Hebu tuchangie kidogo, unamsomesha mtoto English Medium kuanzia chekechea mpaka form six, vyuo vikuu bora kwa sasa nchini mwetu ni vya serikali vikiongozwa na UDSM. Chuoni fani za kusoma kwa mfano ni MD(udaktari wa binadamu), Sheria, Uhasibu, Uhandisi, Uchumi, Sayansi ya kompyuta, ufamasia, udaktari wa mifugo, kilimo n.k Fani zote hizi kila moja ina lugha yake, vile vikiingereza vya kawaida havipo tena kule. Kimsingi kiingereza cha kawaida kinaishia shule ya msingi, baada ya hapo Physics ina lugha yake, Chemistry, Biology, Mathematics hali kadhalika. Mimi sioni mchango wa kiingereza kivile. Cha msingi hiyo shule ya serikali ifundishe vizuri. Shule km Mzumbe, Tabora boys and girls, Kibaha, Masalato, n.k ni shule nzuri sana. Cha maana serikali iboreshe shule zake, iwalipe walimu vizuri na kuwapatia motisha mbalimbali hakuna haja ya kulipa milioni nzima eti ada ya chekechea. Elimu ni mtu mwenyewe km ana nia. Unaenda kusoma computer science/engineering hivyo vikiingereza vyako unavipeleka wapi, kule ni code na logic. Hata vichaa kule kwao uingereza wanaongea kiingereza