HABARI.
Kwa upande wangu na mimi ningependa kutoa Ushauri kwa mtoa uzi. Kutokana na experience yangu niliopitia mtaani.
Kwanza kabisa ningependa kujua mtoa Uzi hiyo 20m ni ya kutoka wapi, yaani ni ya mkopo wa benki, akiba ambayo alikua amejiwekea ama vipi. Hii itasaidia kujua aina ya biashara pia ya kumshauri, maana unaweza ukamshauri biashara ya kuwekeza kisha baada ya miaka 10 ndo uone return kumbe hela ni ya mkopo kila mwezi anatakiwa kurudisha kiasi kadhaa. Kwa maana hiyo ningependa kutoa ushauri wa jumla ili kama kuna mtu mwingine anapenda mawazo na ana muda pia basi ajifunze
So mimi ningependa kushauri kutokana na mawazo mawili
1. Kama hela ni ya mkopo. Basi unahitaji biashara ya kuleta faida baada ya muda mfupi. Na tukifikia hapo sasa inshu ya stress free inakua hamna tena maana biashara za aina hii lazima ukutane na stress na ni LAZIMA WEWE UWE MWANGALIZI MKUU WA HIYO BIASHARA, maana biashara inaingiza hela kila siku kama umeweka mtu mwingine aisimamie lazima akupige.
Biashara zenyewe ni.
a) Kununua makinikia ya mgodini na kwenda kuuza kwenye Plant ama kwenda kuyachenjua mwenyewe na kupata dhahabu ya moja kwa moja. (Hii biashara inahitaji uwe mkoani na uwe mkoa wenye hiyo migodi) lasivyo kutakua hamna usimamizi wako na kumbuka nimesema bila usimamiz unapigwa. Huezi kukosa 3m kwa mzigo
b) Biashara ya Clasher (mashine ya kusagia mawe ya dhahabu)
Hapa kidogo kuna urahisi wa usimamizi japo sio sana, utahitaji kuzitembelea mara moja moja clasher zako, na hii biashara unachofanya ni kununua clasher 2 kwa jumla ya bei ya 8m mpaka 9m kwa Clasher na hapo utakua umetumia 16m au 18m kisha ukiweka kwenye mgodi unampa mtu anaehusika pale mgodi (wakiwa wawili ndio vizuri zaidi) awe ana operate/wana operate kisha wanakuletea hesabu kila mwezi, kiasi kinachozidi ni cha kwao hesabu huwa ni 800k kwa mwezi kwa Clasher 2 itakua 1.6m kwa mwezi ndani ya mwaka utakua umerudisha mtaji unaanza kusoma faida. (Hii hata mimi nafanya)
c)Biashara ya kuchimba madini ya Gemstones
Nenda Morogoro pale chimba madini hayo yapo mengi sana, na soko na return yake ni ya uhakika (Hii nina ndugu anafanya)
d) Biashara ya kununua vitu (nguo, viatu, vifaa vya simu na simu zake, urembo, mashine za kilimo na mashine za kawaida) kutoka China ama nchi za nje.
20m ni hela inayotosha kufunga mzigo wa kutosha kutoka china na ukaja kuuza bongo, kumbuka usimamizi inabidi uwepo wew mwenyew, utapeli unahusika hapa sana kama hautakua makini. Anza kwa kutengeneza masoko yako kkoo, buguruni, manzese, mbezi (hapa nime assume unakaa dar.) Kisha kafunge mzigo China uje uwasambazie (Hii kaka yangu anafanya)
e) Nunua mazao kwa wakulima kisha nenda kauze nchi za nje (mahindi/matunda/korosho/parachichi)
Hii biashara pia inahitaji muda wako sana na usimamizi wa hali ya juu. Kuanzia shambani unapoenda kununua mafekeche ya kiserikali mpaka masoko ya uko nje kwenyewe, ko muongozo mzuri unahitajika hapa.
ASANTENI SANA