaogharimu trillionS of shillings; bila shaka wana sababu zao, hopefully WASIWE WANATENGENEZA maingira ya KUIBIA NCHI kwa ESCROW nyingine tena!!
 
Wewe jamaa yangu fikirisha akili yako,maendeleo yoyote yale duniani yana gharama zake,
Tembelea maeneo yanachimbwa madini,migodi mikubwa kama North Mara,Geita Gold Mine,nakadhalika ,uone jinsi mazingira yalivyokua na yanavyofanana kwa sasa, bepari kalenga mzigo tu,na si vinginevyo
 
sawa Mimi Sina akili mtakapokuja fanya ukanda wa pwani uwe JANGWA NDO MTAELEWA
 
Kwani kwao wazungu siwanao umeme wakutosha mbona sisi hawataki tuwe nao?
Tukiwa na Umeme na Maji ya kijitosheleza tutakuwa tumejikwamua kimaendeleo na kiuchumi. Na hili suala "Wakoloni" hawataki kulisikia, ili waendelee kututawala kwa kutumia miradi ya Maji na Nishati ya Umeme.
Kuna kitu kinaitwa Poverty Trap....
Kwa sisi WaAfrika wamefanikiwa sana kututega katika MAJI na Nishati ya Umeme.
 
SIYO madesa kiongozi
unayo elimu yoyote kuhusiana na hydrology? achilia mbali mambo ya uhifadhi???????
Haihitaji elimu ya ekolojia au haidrolojia kujua kuwa ripoti za WWF ni biased;

Nimeisoma ripoti yao ya mwaka 2017 ina page 55, hapa ni swala la kuangalia faida za ziada za mradi wenyewe kwa uchumi kuliko kulinda wanyama zaidi.

Huu mjadala unanikumbusha debate ya uwepo wa Global warming au la, tumesikia hivi majuzi namna Trump mwenyewe anavyodai kuwa global warming ni propaganda tu. na hivi majuzi tu kesha tia saini executive order kwa ajili ya mambo ya energy inayoundermine baadhi ya environmental laws. Kama wao wenyewe hawajali mambo ya mazingira ili kukuza uchumi wao,

Kwanini waendelee kutudangaya na kutuibia haki ya kufanyia maamuzi rasilimali zetu?
 
Mradi ni muhimu. Na hilo bwawa la kilomita za mraba 12,000 ni bwawa gani hilo!!!?.
 
Gesi tayari ina mikataba tata isiyo na manufaa ya kutosha kwetu. Kumbuka tushaambiwa gesi mabepari washaichukua. Magufuli anafanya kitu sahihi mkii
Tutaamini vipi kwamba mradi huu hatutaambiwa "wamepewa watu wa Ulaya" baada ya yeye kuondoka madarakani?

Katika swala na mgogoro ule wa gesi ya Ntwara tuliaminishwa ni "yetu" na kwamba bei ya unit ya umeme itakuwa sawa na bure!

Leo miaka mitatu baada ya kukamilika tunaambiwa sio gesi yetu!...

Naomba nitunze kidogo my benefit of dout katika Mradi huu wa Stiggler hasa nikiona ni msukumo kama ule ule wa kulazimisha gesi iende Dar!
 
Mradi ujengwe tu maana manufaa ya kiuchumi ni makubwa kuliko hizo athari za kimazingira. Tunahitaji umeme wa uhakika kwa nchi nzima. Hao viumbe laki 2 watakaoathirika wamehesabu mpaka nyoka na kenge wasio na faida kwetu.
Nathani kunamahali watanzania hatuna maarifa na ufahamu wa kutosha. Moja ya maeneo hayo ni umuhimu wa Mazingira!

Na kibaya zaidi tunaona mazingira yanawahusu wao, sie hayatuhusu kabisa.

Umeme unafaida gani kama utakumbwa na madhara ya uharibifu wa ikolojia na mazingira kwa ujumla wake?
 
Kwa hiyo viumbe 200,000 n muhimu kuliko WaTz MIL 50? Mungu amemtupatia dunia tuitawale, siyo itutawale... Yaani vipepeo, mbu, kenge nk vituzuie kupata umeme. Tutachekwa kila mahali, mpaka na shetani!
 
SWALA LINALOHUSU NISHAT YA TAIFA NALIUNGA MKONO. HATA LEO SERIKALI IKISEMA INATAKA IRUTUBISHE URANIUM KWA AJILI HIYO NITAUNGA MKONO.
ila tu mikataba na zoezi zima lisihusishe aina yoyote ya ufisadi/upigaji 10%

ahsante!
 
Gesi tayari ina mikataba tata isiyo na manufaa ya kutosha kwetu. Kumbuka tushaambiwa gesi mabepari washaichukua. Magufuli anafanya kitu sahihi mkii
Gesi wameichukuaje chukuaje hawa Mabeberu wakati inapatikana Mtwara pale? Fafanua plse!!!
 
SWALA LINALOHUSU NISHAT YA TAIFA NALIUNGA MKONO. HATA LEO SERIKALI IKISEMA INATAKA IRUTUBISHE URANIUM KWA AJILI HIYO NITAUNGA MKONO.
ila tu mikataba na zoezi zima lisihusishe aina yoyote ya ufisadi/upigaji 10%

ahsante!
Kwa CCM hii hilo sahau, tunaambiwa hata gesi si yetu tena ni ya mabeberu!!
 
KWANINI WAZUNGU WAKATI WANTAKA URANIUMU MATAIFA YALIKUBALI ENEO KUMEGWA LAKINI KWENYE SISI KUZALISHA UMEME IMEKUWA SHIDA
Nashangaa, na ni hapo hapo selous game reserve
 
Tukiharibu mazingira wakati mito inayoleta maji nayo inategemea mazingira mwisho wake utakuwaje?ni mpumbavu pekee ndie atakaeshindwa kujibu swali hili.
 
Moja ya nchi zinazoongoza uchafuzi wa mazingira
1. China
2. Usa ---> Ilijitoa
3. Next may be tz ---> kwa maslahi
4. Next.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…