Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Tatizo ni umasikini
Huo ndio ukweli kwamba mtu kafika kiwango ambacho vipaumbele vinashindana (apeleke mtoto shule nzuri ya ada kubwa au apeleke ya kawaida na pesa inayobaki afanyie mengine) maana kipato cha familia kidogo. Kingine kilicho wazi ni maandaliz kwa mzazi ambaye alijiandaa toka hajapata watoto na akatafuta kipato kizuri toka mapema ina maana uchumi wake unaweza kuhimili kupeleka watoto hizo shule, kufanya uwekezaji, n.k kifupi kujikuna kunaendana na urefu wa mkono. Haya mengine ni ya kujipa moyo tu!
 
Hebu tuchangie kidogo, unamsomesha mtoto English Medium kuanzia chekechea mpaka form six, vyuo vikuu bora kwa sasa nchini mwetu ni vya serikali vikiongozwa na UDSM. Chuoni fani za kusoma kwa mfano ni MD(udaktari wa binadamu), Sheria, Uhasibu, Uhandisi, Uchumi, Sayansi ya kompyuta, ufamasia, udaktari wa mifugo, kilimo n.k Fani zote hizi kila moja ina lugha yake, vile vikiingereza vya kawaida havipo tena kule. Kimsingi kiingereza cha kawaida kinaishia shule ya msingi, baada ya hapo Physics ina lugha yake, Chemistry, Biology, Mathematics hali kadhalika. Mimi sioni mchango wa kiingereza kivile. Cha msingi hiyo shule ya serikali ifundishe vizuri. Shule km Mzumbe, Tabora boys and girls, Kibaha, Masalato, n.k ni shule nzuri sana. Cha maana serikali iboreshe shule zake, iwalipe walimu vizuri na kuwapatia motisha mbalimbali hakuna haja ya kulipa milioni nzima eti ada ya chekechea. Elimu ni mtu mwenyewe km ana nia. Unaenda kusoma computer science/engineering hivyo vikiingereza vyako unavipeleka wapi, kule ni code na logic. Hata vichaa kule kwao uingereza wanaongea kiingereza
 
Hata kama una pesa lazima ujifunze kubana matumizi.
Sio busara kulipa milioni4 ili mtoto afundishwe A for Apple. Mwisho wa siku maisha ndo haya haya
 

Moderator hii comment naomba mu ipin. Komenti iliyo kwenda shule.

Mkuu , You are the true son of your father.

Baba ako hakusingiziwa. Wewe ni mtoto wake kabisa.
 
Ila maisha yanaenda haraka sana, kipindi chetu tunaingia sekondari miaka ya themanini mwishoni, kusoma private ilikuwa aibu maana ni kwa wale waliofeli, leo kusoma huko ni fahari, kisa kiingereza na ada kubwa. Tumejiwekea social classes kutumia hizi shule, ambaye hana uwezo naye anajifaragau aoneka yumo wakati huo anateseka. Mwisho wengine wanakuja kuuza baa na vikiingereza vyao. Shule mtoto anatakiwa apige vizuri Hisabati na masomo ya sayansi yakiwemo ya uchumi na biashara hayo ndiyo maisha siyo lugha ya watu, bado ni utumwa tu.
 
Kuwajengea nyumba ni Investment? Wewe akili huna.Ungesema unawaanzishia biashara ungeeeleweka .Nyumba na viwanja vyako vya kipuuzi vitawasaidia nini?

Wahindi maisha yao wanapanga wanadomesha watoto.best schools na watoto wao wana maisha mazuri mno.pamoja na watoto wao hawaishi uswahilini wanaishi katikati ya miji maisha mazuri mno wote wazazi na watoto kuliko wewe mwenye viwanja vya hovyo nje ya mji huko uswahilini

Nyumba na viwanja.navyo ni vitu vya kujivunia kuwa ume sacrifice watoto wasome Kayumba kisa ubaki na vihela koko vya kuwajengea nyumba na kuwanunulia viwanja koko nje ya mji huko uswahilini?

Wewe akili zimo kichwani kweli?
Unaelewa maana ya sacrifice?
 
Ndo maana nikasema umasikini na vipaumbele, wanaosomesha watoto wao shule international lengo lao ni mtoto kuelimika na kuwa tofauti na wengine.

Wanaosomesha English medium lengo lao jinginw

Wanaosomesha Elimu Bure wengi wao ni kutokana na umasikini
 
Hata mimi kipato kilipokata nikatoka kwenye steki na soseji nikaingia kwenye dagaa wale wanaokaangwa barabarani, nikawasifu sana kwa utamu wake na ubora wake kwa kurumangia dona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…