MSAADA: Mtoto amefaulu Sekondari ya AHMES, lakini shule aliyomaliza darasa la saba imefutiwa matokeo

MSAADA: Mtoto amefaulu Sekondari ya AHMES, lakini shule aliyomaliza darasa la saba imefutiwa matokeo

Dogo atapata nafasi ya kufanya mtihani kabla ya January au mwanzoni mwa mwezi.

Cha kufanya tulia subiri tangazo.

Zamani ilikuwa free tu. Sijui siku hizi.
Ebu kiongozi tusaidie kitu kimoja jaribu kupakia humu tangazo la nyuma linalotoa maelekezo ya kurudia mtiani wa darasa la saba uwenda nasi tukajua kitu hapa ambacho atukijui
 
Wakuu Msaada.

Kijana wangu amemaliza shule ya msingi iliyofutiwa matokeo. Kwenye interview zote nne nilizompeleka amefaulu. Matokeo ya la Saba yaliyotolewa nuda si mrefu shule yake imekubwa na tatizo Hilo.

Je, akiendelea na sekondari kwa matokeo yapi ya la Saba yatatumika? Kwa maana kwamba ana uhalali wa kuendelea na private?

Kwenye taarifa za Baraza la Mitihani atakuja atumie taarifa zipi huko mbeleni (hii watanielewa wale wanaojua utaratibu pekee kama hujui hapa pita tu)?

Dogo alipita interview zote zenye ushindani ikiwemo Ahmes sekondari.
Subiri mwongozo kutoka NECTA. Mtapewa tu majibu ya namna ya kufanya. Kama hao watoto wote watatakiwa kurudia mtihani, au la.

Maana ukiona matokeo yamefutwa kwa shule nzima, basi utambue fika kulikuwa na udanganyifu uliopitiliza. Jitahidi kufuatilia huko shuleni alikosoma mtoto wako, ili ujue kinachoendelea. Ila kiukweli kwa sasa hakuna njia ya mkato kama zamani.
 
Wakuu Msaada.

Kijana wangu amemaliza shule ya msingi iliyofutiwa matokeo. Kwenye interview zote nne nilizompeleka amefaulu. Matokeo ya la Saba yaliyotolewa nuda si mrefu shule yake imekubwa na tatizo Hilo.

Je, akiendelea na sekondari kwa matokeo yapi ya la Saba yatatumika? Kwa maana kwamba ana uhalali wa kuendelea na private?

Kwenye taarifa za Baraza la Mitihani atakuja atumie taarifa zipi huko mbeleni (hii watanielewa wale wanaojua utaratibu pekee kama hujui hapa pita tu)?

Dogo alipita interview zote zenye ushindani ikiwemo Ahmes sekondari.
... sifa muhimu ya kuingia sekondari whether private or government sio tu entry exam ya sekondari husika bali pia ni kuhitimu elimu ya msingi; na ushahidi wa kuhitimu elimu ya msingi ni cheti; na cheti ni matokeo. Kwa maelezo hayo mafupi kokotoa majibu ya swali lako.
 
Yaani kilichokukuta wewe ni kama kilichonikuta Mimi, Leo tu nimetoka kutumiwa joining instructions za mtoto, Cha ajabu baada ya matokeo naangalia darasa Zima wameandikiwa *W, nimechoka akili yote na hakuna kitu nisichokipenda kama mtoto kupoteza muda kwa kurudia mtihani tena darasa la Saba!!

Nadhani Serikali inatakiwa kupata njia ya kuwasaidia watoto,Ujinga wa wamiliki wa shule na waalimu wao so vyema kumuadhibu mtoto!

Adhabu kubwa itolewe kwa wamiliki wa shule lkn kwa Hawa watoto ni vyema hata wawape hata alama za chini kabisa kuliko kuwafutia au Basi wangewapa mitihani ya kurudia mapema ndani ya mwaka husika kuliko kusubiri mwaka mzima!!

Na kwa wale amabo wazazi wanaweza wapeleka Private ni vyema wakawaruhusu kuendelea na masomo ya Secondary kwa sharti la kurudia mtihani wa darasa la Saba!
 
Matokeo ya PSLE ni qualification ya mwanafunzi kufanya upimaji wa kidato cha pili FTNA, Hivyo lazima awe na matokeo. Hii imeanza mwaka 2019, usajili ulipoanza kufanywa mkondoni (online)
Watu wanachukulia kawaida sana
 
Fanya kitu kimoja, Tafuta shule yenye mfumo wa Cambridge ongea nao aonekane kafanya upper primary hapo then watampa matokeo ambayo baadae utayapeleka baraza la mitihani wakati wanamsajili kufanya mtihani wa kidato cha pili ili wafanye equivalence.
 
Usidanganywe, huwezi kufanya mtihani wa Form 2 kama hujafanya mtihani wa STD 7, hujafanya hii PLSE basi utokee mtaala wa Cambridge, IB au ufanye Edexcel ambayo baraza pia wanaitoa.
Pia kama hujafanya form 2 huwezi kufanya form 4 tena hiyo form 2 lazima ufaulu sio kufanya tu, kama ilivyo pia kwa form 6 huwezi kufanya mpaka uwe umepata credit pass 3 za form 4.
 
BMT wanajua namna ya kutatua hiyo changamoto, wala hatakiwi kurudia tena mtihani huo na atasajiliwa bila shida, na hili wanalifanya wenyewe BARAZA.
Fanya maandalizi ya kwenda kidato cha kwanza, akifika shuleni wakati wa usajili litajitokeza, shule husika watafanya mawasiliano na mzazi na BMT watamsajili kwenye mfumo.
 
Tuliwahi kufutiwa matokeo ya darasa la 7 mwaka 2006. Yule mama msimamizi nyoko sana, pale pale kwenye mtihani alituambia ninavyowaona hapa hakuna atakayetoboa.
Kwa sisi waliokuwa na uwezo waliendelea private, pangu pakavu tukarudia.
 
Ilikuwa ni enzi hizo, baada ya ndakichako kuwa waziri elimu amewabana warudiaji mf. Zamani mtu akimaliza form four anarudia form three siku hizi labda uwe private candidate au utumie jina la mtu aliekatisha masomo, kila form one private/ government lazima prem number (darasa la Saba), hakuna mkato
 
Wahuni wanachofanya, unaongea na Mw mkuu wa shule x, anakupa namba ya Mwanafunzi ambaye hakufaulu na wazazi hawawezi kumpeleka private,unatumia namba na jina lake (bila wao kujua) baadae unaenda mahakamani kuapa kubadili jina moja. Ila ni Mambo ya wahuni!!!!
 
Wala hakuna connection anaendelea Tu labda kama unataka apangiwe shule za serikali ndo arudie. Matokeo ya darasa la Saba KWA SASA HAKUNA YANAPOTUMIKA Almradi umemaliza
Akiendelea hatajuwa na PREMs namba hivyo hatasajiliwa popote pale kufanya FTNA akiwa kidato cha pili.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Wahuni wanachofanya, unaongea na Mw mkuu wa shule x, anakupa namba ya Mwanafunzi ambaye hakufaulu na wazazi hawawezi kumpeleka private,unatumia namba na jina lake (bila wao kujua) baadae unaenda mahakamani kuapa kubadili jina moja. Ila ni Mambo ya wahuni!!!!
Huo uhuni wa zamani sio rahisi kufanya kazi zama hizi ambazo usajili unafanyika mitandaoni. Usajili unatumia namba sio jina kama na yule mlieiba namba yake akeinda sekondari serikalini basi imekula kwenu maana namba Moja haiwezi sajili wanafunzi wawili.

Bado usajili wa kila mwanafunzi unapicha yake
 
Wakuu Msaada.

Kijana wangu amemaliza shule ya msingi iliyofutiwa matokeo. Kwenye interview zote nne nilizompeleka amefaulu. Matokeo ya la Saba yaliyotolewa nuda si mrefu shule yake imekubwa na tatizo Hilo.

Je, akiendelea na sekondari kwa matokeo yapi ya la Saba yatatumika? Kwa maana kwamba ana uhalali wa kuendelea na private?

Kwenye taarifa za Baraza la Mitihani atakuja atumie taarifa zipi huko mbeleni (hii watanielewa wale wanaojua utaratibu pekee kama hujui hapa pita tu)?

Dogo alipita interview zote zenye ushindani ikiwemo Ahmes sekondari.
Interview alizopita hazina maana kama amefutiwa matokeo darasa la saba. Itabidi arudie mtihani kama serikali itakavyoelekeza.
 
It is easy to seek advice kwenye hizo shule alizopasi. They know better
 
Mambo yamebadilika. Siku hizi watoto wote wanaomaliza elimu ya darasa la saba majina yao yanatakiwa kuonekana kwenye mfumo.

Kinyume na hapo, mtoto hawezi kupata usajili. Hata kama unampeleka private! Lazima jina lake lionekane kwenye huo mfumo.
Watu wajuaji humu, hawajui mambo yamebadilika, hata kumhamisha mtoto kutoka shule moja kwenda nyingine lazima awe na hiyo namba ya usajiri ya drs la 7. Ninachojua watoto waliofutiwa matokeo wataandaliwa mtihani mwingine watafanya before January ili kuwawezesha kwenda kidato cha kwanza
 
Ilikuwa ni enzi hizo, baada ya ndakichako kuwa waziri elimu amewabana warudiaji mf. Zamani mtu akimaliza form four anarudia form three siku hizi labda uwe private candidate au utumie jina la mtu aliekatisha masomo, kila form one private/ government lazima prem number (darasa la Saba), hakuna mkato
Ukichukua jina la mtu, hujui tayari una cheti cha kuzaliwa kina picha yako?
 
Back
Top Bottom