Mrejesho: Harakati za kutafuta mpaka kuandikishwa JWTZ

Mrejesho: Harakati za kutafuta mpaka kuandikishwa JWTZ

mkuu tupo wote katika hili. Mimi nlienda jkt mujibu wa sheria na kwenye kulenga shabaha nlikuwa wapili na nliambiwa ntapigiwa simu baada ya mafunzo kuisha pamoja na aliyekuwa msindi wa kwanza lakin mpaka leo simu hazijaitaga kabisaa
 
Ahaaah, watakupigia tuu mkuu kuwa na subira, tunza afya.
 
Habarini ndugu ?

Ninawashirikisha baadhi ya harakati nilizofanya katika kutafuta kuandikishwa na kuwa askari JWTZ.

Ni ndoto yangu tangu nikiwa mdogo kiumri kuwa askari wa JWTZ hususa ni kuwa komandoo. Baada ya kuhitimu kidato cha nne nilitaka kwenda jeshini wazazi wangu wakanikatalia wakasema niende kidato cha tano kwa maana nilifaulu vizuri, nikaenda huko nikahitimu pia. Nilienda JKT kwa mujibu wa sheria sikubahatika kupata nafasi ya kubakizwa na kuendelea na jeshi la wananchi badae wazazi Wakanitaka kwenda chuo kikuu nikaenda kusoma nikahitimu shahada ya sayansi katika fizikia mwaka 2017.

Baada ya Kuhitimu chuo kikuu nilipambana sana kurudi jeshini ila sikufanikiwa. Nilitaka kuachana na haya masuala ya kutafuta uanajeshi lakini kila mda nafsi ikawa inaumia😭😭😭 na kuniambia kuwa ninatakiwa kupambana kwa namna yoyote ili mwishowe nikaitumikie nchi yetu ya Tanzania kupitia kuwa askari JWTZ, Ninaumia sana roho kutokuwa huko mpaka mda huu. Kwa kuwa sina mbanga wa kunisaidia nikaona mbanga ni mimi mwenyewe nikapambana.

Nikafanya maamuzi magumu sana nikabadili majina, nikafanya mtihani wa QT nikafaulu, mwaka uliofuata nikafanya mtihani wa kidato cha nne kama private candidate nikafaulu pia. Nikatafuta na nyaraka zingine muhimu nikazipata ili nikasome kozi ya afya ambayo jeshi linataka halafu nikiihitimu hiyo diploma basi nirudi JKT nikajitolee, ili nafasi za kuandikishwa JWTZ zikitolewa basi nifanye usaili nijiunge nao Tatizo likawa kupata kitambulisho cha NIDA chenye namba ya NIDA, majina na mwaka wa kuzaliwa tofauti na ile NIDA yangu ya kwanza, nilipambana kweli kweli lakini sikufanikiwa watu wa NIDA hata nilioahidi chochote kitu wakakataa na kuniambia haiwezekani. Oparesheni yangu niliyoipa jina la Oparesheni kuandikishwa jeshini ambayo ingechukua miaka saba, ikafeli !

Rejea huu uzi 👇

Nikajaribu kutafuta mtandaoni nchi ambazo zinapokea watu ambao sio hata raia wao ili wawe wanajeshi wao nikaona ni ufaransa kwa programu yao ya French Foreign Legion (FFL) lakini ni gharama sana mpaka kuweza kufanikiwa kuandikishwa FFL maana kuna gharama za visa za kusafiria, kuna nauli ya ndege, kuna hela ya kutumia kipindi mchakato wa usaili ukiendelea, na sina hiyo hela maana kwa sababu sijafanikiwa kujiunga na JWTZ labda ningefanikiwa kule FFL kwa kutumia hela.

OMBI KWA JWTZ: Kuna askari mna umri wa kuweza kuwa hata baba zetu lakini bado mpo jeshini. Kuna vijana tuna umri mdogo kuliko ninyi tunahitaji sana kuwa askari wa JWTZ, tunaomba mtupe nafasi na sisi pia tuje huko tutumikie wote hii nchi kupitia huko maana tunahitaji sana, Tusije kufa na ndoto zetu hazijatimitia. Roho inaniuma sana kukosa jeshi na miaka yangu hii 34 wakati kuna watu mna miaka 50 bado mpo sana mkilitumikia jeshi letu miaka kumi au na zaidi ya hapo, kwa nini mtubague sisi tulio na umri wa chini yenu ? Vita ikitokea mtatuwekea vigezo hivyo hivyo mnavyotuwekea au mnahisi tunafuata posho za jeshi tuu 😭😭😭 ? si tungekuwa wafanyabiashara kama malengo yetu ni kuwa mabilionea ?

Tafadhali tupeni nafasi, tukifia mazoezini kwa sababu ya umri wetu mnaoita ni mkubwa, ni vizuri tuu tutajivunia kuwa tumefia mazoezini JWTZ kuliko kufa kwa visababishi vya hovyo.

Ninawatakieni majukumu mema.​
Tunaweza anzisha jeshi letu mkuu, kama upo tayari. Lengo ni protection kwa nchi yetu
 
Una poteza muda wako Bure kijana
Tafuta maisha jeshi na umri huo we ume sikia wap?
 
Kama unataka kwenda ufaransa inawezekana endelea kuzichanga na ukae mbali na mademu utatoboa
 
Hizi ndio ndoto ambazo wachache sana mnazo,hakika kupitia andiko lako nimejifunza kuwa kuna watu ambao mkiamua jambo lenu mnapambana mpaka mnalifanikisha,,endelea kupambana

Lakini upande wa pili hapa nawalaumu wazazi wako ambao wameshindwa kujua ndoto uliyo kuwa nayo,naamini kabisa kama wangefanikiwa kusoma andiko hili naamini kabisa wangejilaumu sana kwa huu ukatili walio ufanya bila kudhamiria,najua walikuwa na plan nzuri na maisha yako lkn hawakujua kuwa jeshi ndio maisha yako

Ni somo zuri kwa sie wazazi ambao wenetu wanakua,ebu tujaribu kufahamu ndoto za vijana wetu,tuwasikilize na kujua nini hasa wanahitaji katika maisha,naamini kazi si kupata mshahara mzuri tu bali na mapenzi juu ya hiyo kazi yanapaswa yawepo

Ila kongole sana mwamba kwa kupigania ndoto zako hata kama bado hujafanikiwa lkn umetufundisha kukomaa kwa kile tunachokiamini
 
Majina hubadilishwa mbona hiyo huduma IPO unakana majina yako unachukua mengine
Namba ya nida si inabakia ileile haibadiliki ? Nimewaambia pia wanisajiri bila alama za vidole kama shida ni fingerprint nipate ile namba na kitambulisho kingine nifanye harakati wamenigomea kuwa haiwezekani.
 
Dah nawaza tu hizi Juhudi ungezielekeza kwenye Mambo mengne si Ungekuwa mbali Sana?

But anyway Usikate tamaa, unaweza kufanikiwa
Naam ndugu BARON99 yote ni katika kupambania ndoto yangu kwa kazi ninayopenda sana ya jeshi. Asante
 
Hizi ndio ndoto ambazo wachache sana mnazo,hakika kupitia andiko lako nimejifunza kuwa kuna watu ambao mkiamua jambo lenu mnapambana mpaka mnalifanikisha,,endelea kupambana

Lakini upande wa pili hapa nawalaumu wazazi wako ambao wameshindwa kujua ndoto uliyo kuwa nayo,naamini kabisa kama wangefanikiwa kusoma andiko hili naamini kabisa wangejilaumu sana kwa huu ukatili walio ufanya bila kudhamiria,najua walikuwa na plan nzuri na maisha yako lkn hawakujua kuwa jeshi ndio maisha yako

Ni somo zuri kwa sie wazazi ambao wenetu wanakua,ebu tujaribu kufahamu ndoto za vijana wetu,tuwasikilize na kujua nini hasa wanahitaji katika maisha,naamini kazi si kupata mshahara mzuri tu bali na mapenzi juu ya hiyo kazi yanapaswa yawepo

Ila kongole sana mwamba kwa kupigania ndoto zako hata kama bado hujafanikiwa lkn umetufundisha kukomaa kwa kile tunachokiamini
Asante sana, nimekuelewa ndugu.
 
mkuu tupo wote katika hili. Mimi nlienda jkt mujibu wa sheria na kwenye kulenga shabaha nlikuwa wapili na nliambiwa ntapigiwa simu baada ya mafunzo kuisha pamoja na aliyekuwa msindi wa kwanza lakin mpaka leo simu hazijaitaga kabisaa
toka 2019 hadi leo ni miaka 6 mkuu imepita so mambo ni mengi ikotokea sawa. maana nlitamani sana kuwa sniper wa jwtz lakini ilshindikana. NACHOWEZA KUSEMA NI NANI ALIYE KARIBU NA WEWE ALIYEPO KWENYE MFUMO ILI AKUBEBE? KAMA HAKUNA BRO KWA SASA BAHATI HAKUNA
 
Back
Top Bottom