Msaada: Biashara unayoweza kufanya kwa mtaji wa Tsh. Milioni 20

Au awe anabeti. Anatengeneza mkeka wa kesho Leo usiku, asubuhi anaingia kazini. Jioni anasubiri maokoto huku akiandaa mkeka mwingine.
Ila nyie madogo janja daah sasa acheze kamari tena daah πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, na mtu anataka kufanya investment inayoonekana ?
 
Lakini kumbuka hela za haraka, hupotea haraka pia. Mimi niliweka 25m miaka mitatu imepita saivi inasoma 34+ sio haba
Kwa miezi 36 umeingiza mil 9

Hii ni wastani wa sh laki mbili na nusu kwa mwezi.
Ukiwekeza mil hizo 25 kwa kuingiza 250k kila mwezi ni waste. Ila kama umehifadhi tuu huku ukiendelea kutafuta hela kwa namna ulivuoingiza hiyo mil 25, that's something
 
Una kitu utafika mbali
 
Kwakisema ni rahisi sana ….. haya tupe na changamoto zake
 
Kipindi unawaza ufanye nini kata million 2 kwenye hiyo kibunda anza kupaisha kindege aka aviator weka dau la ten ten na usiwe na tamaa kikipaa kwanzia odd 2 chukua mpaka linazama utakuwa hukosi laki kila siku
 
Una experience nayo? Ili uniambie zaidi
Unatafuta laini za uwakala mitandao pendwa pamoja uwakala wa bank pendwa

Unajenga vizuri madirisha yako Ili kusiwe na direct contact kati ya wahudumu na wateja

Kama inawezekana jengea nondo Kwa ndani ya ofisi yako Ili pesa na simu zote ziwe zinalala humo humo

Wewe ukienda kukagua unaangalia cash ipo shilingi ngapi na masalio yapo shilingi ngapi unajumlisha yote unapata jumla ya mtaji wako
 
πŸ˜„ 🀣 πŸ˜‚
Dah,
Kwamba kuna biashara ya SERO za binafsi?!!!
Unakuwa wakala wa Polisi, au?
 
Unadhani Kila mtu ana muda, mazingira sawa na wewe. Mtu kaajiriwa ndichi huko na bado kazini anatoka saa 11 jioni. Ila ndo hivyo anayo hiyo 20m , aiweke chini ya godoro?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kuliko kuweka chini ya Godoro bora afungue account UTT
 
 
Mkuu Mbogo_beichee , stay blessed kwa mchango wako mzuri sana.

Hizo ideas 1 (d) & (e) nina mpango nazo hivi karibuni early next year, moja wapo:

(d) Kufuata mzigo China na kuja kuuza kwa Jumla/wholesale hapa Tz.

Hapa bado naendelea kufanya utafiti ni bidhaa gani inayotoka chap chap pasipo usumbufu wa kuiuza. Hata kama Faida ni kidogo lakini iwe yenye mzunguko mkubwa.

(e) Kununua mazao ya nafaka (specifically nalenga mchele) na kupeleka kuuza nje ya nchi.

Hapa pia bado naendelea kujifunza by desk research ili kufahamu yote ya msingi ikiwemo changamoto zake na mengineyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…