MSAADA: Mtoto amefaulu Sekondari ya AHMES, lakini shule aliyomaliza darasa la saba imefutiwa matokeo

Sahihi kabisa
 
ubaya hamjui mambo yamebadilika na siku hizi hiyo ya kuvushwa toka la sita kwenda form 1 haipo tena yani... so labda mtoto aanze form one ila atarudia kufanya mtihani wa darasa la saba
Siku hizi unazoengelea ni zipi? Na zamani unayoiongelea ni ipi? Je muongozo wa elimu unaeleza kuhusu kurudia mtihani wa la saba? Ninajua mtihani wa maarifa kwa maana ya QT na kuendelea.
 
Watoto hawawezi kuwa victims kwa makosa ya wenye shule/vituo. Wataandaliwa mtihani special waufanyie kwenye centers zitakazotolewa na Baraza kabla ya shule kuanzia 2023, mara nyingi huwa ni shule za msingi za serikali. Ilitokea hii yapata miaka 4 nyuma waliokumbwa mmoja wapi ni Atlas na Maktaba za Dar es Salaam. Matokeo ya darasa la 7 huwa yanahitajika kwa usajili wa mitihani huko mbeleni.
 
Umejibu kinecta necta asante mkuu.
 
Umejibu kinecta necta asante mkuu.
Mimi bado sijaelewa matokeo ya la saba yanhitajika kwa ajili ya mitihani ipi mkuu? Make mimi kijana wangu kasoma mpaka la sita akafanya mtihani wa kujiunga kidato cha kwanza shule ya binafsi na leo yuko chuo mwaka wa pili, labda kwenye kazi za serikali huko ndo niliwahi kuona tangazo. Ambapo ilitakiwa kuwa na cheti cha darasa la saba. Tofauti na hapo sioni cheti cha la saba kinafanya nini kwenye taaluma.
 
Anaenda vzuri ndugu form one akuna sheria inayomzuia sio lazima mim ninandugu zangu awaijui darasa la 7 kabisa walikua wanarushwa madarasa kulingana na performance yao awajawai fanya mtihani wa darasa la saba now wapo wanapambana na module vyuon ukoo
 
Anaenda vzuri ndugu form one akuna sheria inayomzuia sio lazima mim ninandugu zangu awaijui darasa la 7 kabisa walikua wanarushwa madarasa kulingana na performance yao awajawai fanya mtihani wa darasa la saba now wapo wanapambana na module vyuon ukoo
Ilikuwa zamani, hivi sasa ni lazima awe na matokeo ya darasa la 7.
 
Chukua ushauri huuu

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua mimi sheria hipo form 4 tu ndo akuna mtahiniwa atakayefanya mtihani wa form4 pasi ya kuhufanya wa form tu basi hyo ya la saba kuwa pingamizi kwa mtoto kuenda form one hapana atoenda shule za serikali tu hila private anapiga mzigo tena kihalali tu sio illegal
 
Wala hakuna connection anaendelea Tu labda kama unataka apangiwe shule za serikali ndo arudie. Matokeo ya darasa la Saba KWA SASA HAKUNA YANAPOTUMIKA Almradi umemaliza
Mkurugenzi, una uhakika kweli na hiki ulichokisema hapa!!
 
Kuna Cheti cha Darasa la Saba zaidi ya Leaving Certificate ?

Nadhani ukijibu hili utakuwa umepata jibu..., Leaving Certificate ambayo kila mtu anapata hata kabla majibu hayajatoka ndio yanakutaarifu kwamba umesoma Primary
 
Mambo yamebadilika. Siku hizi watoto wote wanaomaliza elimu ya darasa la saba majina yao yanatakiwa kuonekana kwenye mfumo.

Kinyume na hapo, mtoto hawezi kupata usajili. Hata kama unampeleka private! Lazima jina lake lionekane kwenye huo mfumo.
 
Mambo yamebadilika. Siku hizi watoto wote wanaomaliza elimu ya darasa la saba majina yao yanatakiwa kuonekana kwenye mfumo.

Kinyume na hapo, mtoto hawezi kupata usajili. Hata kama unampeleka private! Lazima jina lake lionekane kwenye huo mfumo.
Nafikiri huu ndo ukweli.
 
Siku hizi hata mwanafunzi kurudia darasa lazima ukaombe kibali serikalini ili namba yake irekebishwe

Mambo yamebadilika
 
Mkuu hii sio sahihi
 
Dogo atapata nafasi ya kufanya mtihani kabla ya January au mwanzoni mwa mwezi.

Cha kufanya tulia subiri tangazo.

Zamani ilikuwa free tu. Sijui siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…