Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Kitu kingine, ongeza nguvu sana kwenye social media na marketing. Uzuri ni kwamba kila kitu ni kipya tumia fursa hiyo kujitangaza. Wabongo wengi wavivu na wanadharau nguvu ya mitandao, au wanawekeza kidogo sana. Mtu katumia 100M+ ukimwambia tia 1M kwenye social media anakataa wakati hela inakuja.

Ukitumia mtandao vizuri na ukawa na consistency utapata wateja wengi na badala ya hesabu ya vyumba vinne kati ya 10 ukajaza zaidi ya hapo. Weka na mfumo wa kujua vyumba vipo wazi au vimejaa, utaratibu wa kufanya booking mapema, hakikisha breakfast haikosi hii sio utani.

Nyumba ya wageni inayotegemea bodaboda na wenyeji wajitutumue ndio waingie haijawahi kuishinda inayotegemea wageni. Sasa wageni watakujua vipi. Imagine hapa nimesearch polyclinic nikapewa hizi options, fikiria mtu anaenda hiyo wilaya akatafuta lodge zilizopo akapewa hiyo kati ya machaguo ya kwanza
 
Umesema jambo muhimu sana Mkuu

Nitafanyia kazi boss
 
Ushauri mzuri sana...siku hizi social media ni kila kitu
Tena afanye bidii kuiweka pia kwenye Google map
 
Mkuu hongera.

Lakini pia pole kwa uwizi wa watanzania. Hii nchi hovyo sana na hatutaweza kuendelea kwa kizazi hiki. Labda kutokee muujiza wa wale wenye uzalendo wa kweli kuchukua nchi.

Kuna wakati watu wanalaumu wachina eti kwanini wakipewa tenda kubwa za ujenzi wanaleta vibarua kutoka kwao uchina. Shida ni wizi wa watanzania kuanzia juu hadi chini.

Nchi ya hovyo sana hii. Watu wengi wa hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…