Msaada: Biashara unayoweza kufanya kwa mtaji wa Tsh. Milioni 20

Faida hiyo na zaidi ukiamua kuwa unanunua tanzanite unakata unawauzia wenye maduka ya utalii kwa mil 25 kama ni mjuzi wa mawe 10 mil kwa mwezi unapata
Sawa, nisikubishie lakini kuna time nilikuwa na roll mitaa ya Goliondoi, Arusha. Nikakutana na ushauri wa biashara ya Tanzanite.

Kisha nikamshirikisha Babu yangu, akaniambia achana nao hao, afadhali umeniambia mapema.

Sidhani kama ni biashara anaweza kwenda fasta na kuielewa na kuanza kuifanya. Na akisema asaidiwe, anawez nasa kwa wapigaji.
 
Ndo maana nkaweka "kama unayajua mawe" Babako alitakiwa akupeleke ukasomee gemology mwaka .Kisha ukirudi uanze kuwa dalali miez 6 leo ungekuwa billionaire
 
Business idea and plan zinaanza hata kabla hujapata Hela ya mtaji kinyume na hapo all the best
Uzi ufungwe.
Hapa Niko natafuta mil 50 huku kichwani nishamaliza kila kitu, kwamba hizo mil 50 zinaenda wapi na zitafanya nini..!!!
Japo sijui pazukipatia..!!!

#YNWA
 
Aloo
Mkuu kwa 20m unapata eneo la 3m huko chaka unajenga kajumba kenye mapokezi na sero hakatamaliza 10m alafu unaajiri askari 2 unawalipa 300k kila mmoja mdogo mdogo unatafuta na vibaka wawili utarudisha hela yako ndani ya muda mfupi na ww unakua mkuu wa kituo unavimba mjini. Pesa yako itarudi na faida hadi utanikumbuka

HABARI.
Kwa upande wangu na mimi ningependa kutoa Ushauri kwa mtoa uzi. Kutokana na experience yangu niliopitia mtaani.

Kwanza kabisa ningependa kujua mtoa Uzi hiyo 20m ni ya kutoka wapi, yaani ni ya mkopo wa benki, akiba ambayo alikua amejiwekea ama vipi. Hii itasaidia kujua aina ya biashara pia ya kumshauri, maana unaweza ukamshauri biashara ya kuwekeza kisha baada ya miaka 10 ndo uone return kumbe hela ni ya mkopo kila mwezi anatakiwa kurudisha kiasi kadhaa. Kwa maana hiyo ningependa kutoa ushauri wa jumla ili kama kuna mtu mwingine anapenda mawazo na ana muda pia basi ajifunze

So mimi ningependa kushauri kutokana na mawazo mawili
1. Kama hela ni ya mkopo. Basi unahitaji biashara ya kuleta faida baada ya muda mfupi. Na tukifikia hapo sasa inshu ya stress free inakua hamna tena maana biashara za aina hii lazima ukutane na stress na ni LAZIMA WEWE UWE MWANGALIZI MKUU WA HIYO BIASHARA, maana biashara inaingiza hela kila siku kama umeweka mtu mwingine aisimamie lazima akupige.
Biashara zenyewe ni.

a) Kununua makinikia ya mgodini na kwenda kuuza kwenye Plant ama kwenda kuyachenjua mwenyewe na kupata dhahabu ya moja kwa moja. (Hii biashara inahitaji uwe mkoani na uwe mkoa wenye hiyo migodi) lasivyo kutakua hamna usimamizi wako na kumbuka nimesema bila usimamiz unapigwa. Huezi kukosa 3m kwa mzigo

b) Biashara ya Clasher (mashine ya kusagia mawe ya dhahabu)
Hapa kidogo kuna urahisi wa usimamizi japo sio sana, utahitaji kuzitembelea mara moja moja clasher zako, na hii biashara unachofanya ni kununua clasher 2 kwa jumla ya bei ya 8m mpaka 9m kwa Clasher na hapo utakua umetumia 16m au 18m kisha ukiweka kwenye mgodi unampa mtu anaehusika pale mgodi (wakiwa wawili ndio vizuri zaidi) awe ana operate/wana operate kisha wanakuletea hesabu kila mwezi, kiasi kinachozidi ni cha kwao hesabu huwa ni 800k kwa mwezi kwa Clasher 2 itakua 1.6m kwa mwezi ndani ya mwaka utakua umerudisha mtaji unaanza kusoma faida. (Hii hata mimi nafanya)

c)Biashara ya kuchimba madini ya Gemstones
Nenda Morogoro pale chimba madini hayo yapo mengi sana, na soko na return yake ni ya uhakika (Hii nina ndugu anafanya)

d) Biashara ya kununua vitu (nguo, viatu, vifaa vya simu na simu zake, urembo, mashine za kilimo na mashine za kawaida) kutoka China ama nchi za nje.
20m ni hela inayotosha kufunga mzigo wa kutosha kutoka china na ukaja kuuza bongo, kumbuka usimamizi inabidi uwepo wew mwenyew, utapeli unahusika hapa sana kama hautakua makini. Anza kwa kutengeneza masoko yako kkoo, buguruni, manzese, mbezi (hapa nime assume unakaa dar.) Kisha kafunge mzigo China uje uwasambazie (Hii kaka yangu anafanya)

e) Nunua mazao kwa wakulima kisha nenda kauze nchi za nje (mahindi/matunda/korosho/parachichi)
Hii biashara pia inahitaji muda wako sana na usimamizi wa hali ya juu. Kuanzia shambani unapoenda kununua mafekeche ya kiserikali mpaka masoko ya uko nje kwenyewe, ko muongozo mzuri unahitajika hapa.

f) Nunua viazi mviringo/mkaa/nyanya/mihogo/vitunguu njoo uuze Dar.
Kwa mtaji wako hapo kila badaa ya week utakua unaingiza gari 3 mpaka nne hivyo faida itakua juu sana. Ila muhimu uwepo wewe usiagize mtu.

g)Fungua duka la vipodozi
katika maduka yanayoongoza kwa kuingiza hela nzuri kama location ikiwa nzuri basi ni duka la vipodozi

h)Duka la pembejeo za kilimo/vifaa vya ujenzi/nguo n.k
Duka la aina yoyote halina mtaji maalum kwa kufungulia kwa hiyo 20m unafungua duka la aina yoyote ile

Kama hela si ya mkopo (Yaani haina marejesho)
kama hela haina marejesho ndio kwa umbali unaweza ukapata biashara ambazo uangalizi wake ni mdogo (kumbuka nimesema mdogo ila sio kama hamna uangalizi kabisa)
Biashara zenyewe ni

A. Lima shamba la miti
Hapa unaweza ukanunua shamba ukapanda mwenye au ukaenda iringa pale ukanunua shamba ambalo limeshapandwa kabisa na unakuta limebakiza miaka michache mpaka kuvuna ukasubiri hiyo miaka ukavuna. Hizi ni biashara ambazo uangalizi ni mdogo, unaweza ukawa unaenda shamba mara moja kwa miezi na sio kila mara.

B. Lima shamba la mazao ya miaka 3
Hapa namaanisha mazao kama Korosho za kisasa, embe za kisasa, michikichi ya kisasa, chungwa za kisasa, kokoa, n.k Haya ni mazao ambayo utaingia ghalama kwa miaka mitatu then baada ya hapo unaanza kula faida kila mwaka for the rest of your life mpaka wajukuu. Pia na usimamizi wake ni mdogo haikulazimu kwenda shamba kila siku bali unaweza ukawa unaenda mara moja kwa mwezi tuu. Sijajua wew ni mwenyeji wa wapi ila kama uko kwenu unaweza kupata mashamba ya 50k mpaka 100k kwa eka basi utakua na eka 100 mpaka 200 (ukitumia 10m kununua shamba na 10m kuhudumia shamba) mfano korosho unaweza ukaingiza zaidi ya 3m kwa eka mazao yakiwa na zaidi ya miaka 5 kwa eka 100 au 200 unaweza ukawa na 300m mpak 600m kwa mwaka (Hii mimi pia nafanya kwa zao la Korosho)

C. Nunua hisa za makampuni
Hapa unaweza ukachukua nusu hela ukaweza kwenye makampuni tofauti ila angalia tuu rudisho lao ni la muda gani, na fatilia storia ya kampuni ili isije ikafa na wew hujarudisha hela yako. Hizi ni biashara ambazo haziitaji wewe uwepo pale na zinachukua muda fulani mpaka uanze kuona faida. Na kumbuka research ni muhimu sana.

D. Nenda sehem ambayo viwanja ni bei rahisi nunua kiwanja kisha tengenezesha frem, kumbuka kama bei za viwanja itakua rahisi na frem zitakua za bei rahis as well so ukipata frem 10 ukapangisha kwa 30k mpak 50k hela yako itarudi na faida ya muda mrefu itakuepo.

E. Nunua mazao (mpunga/mahindi/mchele/ufuta/korosho)
Biashara ya mazao inalipa ila cha muhimu kwanza tafuta mtu mwenye uzoefu na hii biashara kwa sababu changamoto moja ya hii biashara inaweza kukata mtaji palefu kama sio kuuchukua wote. Ila inalipa sanaaaaaa.

F. Vuna miti ya mbao mkoani njoo uuze Dar.
Tafuta mtu anaefanya hii kitu akuelekeze inalipa sana.

E. Tengeneza laini ya uwakala mkuu (Super Agent)
Tengeneza ofisi, kisha nunua laini ya uwakala mkuu. Faida yake ni nzuri na ufanyaji kazi wake unaweza ukaufatilia kiurahisi hata kama haukuepo siku nzima/wiki nzima.

F. Fuga wanyama (nguruwe, kuku, bata, mbuzi, ng'ombe)
Hapa kuna maswala ya imani pia ko utajitathimin mwenyew uone ni mfugo gani unakufaa kuufuga.

KATIKA MAWAZO YOTE NILIOTOA YOTE NI MAZURI KWA SABABU KATIKA KILA WAZO KUNA MTU/WATU HUKU MTAANI WAMETOBOA KWA MAWAZO YOYOTE HAPO JUU. NA KUNA WENGINE WAMEFELI PIA KWA MAWAZO HAYO HAYO. HIVYO WAZO LINAWEZA KUA ZURI AU BAYA KUTOKANA NA WEW MCHUKUA WAZO UMENALIONAJE, MTAJI WAKO, IMANI, UFANYAJI KAZI WAKO, KUJITUMA KWAKO, VIJANA UNAOWATUMIA KUENDESHA BIASHARA, MAJILANI ZAKO, MKE/MME WAKO N.K KO CHA MUHIMU EM JITATHMINI WEWE ZAIDI KABLA HAUJAAMUA NI BIASHARA IPI UTAIFANYA. A

ASANTENI SANA.
Shukrani kaka kwa mawazo yako, yote nayaona mawazo bora hata kwa ambae anataka kufanya biashara ila chakuongezea ni kuwa biashara zote zonahitaji muda ni muhimu kwa biashara ambayo utaichagua ukaipa muda wakutosha ili kuona matokea bora
 
Faida hiyo na zaidi ukiamua kuwa unanunua tanzanite unakata unawauzia wenye maduka ya utalii kwa mil 25 kama ni mjuzi wa mawe 10 mil kwa mwezi unapata
Biashara ya mawe haiko straight foward namna hiyo. 1. Kwanza hakuna uhakika wa kupata mawe kila wakati. 2. Ukipata hakuna uhakika wa kuwa na thamani unayotegemea 3. Plus risks nyingine nyingi sana ambazo mpaka uwe kwenye field ndiyo utazijua.
 
Mm nko field mkuu.kinacholipa kwenye mawe sio kuvizia misimu .ni kuongeza thaman
 
Hakuna BIASHARA ambayo ni stress free labda ununue bond za serikali
Yani mtu anasemaje biashara halafu stress free?
Biashara na stress ni mapacha huwezi kuwatenganisha.

Hata hizo Bondi za serikali kipindi cha jiwe kuna watu walifilisiwa. Watu wanakuja wanakuuliza una bond milioni 300 umetoa wapi pesa, umefanya biashara gani, unalipa kodi Tsh ngapi
Pesa inakwenda.
 
HABARI.
Kwa upande wangu na mimi ningependa kutoa Ushauri kwa mtoa uzi. Kutokana na experience yangu niliopitia mtaani.

Kwanza kabisa ningependa kujua mtoa Uzi hiyo 20m ni ya kutoka wapi, yaani ni ya mkopo wa benki, akiba ambayo alikua amejiwekea ama vipi. Hii itasaidia kujua aina ya biashara pia ya kumshauri, maana unaweza ukamshauri biashara ya kuwekeza kisha baada ya miaka 10 ndo uone return kumbe hela ni ya mkopo kila mwezi anatakiwa kurudisha kiasi kadhaa. Kwa maana hiyo ningependa kutoa ushauri wa jumla ili kama kuna mtu mwingine anapenda mawazo na ana muda pia basi ajifunze

So mimi ningependa kushauri kutokana na mawazo mawili
1. Kama hela ni ya mkopo. Basi unahitaji biashara ya kuleta faida baada ya muda mfupi. Na tukifikia hapo sasa inshu ya stress free inakua hamna tena maana biashara za aina hii lazima ukutane na stress na ni LAZIMA WEWE UWE MWANGALIZI MKUU WA HIYO BIASHARA, maana biashara inaingiza hela kila siku kama umeweka mtu mwingine aisimamie lazima akupige.
Biashara zenyewe ni.

a) Kununua makinikia ya mgodini na kwenda kuuza kwenye Plant ama kwenda kuyachenjua mwenyewe na kupata dhahabu ya moja kwa moja. (Hii biashara inahitaji uwe mkoani na uwe mkoa wenye hiyo migodi) lasivyo kutakua hamna usimamizi wako na kumbuka nimesema bila usimamiz unapigwa. Huezi kukosa 3m kwa mzigo

b) Biashara ya Clasher (mashine ya kusagia mawe ya dhahabu)
Hapa kidogo kuna urahisi wa usimamizi japo sio sana, utahitaji kuzitembelea mara moja moja clasher zako, na hii biashara unachofanya ni kununua clasher 2 kwa jumla ya bei ya 8m mpaka 9m kwa Clasher na hapo utakua umetumia 16m au 18m kisha ukiweka kwenye mgodi unampa mtu anaehusika pale mgodi (wakiwa wawili ndio vizuri zaidi) awe ana operate/wana operate kisha wanakuletea hesabu kila mwezi, kiasi kinachozidi ni cha kwao hesabu huwa ni 800k kwa mwezi kwa Clasher 2 itakua 1.6m kwa mwezi ndani ya mwaka utakua umerudisha mtaji unaanza kusoma faida. (Hii hata mimi nafanya)

c)Biashara ya kuchimba madini ya Gemstones
Nenda Morogoro pale chimba madini hayo yapo mengi sana, na soko na return yake ni ya uhakika (Hii nina ndugu anafanya)

d) Biashara ya kununua vitu (nguo, viatu, vifaa vya simu na simu zake, urembo, mashine za kilimo na mashine za kawaida) kutoka China ama nchi za nje.
20m ni hela inayotosha kufunga mzigo wa kutosha kutoka china na ukaja kuuza bongo, kumbuka usimamizi inabidi uwepo wew mwenyew, utapeli unahusika hapa sana kama hautakua makini. Anza kwa kutengeneza masoko yako kkoo, buguruni, manzese, mbezi (hapa nime assume unakaa dar.) Kisha kafunge mzigo China uje uwasambazie (Hii kaka yangu anafanya)

e) Nunua mazao kwa wakulima kisha nenda kauze nchi za nje (mahindi/matunda/korosho/parachichi)
Hii biashara pia inahitaji muda wako sana na usimamizi wa hali ya juu. Kuanzia shambani unapoenda kununua mafekeche ya kiserikali mpaka masoko ya uko nje kwenyewe, ko muongozo mzuri unahitajika hapa.

f) Nunua viazi mviringo/mkaa/nyanya/mihogo/vitunguu njoo uuze Dar.
Kwa mtaji wako hapo kila badaa ya week utakua unaingiza gari 3 mpaka nne hivyo faida itakua juu sana. Ila muhimu uwepo wewe usiagize mtu.

g)Fungua duka la vipodozi
katika maduka yanayoongoza kwa kuingiza hela nzuri kama location ikiwa nzuri basi ni duka la vipodozi

h)Duka la pembejeo za kilimo/vifaa vya ujenzi/nguo n.k
Duka la aina yoyote halina mtaji maalum kwa kufungulia kwa hiyo 20m unafungua duka la aina yoyote ile

Kama hela si ya mkopo (Yaani haina marejesho)
kama hela haina marejesho ndio kwa umbali unaweza ukapata biashara ambazo uangalizi wake ni mdogo (kumbuka nimesema mdogo ila sio kama hamna uangalizi kabisa)
Biashara zenyewe ni

A. Lima shamba la miti
Hapa unaweza ukanunua shamba ukapanda mwenye au ukaenda iringa pale ukanunua shamba ambalo limeshapandwa kabisa na unakuta limebakiza miaka michache mpaka kuvuna ukasubiri hiyo miaka ukavuna. Hizi ni biashara ambazo uangalizi ni mdogo, unaweza ukawa unaenda shamba mara moja kwa miezi na sio kila mara.

B. Lima shamba la mazao ya miaka 3
Hapa namaanisha mazao kama Korosho za kisasa, embe za kisasa, michikichi ya kisasa, chungwa za kisasa, kokoa, n.k Haya ni mazao ambayo utaingia ghalama kwa miaka mitatu then baada ya hapo unaanza kula faida kila mwaka for the rest of your life mpaka wajukuu. Pia na usimamizi wake ni mdogo haikulazimu kwenda shamba kila siku bali unaweza ukawa unaenda mara moja kwa mwezi tuu. Sijajua wew ni mwenyeji wa wapi ila kama uko kwenu unaweza kupata mashamba ya 50k mpaka 100k kwa eka basi utakua na eka 100 mpaka 200 (ukitumia 10m kununua shamba na 10m kuhudumia shamba) mfano korosho unaweza ukaingiza zaidi ya 3m kwa eka mazao yakiwa na zaidi ya miaka 5 kwa eka 100 au 200 unaweza ukawa na 300m mpak 600m kwa mwaka (Hii mimi pia nafanya kwa zao la Korosho)

C. Nunua hisa za makampuni
Hapa unaweza ukachukua nusu hela ukaweza kwenye makampuni tofauti ila angalia tuu rudisho lao ni la muda gani, na fatilia storia ya kampuni ili isije ikafa na wew hujarudisha hela yako. Hizi ni biashara ambazo haziitaji wewe uwepo pale na zinachukua muda fulani mpaka uanze kuona faida. Na kumbuka research ni muhimu sana.

D. Nenda sehem ambayo viwanja ni bei rahisi nunua kiwanja kisha tengenezesha frem, kumbuka kama bei za viwanja itakua rahisi na frem zitakua za bei rahis as well so ukipata frem 10 ukapangisha kwa 30k mpak 50k hela yako itarudi na faida ya muda mrefu itakuepo.

E. Nunua mazao (mpunga/mahindi/mchele/ufuta/korosho)
Biashara ya mazao inalipa ila cha muhimu kwanza tafuta mtu mwenye uzoefu na hii biashara kwa sababu changamoto moja ya hii biashara inaweza kukata mtaji palefu kama sio kuuchukua wote. Ila inalipa sanaaaaaa.

F. Vuna miti ya mbao mkoani njoo uuze Dar.
Tafuta mtu anaefanya hii kitu akuelekeze inalipa sana.

E. Tengeneza laini ya uwakala mkuu (Super Agent)
Tengeneza ofisi, kisha nunua laini ya uwakala mkuu. Faida yake ni nzuri na ufanyaji kazi wake unaweza ukaufatilia kiurahisi hata kama haukuepo siku nzima/wiki nzima.

F. Fuga wanyama (nguruwe, kuku, bata, mbuzi, ng'ombe)
Hapa kuna maswala ya imani pia ko utajitathimin mwenyew uone ni mfugo gani unakufaa kuufuga.

KATIKA MAWAZO YOTE NILIOTOA YOTE NI MAZURI KWA SABABU KATIKA KILA WAZO KUNA MTU/WATU HUKU MTAANI WAMETOBOA KWA MAWAZO YOYOTE HAPO JUU. NA KUNA WENGINE WAMEFELI PIA KWA MAWAZO HAYO HAYO. HIVYO WAZO LINAWEZA KUA ZURI AU BAYA KUTOKANA NA WEW MCHUKUA WAZO UMENALIONAJE, MTAJI WAKO, IMANI, UFANYAJI KAZI WAKO, KUJITUMA KWAKO, VIJANA UNAOWATUMIA KUENDESHA BIASHARA, MAJILANI ZAKO, MKE/MME WAKO N.K KO CHA MUHIMU EM JITATHMINI WEWE ZAIDI KABLA HAUJAAMUA NI BIASHARA IPI UTAIFANYA. A

ASANTENI SANA.
Ubarikiwe Mkuu pamoja na wote walionipa ideas nawashukuruni sana
 
Napendelea ile biashara ambayo ni stress free, na ambayo inaweza kusimama vizuri bila direct involvement kwenye biashara.
Hakuna biashara ambayo ni stress free. Waswahili husemaa "Biashara mtu mwenyewe".
 
Good evening wadau,

Naombeni mawazo yenu na experience ni biashara gani au investment ambayo nitaweza kufanya Kwa mtaji wa Tsh. Milioni 20.

Napendelea ile biashara ambayo ni stress free, na ambayo inaweza kusimama vizuri bila direct involvement kwenye biashara.
Lengo langu hasa la kufingua huu uzi ni kuangalia aina tofauti za biashara just incase i want to jump in I would know some clues and all that, ila uliposema “inayoweza kusimama vizuri bila direct involvement” , I was like , nope let me start with that, homie business doesn't run like that, You have to be involved 100%, i mean all in. You have to look for a way to be involved I mean thaaaat involved regardless you being full time employed. Business is no joke my brother, BUSINESS IS WAR and you got to be THE INFANTRY, lo entiendes ?
 
Back
Top Bottom