Mrithi wa Samia ana kazi nzito kurudisha uchumi wa Tanzania kwenye Mstari

Wewe mpumbavu hujui misingi ya uchumi. Nenda uani kajisetiri halafu ukalale.

Uchumi kavuruga Magufuli, ila Rais Samia ndiyo anaujenga.
Anajengea kwenye makalio yako .watu wanaongea vitu sensitive ww unaketa porojo
 
Sioni kama Kuna ukweli maana kwenye gawio la Hisa tu pale CRDB mimi naona badiliko kubwa mno ni zaidi ya Mara nane ongezeko ukilinganisha na mwaka 2018.
Uchumi umewahi kuharibika ndio ila ni miaka ya nyuma kidogo
 
Hii nchi inavijana walioenda shule lakini ni wajinga sana wajinga mnooo. wanakuja na hallucination mbovu za kiuchumi zisizo na mantiki yoyote. wakati mleta thread ameandika simple na kueleweka mswano kabisa.
Hili li nchi litaendelea kuwa hivi hivi kwa sababu ya mavijana majinga
 
kufariki kwa rais ilikua mbaya. Ila wazalendo kuzidiwa na kuiachia nchi ilikua mbaya zaidi. Ni muhimu kurekebisha bila kulaumiana
 
21. Kumuua Membe
 
Unajua IMF na WB mission zao kwa Africa wewe tako??
 
mikopo mikbwa mikubwa huku nchi ikiwa Hoi bin taabani . Mfumuko wa bei uliopo Nchini Siyo wa kitoto, wakati huo huo purchasing power ya hela yetu ikiwa Chini Sana,. Pia serikali ikizalisha mikodi ya kila Aina kukandamiza mwananchi wa kawaida...
Mosi, una uelewa finyu wa mambo ya kiuchumi, na pili, ama hujui kilichokuwa kinaendelea wakati wa JPM au unajizimisha data tu!

Nikianza na uelewa finyu ni kwamba, mikopo mingi kama sio yote ambayo SSH anachukua ni kutoka World Bank, IMF, na Paris Club!

Hizo taasisi huwa zinatowa CONCESSIONALLY LOANS... meaning, ama inakuwa INTEREST FREE LOANS or a very small interest.

In contrary, kuonesha kwamba hujui nini kilikuwa kinaendelea wakati wa JPM, pitia hapa chini:-

JPM huyo kachukua Mkopo Credit Suisse... hiyo ni COMMERCIAL LOAN, na sidhani kama nahitaji kupoteza muda kufafanua hatari za commercial loans kwa nchi... hiyo ni 2018; but AGAIN...

In 2020 akachukua tena almost USD 1.5 BILLION na kwa mara nyingine ni COMMERCIAL LOAN!

Nikuwekee mikopo mingine ya kibiashara ambayo Magu alichukua halafu mnadanganyana eti alikuwa anatumia pesa za ndani?

Fanya utafiti wako mwenyewe uone ni kwanini SGR alipewa Mturuki na uone jinsi ambavyo gharama ya ujenzi ilivyokuwa imeongezwa maradufu... huo ndo utamu wa Commercial Loans kwa development Projects let alone corruptions ambayo hutawala huko!!
Hapa kuna elements za UDINI manake kuna Majuha wanaoaminisha Majuha wenzao kwamba:-
Majuha wenyewe ndo kama huyu!!

Nyerere aliacha nchi ikiwa HAINA HATA BIDHAA MUHIMU MADUKANI! Hata sabuni za kuogea zilikuwa zinatoka Kenya! Sukari ilikuwa inapatikana kwa mgao tena kwa kupanga foleni!

! Huko vijijini watu walikuwa wanafua kwa kutumia majani ya mpapaya!

Pamoja na yote hayo anatokea Mwehu anasema Mwinyi aliua uchumi!! Uchumi upi aliua Mwinyi wakati alikuta nchi almost defaul!

Anyway, pamoja na nchi kuiacha hoi lakini angalau Nyerere alijenga viwanda!! Nani alikuja kuuza mashirika ya umma tena kwa bei ya kutupa kama sio Ben Mkapa?! Au ndo kujenga uchumi huko?

Nani alikuja kuuza nyumba za serikali na matokeo yake kuifanya serikali iingie gharama ya kujenga nyumba zingine kama sio Mkapa?! Au Mkapa ni Mwislam?

Nani aliuza NBC hadi Nyerere akatoa mapovu? Nani alibinafsisha NMB na kudanganya hadharani eti benki ilikuwa inaiingizia serikali hasara hadi CEO wa NMB akatoka hadharani na kusema huo ni UONGO na kisha akarudi zake Marekani?

Huo ndo ujengaji wa uchumi wa hao uliowaita Wagalatia?!

Nani alitoa mkataba wa miaka 10 kwa TICTS lakini kabla haujaisha TICTS wakaongezewa miaka mingine 15? Nani alitoa Mkataba kwa IPTL lakini kabla haujaisha wakaongezewa mkataba mwingine?

Hayo yalifanywa na Rais Mwislam?

CHUKI ZENU ZA UDINI ndo zinawatia upofu!!

Turudi kwa JPM...

Ni nani mwenye akili timamu asiyefahamu jinsi ambavyo JPM alii-shake sekta binafsi?! Unajenga vipi uchumi huku ukii-shake sekta binafsi?

Wakati mkidanganyana eti JPM alikuwa anatumia pesa za ndani, ushahidi hapo juu unaonesha alikuwa anachukua MIKOPO YA KIBIASHARA tena kutoka kwa wale wale aliokuwa anawaita Mabeberu!

Hivi ni nani alinunua ndege ambazo hadi kesho wala hazina mwelekeo!

Unajenga vipi uchumi wakati hata kuajiri HUTAKI?!

Unajenga vipi uchumi wakati miradi ambayo ilitakiwa kufanywa na private sector inaenda kufanywa na JKT?
Wasiwasi wangu je tutakuja kupata mtu mzalendo ambae atakuja kuweka uchumi wetu imara, Tuombe iwe hivo kama hatapatikana basi Taifa la Tanzania linaenda kuangamia kama mrithi wa Samia atakuwa na akili hizihizi Tunazoshuhudia Sasa.....
Ni wakati sasa mumjibu FaizaFoxy swali lake kwamba "Hivi huko shule mnaenda kusomea ujinga"?
 
Huyu mama namuona wa hovyo kama Kikwete na Mwinyi. Ni rais ambaye ni ajali na zari kwa taifa. Tungefanya kila liwezekanalo asigombee uchaguzi ujao. She is weak and unpatriotic na mama misifa anayependa kusifiwa akijiita daktari wakati hata hiyo maste's anayosema anayo ilikuwa ni kukusanya hotuba za watu tena wakiwa kundi. Bonyeza hii link au weka
 
Umeliweka vizuri sana mkuu
 
Mapaka😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
SI Hilo TU mrithi atateseka kudeal na majizi.
 
Hap NO 19😭😭😭😭😭😭
 
Msingi wa uingozi wowote ni competency hayo mengine ni porojo tu
 
Haya ni maoni yako na unaruhusiwa kuwa nayo. Ukiuliza wafanyabiashara halisi watakwambia namna SSH anavyoufufua uchumi uliokufa kipindi cha awamu ya tano.

Nenda kaongee na wenye frames zao kula Masaki , Kinondoni na katikati ya jiji watakwambia ahueni wanayoipata kipindi hiki cha Samia kulinganisha na cha JPM.

Sijui ulikuwa na umri gani wakati wa Magufuli kiasi cha kupitwa na ule unyama aliokuwa anawafanyia wafanyabiashara wa kanda ya kaskazini mpaka wakafunga mashamba ya maua wakati soko likiwa bado lipo kule Uholanzi.

JPM pengine alikuwa na nia njema lakini kuonyesha ule utayari wa kuumiza baadhi ya watu na wakati huo huo akawa na utayari tena wa wazi wazi kabisa wa kuwabeba baadhi, ule ulikuwa ni ufa mkubwa sana wa uongozi wake.

Ukosefu wa hekima ya kuishi na watu haswa jamii ya wafanyabiashara. Hakuwa na kule kujali vilio vya wadau wake muhimu wa maendeleo pia akawa na ukosefu wa busara za kuongoza taifa la Tanzania.

Samia anao uwezo wa kusikiliza na hafanyi maamuzi bila ya kufanya utafiti wa kina juu ya faida na madhara ya maamuzi atakayofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…