Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunao watoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"
Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa " faida" nitakazo zipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.
Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:
1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapo fika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.
2. Sintokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote( ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanao soma kayumba wanaenda shule.
Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa
1. Binti yangu ( yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko walio soma shule za kiingereza.
3. Brother wangu wa mtaani ambae na yeye kawarudisha watoto wake kayumba.. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary. Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.
Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa" anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu"
Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..
Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.
Akaongeza " shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini ( ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake)
Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.
MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.
Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa sh.laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni" wewe ukiwa na hela yoyote hata laki TANO niite kwa lako TANO hiyo hiyo nitafanya kitu . Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kino garden au hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anao wajengea nyumba anasema ' huyu anauza mchicha' huyu mama lishe, etc. Nikawa inspired.
Kuhusu somo la kiingereza: nimenunua vitabu na cds ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.
Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.
Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.
Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.