MREJESHO: Uzoefu wangu wa kutapeliwa na member, jihadhari!

MREJESHO: Uzoefu wangu wa kutapeliwa na member, jihadhari!

Ndugu Zangu Majizi Yapo Hata CCM
Nasema Uongo Ndugu Zangu ?
By Mzilankende, Jiwe, Chuma
 
Kuna id moja hivi ya m.ke humu ndani ilitaka kunitapeli na aliandika thread kabisaa ya kutafuta Mwani nikamwambia kwa huku Zbr unapatikana akapiga domo weee mara anataka vithibitisho kumbe mwisho wa siku ananambia nimtumie 15k hhhhh ndo mwisho wa maongezi
Tena katumia karibia ya wiki kutaka iyo pesa
 
Ni lazima wajinga wawepo ili wajanja waweze kuishi, wajinga ni chakula ya wajanja, kama ilivyo nyumbu kuwa chakula cha mamba
 
Natumai wote mko salama.

Napenda kushiriki kwa uchungu na tahadhari kuhusu tukio lililonikumba hivi karibuni kupitia jukwaa hili. Niliingia mawasiliano na mmoja wa wanachama humu ambaye aliniahidi kutuma game pamoja na simu Tulizungumza kwa muda, akanivuta kwa uaminifu na hatimaye nikatuma kiasi cha pesa shilingi laki tatu sitini.

Baada ya hapo – mawasiliano yakakatika. Hajawahi kujibu tena, na kila dalili zinaonesha kuwa ilikuwa ni njama ya kitapeli.

Ninachotaka kufikisha hapa ni tahadhari kwa wanajamii wengine:
  • Jihadharini kabla ya kutuma fedha kwa mtu yeyote mtandaoni.
  • Hakikisheni mna uthibitisho wa kutosha kuhusu mtu, huduma, au bidhaa kabla ya kufanya miamala.
  • Kama kuna wasiwasi wowote – ni bora kuuliza kwanza hapa JF au kufanya utafiti wa kina.
Nimesikitishwa sana kwa kuwa nilikuwa na imani kuwa JamiiForums ni jukwaa salama kwa mijadala na hata biashara, lakini tukio hili limenifungua macho. Natarajia uongozi wa JF wataendelea kuweka mazingira salama kwa wote.

Nawashukuru kwa kunisoma – na naomba ujumbe huu uwafikie wengi ili wengine wasije wakakumbwa na hali kama yangu.

View attachment 3357376View attachment 3357377
Kaka weka ID
 
umereta mrejesho,

Angalizo isijekuwa umejisafishia njia ya kututapeli😳

mnaotaka simu kwa jamaa kuweni makini, jamaa anaweza piga comeback 😳
 
Tapeli sio lazima awe hamfahamiani mzee. Jamaa yangu kapigwa zaidi ya laki nne na kidogo na member wa group la whatsap ambaye Kimsingi wanafahamiana vizuri tu
 
umereta mrejesho,

Angalizo isijekuwa umejisafishia njia ya kututapeli😳

mnaotaka simu kwa jamaa kuweni makini, jamaa anaweza piga comeback 😳
Kivipi sijajua una maanisha nini
 
Back
Top Bottom