MREJESHO: Uzoefu wangu wa kutapeliwa na member, jihadhari!

MREJESHO: Uzoefu wangu wa kutapeliwa na member, jihadhari!

Mtu kazi yake ni kubet ulishindwa kuangalia history yake?🤣🤣🤣
Screenshot_2025-06-06-19-02-23-03.png
 
Asante sana, wabaya watu
Kwenye ishu ya pesa umakini unahitajika n mkubwa sana, watu wanaitaka pesa yako kwa kila namna. Next time kuwa makini, wewe ndo ulisema upo mwanza unahitaji computer?
 
Natumai wote mko salama.

Napenda kushiriki kwa uchungu na tahadhari kuhusu tukio lililonikumba hivi karibuni kupitia jukwaa hili. Niliingia mawasiliano na mmoja wa wanachama humu ambaye aliniahidi kutuma game pamoja na simu Tulizungumza kwa muda, akanivuta kwa uaminifu na hatimaye nikatuma kiasi cha pesa shilingi laki tatu sitini.

Baada ya hapo – mawasiliano yakakatika. Hajawahi kujibu tena, na kila dalili zinaonesha kuwa ilikuwa ni njama ya kitapeli.

Ninachotaka kufikisha hapa ni tahadhari kwa wanajamii wengine:
  • Jihadharini kabla ya kutuma fedha kwa mtu yeyote mtandaoni.
  • Hakikisheni mna uthibitisho wa kutosha kuhusu mtu, huduma, au bidhaa kabla ya kufanya miamala.
  • Kama kuna wasiwasi wowote – ni bora kuuliza kwanza hapa JF au kufanya utafiti wa kina.
Nimesikitishwa sana kwa kuwa nilikuwa na imani kuwa JamiiForums ni jukwaa salama kwa mijadala na hata biashara, lakini tukio hili limenifungua macho. Natarajia uongozi wa JF wataendelea kuweka mazingira salama kwa wote.

Nawashukuru kwa kunisoma – na naomba ujumbe huu uwafikie wengi ili wengine wasije wakakumbwa na hali kama yangu.

View attachment 3357376View attachment 3357377
Bwege kweli wewe
 
Utapeli uliokuwa facebook, instagraam na Twitter sasa unahamia JF kwa kasi. Muwe mnaanika ID zao tuwahafamu ili tuwaepuke mapema.
 
Back
Top Bottom