Mrejesho: Kilichotokea baada ya mke wangu kurudi saa sita usiku

Mrejesho: Kilichotokea baada ya mke wangu kurudi saa sita usiku

Kaza buti visa viko vingi mno, namna ulivyoanza story yako hustahili kuonewa huruma, na baadae umesema mkeo anajua michepuko na kataja, sasa kwa kuwa wewe ndiye uliemuoa ungepiga mpaka ashindwe kwenda kazini wiki zima.
Kupiga hata hakusaidii. Muhimu ni kuzungumza. HAMNA KITU NACHUKIA KAMA MWANAUME ANAEMPIGA MKEWE. HATA KOSA LIWE LIPI. JAMAA KAMPIGA NGUMI YA USO MKEWE. SASA ANGEMPOFUA! YEYE NAE NI MTOTO WA MTU.
 
Mkuu nipo kwenye ndoa mwaka wa kumi na mbili sasa...nakushauri kitu ambacho nakijua wewe utaamua cha kufanya lakini jukumu la kukushauri ni jukumu langu.

1.usimuache kabisa huyo mke wako
2.wake za watu wanaliwa sana, ikiwemo wangu
3.usisahau na wewe una mchepuko
4.kinachowaunganisha ni watoto na ndio watakaoumia
5.vumilia,fatilia,mkanye,kuwa mkali ila usimuache...

nicheki Pm nikupe namba yangu kwa ushauri zaidi
 
Mkuu mi sijaoa,

Lakinj nashauri Umsamehe mwenzio mkae muishi pamoja na kukea watoto.

Kwa sababu kama kucheat na wewe ulicheat, kama kuumia nae aliumia the same sasa tazama usaliti wake ni kama malipo ya dhambi zako. Ukijitazama peke yako utaishia kuwatesa watoto tu kaka.

Katima Uandishi wako umeonekana kuwa Objective sana naaminj utanisikiliza.

Tubu, Tulia na mkeo, msihi nae atulie mjenge Familia yenu.
Ushauri huu hapa kabunda88

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Wanaondoa wengi wanavumiliana kwa sababu ya watoto..
Watoto bado wadogo hao..

Kama mnaishi nyumba kubwa, hakuna haja ya kumfukuza..
Hama chumba, jitengee chumba chako...kaa kimya na mambo yako...

Ukitaka kutoka, toka kimya kimya na asikuhoji why..

Matumizi ya familia mpatie ikiwezekana mtumie kwa mpesa japo mpo nyumba moja.

Hudumia wanao...

Kwa adhabu hii lazima atajirudi, na asipo jirudi ataondoka mwenyewe na weww utakuwa kwenye upande salama kuwa Hujamfukuza bali kaondoka mwenyewe.
 
Mkuu nipo kwenye ndoa mwaka wa kumi na mbili sasa...nakushauri kitu ambacho nakijua wewe utaamua cha kufanya lakini jukumu la kukushauri ni jukumu langu.

1.usimuache kabisa huyo mke wako
2.wake za watu wanaliwa sana, ikiwemo wangu
3.usisahau na wewe una mchepuko
4.kinachowaunganisha ni watoto na ndio watakaoumia
5.vumilia,fatilia,mkanye,kuwa mkali ila usimuache...

nicheki Pm nikupe namba yangu kwa ushauri zaidi

Asante mkuu
 
Hapo kama kweli umeoa basi huna mke kabisa ndugu! Ni ukweli mchungu ila lazma niuseme tu, mke kukosa hata tone la aibu na kuleta ubishi wakati kitu kafanya na ushahidi wa kimawasiliano unaashiria hilo ni dharau! Ukimsamehe tegemea matukio mazito zaidi...

Maamuzi ya mke kuchepuka anayafanya akijua kabisa madhara yake ni fatal wala sio kwamba shetani au vipi! Amefanya kusudi kuchepuka na alipanga kabisa hilo!

Hicho unachopitia niliwahi pitia ila mie nilimfumania akiwa na msela chumbani kwangu kabisa japo walikuwa hawajaanza kusex!
Kumbe pamoja na utata wako kidume kilishaletwa mpaka home?
 
Pole sana,tunza watoto,ila kama una moyo mgumu kama Nduli(Mimi ninao),usiondoke nyumbani,hama kitanda tu,Ili watoto waendelee kukuona,fanya juu chini watoto waendelee kuwaona wote pamoja,watakushukuru siku moja maishani,usikimbilie kutafuta mwingine,jipe muda,mkeo anaweza akabadirika akawa kama maraika ukakuta mnaongeza watoto wengine wawili,jipe muda kidogo,watoto wakishakuwa wakubwa,kwenye miaka 12/14 hapo ukitaka kutengana kabisa ni poa,ila iwe ni last option.
Umeshauri vizuri sana na kiutu uzima. Kuachana na mke kuna changamoto sana. Unaweza ukafanya kwa hasira ila madhara yake ni makubwa mno kuanzia kwa watoto wako, mke utakayemuoa na watoto utakaowazaa na hiyo mke.

Ni muhimu kuwa mtulivu sana wakati huu na wala usichukue maamuzi yoyote mpka hasira ziishe.

Usimsemeshe tena mkeo kuhusu hilo jambo. Unaweza kuchukua simu yake ukakusanya ushahidi kwa ajili ya hatua za baadae kama mambo yakishindikana
 
Mijanaume mingine ni wapuuzi sana, ukute ana matukio ya kutosha yaliyomfanya mke wake achepuke halafu anakuja hapa apate ushauri na huruma kutoka kwa mabaharia wenzake.
Simtetei mke ila kuweka wazi kuwa na yeye ana mchepuko na wala hajutii ni ukosefu wa akili.
Amekomeshwa na hata akiachana na mke wake kidonda alichokipata hakitafutika kamwe. Wazinzi wote they deserve each other.
Mie pia nasimama na mkewe, maan huyo mkewe amefanya hivyo kwa kulipiza kisasi kwa matukio ya mumewe, maaan amesema mkewe kataja wanawake anaohisi anatembea nao, na ukweli kawapatia wote sasa hapo nn?
Mkewe hana kosa lolote, tiba ya usaliti ni kisasi.
 
Unafikri jana angekua kapokelwa na mchepuko angeyajua haya ya mke kurud saa sita 6 kuna muda mchepuko unasaidia kulinda ndoa imagine sasa hv ndoa inaelekea kufa kisa mchepuko kapitiwa na usingizi hii jeur ya kulala na babe wake anarud kaitoa wapi?
[emoji23][emoji23][emoji23] sasa, mchepuko unataka kuchukua nafas ya ndoa.
 
Back
Top Bottom