Mrejesho kuhusu kupima DNA za watoto wangu

Mrejesho kuhusu kupima DNA za watoto wangu

Hongera Mkuu.

Kama Wakili amekupa nakala ya matokeo, itunze sehemu salama. Naamini atakuwa amekuambia namna hiyo nyaraka ilivyo sensitive, kama hajakupatia pia inabidi umuelewe Mkuu sababu hayo majibu sio yako ni ya kwake Wakili.
Kweli kabisa. Pia jamaa aseme wazi kama nakala anayo.
 
Majibu ya DNA Huwa siyo ya kweli..in most cases huwa wanaangalia Zaidi ustawi wa mtoto..coz wanaangalia wakikiuambia wewe siyo baba hao watoto wataishije...refer case ya Diamond na Hamisa
 
Majibu ya DNA Huwa siyo ya kweli..in most cases huwa wanaangalia Zaidi ustawi wa mtoto..coz wanaangalia wakikiuambia wewe siyo baba hao watoto wataishije...refer case ya Diamond na Hamisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mondi +mobeto = nenga
 
Miezi kadhaa imepita niliandika uzi humu nikasema nitaenda kupima DNA watoto wangu.

Nilipatiwa muongozo kwenye ule uzi na baadhi ya wanasheria/mawakili waliomo humu ikabidi kumjulisha wakili wangu akasema inawezekana na ni rahisi sana.

Nashukuru nimekuta mabao yote ni yangu, I felt like Messi for a while, hahahahahaaa.

Naendelea kuwashauri wanaume wenzangu kuzingatia kupima DNA za watoto wenu, kulea mtoto asie wako watakuja kukuletea shida ukubwani.

Ciao

Fanya mchakato upime tena sampuli ziende south Africa au Kenya Nairobi then ulete mrejesho tena
 
Miezi kadhaa imepita niliandika uzi humu nikasema nitaenda kupima DNA watoto wangu.

Nilipatiwa muongozo kwenye ule uzi na baadhi ya wanasheria/mawakili waliomo humu ikabidi kumjulisha wakili wangu akasema inawezekana na ni rahisi sana.

Nashukuru nimekuta mabao yote ni yangu, I felt like Messi for a while, hahahahahaaa.

Naendelea kuwashauri wanaume wenzangu kuzingatia kupima DNA za watoto wenu, kulea mtoto asie wako watakuja kukuletea shida ukubwani.

Ciao
Majibu ya DNA Kwa Tanzania hii wanasema yanaweza yakawa si sahihi. Ili kuepusha migoro wanakuambia ni wa kwako.
Hongera lkn.
 
Kati ya mambo sitokuja fanya maishani mwangu ni kujaribu kupima DNA kutafuta uhalali wa mtoto wangu kama ndie au sie..
Ukute mchepuko wa mkeo,unamwambiaga mkeo amzalie mtoto,ila hofu inamfanya (mchepuko) asimpe mimba mkeo,kumbe mume wala huna wasiswasi na ukute mkeo anajua kua huna shida,ila michepuko yake ndiyo insmfelisha,ndoa hizi bhana.
 
We unafkri ofisi ya mkemia ni wajinga wakuambie SI wako?...

sababu zilizokufanya ukapime DNA ,ndio majibu ya kweli kwamba kwenye watoto wako Kuna uncertainty....
 
Watu kibao wameambiwa migonjwa mikubwa mikubwa au wengine kuonekana hawana matatizo yoyote japo wanaumwa lakini walipoenda kwingine wakapata majibu tofauti sasa wewe endelea kufurahia tu.
 
Haya mambo ni magumu yaache tu
Ex anapewa mchana usiku unapewa wewe ujui ya nani imenasa
 
Kuna kipindi mkemia mkuu wa serikali alisema asilimia kubwa ya wanaopima watoto wanakua sio wao ila wanaambiwa ni wao ili kupunguza watoto wa mtaani.
mradi tu kumpunguza mwenzio Handas! AHAAHAHAHHAHAHA nimecheka sana! Hata mimi kama mtu wa maabara wewe, nianze tu kusema huyu mtoto sio wako na wewe ndo mume na ndo baba umemlea toka anazaliwa! Weeee nakupa tuuuuu!
 
Kwann usifanye dna ya asili mkuu,angalia vitu ambavyo mnavyo kwenu kwenye ukoo kama alama,meno vidole mbona simple sana,mfano ss kwetu tuna alama mbili tunazo mgongoni yaan ukoo wote tunavyo aisee awe wa kike au kiume wote lazima wawe na alama,asipokua na alama huyo siyo wetu!
 
mradi tu kumpunguza mwenzio Handas! AHAAHAHAHHAHAHA nimecheka sana! Hata mimi kama mtu wa maabara wewe, nianze tu kusema huyu mtoto sio wako na wewe ndo mume na ndo baba umemlea toka anazaliwa! Weeee nakupa tuuuuu!
Ndio maana nikamwambia hapo angekua na uhakika kama huyo mpimaji wa maabara either ni ndugu yake au jamaa wake wa karibu!! Otherwise kazi anayo bado
 
Back
Top Bottom