Lucas philipo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2017
- 2,039
- 2,676
Usimpotoshe mkuu!!Wala hakuna connection anaendelea Tu labda kama unataka apangiwe shule za serikali ndio arudie. Matokeo ya darasa la Saba KWA SASA HAKUNA YANAPOTUMIKA Almradi umemaliza
Hawezi kuendelea na masomo ya sekondari kama hajahitimu drs la 7. Ili apate usajili na kutambulika kama bonafide student atakayehitimu form four wanahitaji vitu vifuatavyo!
1. Awe amefanya mtihani wa upimaji kidato Cha pili yaani FTNA. Na hawezi kufanya mtihani huo kama huna PreMS number na hii inatolewa kwa waliomaliza Drs la saba yaani shule ya msingi, of which yeye hasomeki kama mhitimu.
2. Usajili kwa Sasa ni tofauti na zamani. Hata joining instruction ya shule aliyochaguliwa lazima kuna sehemu imemwambia ajaze PreMS namba ya shule ya msingi ndo automatically jina litatokea na atapata verification number ili waweze kum-enroll.
3.Details nyingi Sana za kidato Cha nne zinatokana na taarifa za mwanafunzi shule ya msingi na mitihani wa upimaji kidato Cha pili(form two wanategemea shule ya msingi). Ndiyo maana ukiingiza hizo number analetewa majina yake Kama alivyojiandikisha shule ya msingi.