Mrejesho: Kilichotokea baada ya mke wangu kurudi saa sita usiku

Kaza buti visa viko vingi mno, namna ulivyoanza story yako hustahili kuonewa huruma, na baadae umesema mkeo anajua michepuko na kataja, sasa kwa kuwa wewe ndiye uliemuoa ungepiga mpaka ashindwe kwenda kazini wiki zima.
Kupiga hata hakusaidii. Muhimu ni kuzungumza. HAMNA KITU NACHUKIA KAMA MWANAUME ANAEMPIGA MKEWE. HATA KOSA LIWE LIPI. JAMAA KAMPIGA NGUMI YA USO MKEWE. SASA ANGEMPOFUA! YEYE NAE NI MTOTO WA MTU.
 
Mkuu nipo kwenye ndoa mwaka wa kumi na mbili sasa...nakushauri kitu ambacho nakijua wewe utaamua cha kufanya lakini jukumu la kukushauri ni jukumu langu.

1.usimuache kabisa huyo mke wako
2.wake za watu wanaliwa sana, ikiwemo wangu
3.usisahau na wewe una mchepuko
4.kinachowaunganisha ni watoto na ndio watakaoumia
5.vumilia,fatilia,mkanye,kuwa mkali ila usimuache...

nicheki Pm nikupe namba yangu kwa ushauri zaidi
 
Ushauri huu hapa kabunda88

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Wanaondoa wengi wanavumiliana kwa sababu ya watoto..
Watoto bado wadogo hao..

Kama mnaishi nyumba kubwa, hakuna haja ya kumfukuza..
Hama chumba, jitengee chumba chako...kaa kimya na mambo yako...

Ukitaka kutoka, toka kimya kimya na asikuhoji why..

Matumizi ya familia mpatie ikiwezekana mtumie kwa mpesa japo mpo nyumba moja.

Hudumia wanao...

Kwa adhabu hii lazima atajirudi, na asipo jirudi ataondoka mwenyewe na weww utakuwa kwenye upande salama kuwa Hujamfukuza bali kaondoka mwenyewe.
 

Asante mkuu
 
Kumbe pamoja na utata wako kidume kilishaletwa mpaka home?
 
Umeshauri vizuri sana na kiutu uzima. Kuachana na mke kuna changamoto sana. Unaweza ukafanya kwa hasira ila madhara yake ni makubwa mno kuanzia kwa watoto wako, mke utakayemuoa na watoto utakaowazaa na hiyo mke.

Ni muhimu kuwa mtulivu sana wakati huu na wala usichukue maamuzi yoyote mpka hasira ziishe.

Usimsemeshe tena mkeo kuhusu hilo jambo. Unaweza kuchukua simu yake ukakusanya ushahidi kwa ajili ya hatua za baadae kama mambo yakishindikana
 
Mie pia nasimama na mkewe, maan huyo mkewe amefanya hivyo kwa kulipiza kisasi kwa matukio ya mumewe, maaan amesema mkewe kataja wanawake anaohisi anatembea nao, na ukweli kawapatia wote sasa hapo nn?
Mkewe hana kosa lolote, tiba ya usaliti ni kisasi.
 
Unafikri jana angekua kapokelwa na mchepuko angeyajua haya ya mke kurud saa sita 6 kuna muda mchepuko unasaidia kulinda ndoa imagine sasa hv ndoa inaelekea kufa kisa mchepuko kapitiwa na usingizi hii jeur ya kulala na babe wake anarud kaitoa wapi?
[emoji23][emoji23][emoji23] sasa, mchepuko unataka kuchukua nafas ya ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…