Mrejesho: Harakati za kutafuta mpaka kuandikishwa JWTZ

Mkuu umri umeshaenda, huwezi kupata nafasi jeshini. Labda uende sehemu zenye vita kama Ukraine ukajitolee.
 
Mkuu umri umeshaenda, huwezi kupata nafasi jeshini. Labda uende sehemu zenye vita kama Ukraine ukajitolee.
Ni kweli mkuu ila ujue kuna watu wana umri wa baba yangu bado wanafanya kazi jeshini sasa ukubwa wangu sio shida kabisa. Kuhusu kwenda nchi ya nje kujitolea ni vizuri, ila lazima mtu awe na hela ya kutosha milioni kadhaa, mimi sina.
 
Ambaye ana ufahamu na haya masuala ninaomba anipe ufafanuzi.
 
Pole sana kwa changamoto hiyo sasa ngoja nikupe yangu utoana siyo wew tu unayo pitia hayo.

Mm nilikuwa na ndoto kubwa sana ya kwenda jeshini lakn ilishindikana JWTZ ,nikajaribu UHAMIAJI ikashindikana nikajaribu MAGEREZA bado ikashindikana na mwisho kabisa nilijarobu polisi pia sikupata nafasi .

Japo kuwa polisi ni kazi ambayo siipendi kabisa .lakini ilibidi niombe tu!

Ndoto za jeshini zilianza miaka mingi kwanzia kipindi nipo mtoto nilikuwa napenda na akili zangu zilivyo kuwa zinaongeza na kukua nilidhi kupenda na kuweka juhudi kubwa kufanikisha ndoto yangu .lakin ilikuwa ni ndoto ya mchana niliyo kuwa na otaπŸ˜‚

Nilivyo fika kidato cha pili ndio nilianza kujua kwamba kunakozi inaitwa military science naniliwekeza nguvu kubwa kwenye kusoma masomo ya science hivi niwe na msingi bora huko mbele . Nilenda kidato cha tano na sita na kuhitimu

Nilijiunga na mafunzo ya mujibu wa sheria .ilikuwa nimesha chunguza kido go kuhusu OP zilizo tangulia usahili ulifanyika wap?.kama miaka mitatu nyuma hivi

Na kikosi nilichoenda ndio uamsaili ulipo fanyikia .nilifanya usahili vizuri na kwa combination yetu tulikuwa wachache sana mm nilisoma PGM. Tulikuwa?wa chache sana kulinganisha na combination nyingine kama PCB,CBG,EGM,HGE na ECA walikuwa wengi sana PGM na PMC ndio tulikuwa wachache.

Tuka ambiwa kila kitu kipo vizuri tusubiri kupigiwa cm lakn kwa bahati mbaya hamna ata 1 ninaye mjua alipigiwa. Hiyo simu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Nikaomba JWTZ nikawe ata private lkn bado nilikosa tena nilitumia na gharama kubwa lakin wap😀😀

Nikapiga moyo konge omba jeshi la uhamiaji lakn wapπŸ˜‚πŸ˜‚

Nikajaribu magereza lakn wap?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mwisho kabisa nikaona bora niende polisi ambayo siipendi ila kwa sababu tu nashida lakn bado ata hapo nilikosa πŸ˜…

Mwisho japo siyo kwa muhumi kwa hii tanzania kama una connection wew usiangahike kabisa .utajikuta unapoteza ela ,muda na bado utakosa tuu . Mm nakushauri wew achana na hayo mambo kama unataka labda tengeneza connection kwa ajili ya watoto wako siyo wew tena.
 
Tafuta familia ya mwanajeshi mmja Jenga nae mahusuano mazuri mkuu
 
Huwezi kwenda kwa umri huo mkuu

Unless una connection kubwa sana ya mtu kukupeleka.

Nakushauri fanya ishu zingine tu.

Wanaofanya kazi wakiwa na umri mkubwa unaosemea wao walianza kazi wakiwa vijana miaka 22 unakuta 21 sasa una 34 kama sikosei
 
Pole mkuu, inaumiza sana kuishi nje na ndoto. Kama umri unakuruhusu nenda JKT ukajitolee ya Mungu ni mengi unaweza kubahatika ukapata nafasi kupitia huko.
 
Pole mkuu, inaumiza sana kuishi nje na ndoto. Kama umri unakuruhusu nenda JKT ukajitolee ya Mungu ni mengi unaweza kubahatika ukapata nafasi kupitia huko.
Umri bado unaruhusu lakn cheti cha jkt ninacho kwenda kule bila connection nikupoteza muda tuu. Amin nakwambia
 
Tafuta familia ya mwanajeshi mmja Jenga nae mahusuano mazuri mkuu
Kipaji cha kujipendekeza kwa watu sina. Watu ni wachoyo sana, hata ukiwa na urafiki nao hawawezi kukusaidia. Atasaidia ndugu zake wa damu tuu ila siyo wewe kwa hiyo ni kupoteza mda ndio maana nilikuwa ninapambana mimi mwenyewe.
 
Tall or short, if your mind does not work well you are just a fool.
Yani unagraduate unaamua kurudi tena form four?
Very foolish.
 
Tall or short, if your mind does not work well you are just a fool.
Yani unagraduate unaamua kurudi tena form four?
Very foolish.
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Asante ndugu kwa kuandika ujumbe wako katika huu uzi. Ukipata mda karibu tena uandike ujumbe mwingine wa maandishi πŸ™.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…