Unajua sisi masikini huwa tunajifariji sana tusionekane tumeshindwa au hatuna hela. Utasikia yeye anaishi kwenye ghorofa mimi kwenye nyumba ya kawaida ila usingizi ni ule ule.
Hapa duniani kuna watu wanaishi na wengine wanapambana ili waishi.
Kuna watu watoto wao wanasoma kwenye shule za hela, maendeleo anafanya, akimaliza mtoto anaenda kusoma nje ya nchi km Canada. Sisi masikini ukipata hela, una fake maisha ili uonekane na wewe una hela.
Kuna watu wanakaa hoteli ya nyota 5 mwaka mzima akifanya shughuli zake yaani kifupi hela kwake siyo tatizo.
Huyu bwana hakuwa na hela ila alifake maisha aonekane na yeye ana hela matokeo yake akarudi kwenye uhalisia.
Kuna watu wanahela na hela kwao siyo tatizo.