MSAADA: Mtoto amefaulu Sekondari ya AHMES, lakini shule aliyomaliza darasa la saba imefutiwa matokeo

Wala hakuna connection anaendelea Tu labda kama unataka apangiwe shule za serikali ndio arudie. Matokeo ya darasa la Saba KWA SASA HAKUNA YANAPOTUMIKA Almradi umemaliza
Usimpotoshe mkuu!!

Hawezi kuendelea na masomo ya sekondari kama hajahitimu drs la 7. Ili apate usajili na kutambulika kama bonafide student atakayehitimu form four wanahitaji vitu vifuatavyo!

1. Awe amefanya mtihani wa upimaji kidato Cha pili yaani FTNA. Na hawezi kufanya mtihani huo kama huna PreMS number na hii inatolewa kwa waliomaliza Drs la saba yaani shule ya msingi, of which yeye hasomeki kama mhitimu.

2. Usajili kwa Sasa ni tofauti na zamani. Hata joining instruction ya shule aliyochaguliwa lazima kuna sehemu imemwambia ajaze PreMS namba ya shule ya msingi ndo automatically jina litatokea na atapata verification number ili waweze kum-enroll.

3.Details nyingi Sana za kidato Cha nne zinatokana na taarifa za mwanafunzi shule ya msingi na mitihani wa upimaji kidato Cha pili(form two wanategemea shule ya msingi). Ndiyo maana ukiingiza hizo number analetewa majina yake Kama alivyojiandikisha shule ya msingi.
 
Hawa wasikukatishe tamaa. Mwanao anaendelea kama kawaida. Wengine walimaliza darasa la sita wakaenda form one nani aliwadai matokeo?

Huko sio kala form four na six kwenye complications
Mkuu kuna kitu kinaitwa PreMS number.. usimpotoshe kabisa hatasajiliwa!
 
Mkuu mambo yamebadilika
 
Anaenda vzuri ndugu form one akuna sheria inayomzuia sio lazima mim ninandugu zangu awaijui darasa la 7 kabisa walikua wanarushwa madarasa kulingana na performance yao awajawai fanya mtihani wa darasa la saba now wapo wanapambana na module vyuon ukoo
Ni zamani mkuu, kwa sasa utaratibu umebadilika
 
Means walianza form 1 na baadaye wakafanya Mtihani?
 
Sasa Naomba kuuliza tena hiyo Prem Namba Mbona kwenye majina ya Watoto waliofutiwa inaonekana?
 
Mm ninavyoelewa elimu ya msingi ni utambulisho tu.Atachukua cheti cha kumaliza ambacho kitamtambulisha kuwa alimaliza shule ya msingi.Yeye aanze tu sekondari ya private hakuna shida.Wanaofaulu na kuendelea ni wale wanaokwenda shule za serikali.
 
Acha kuandika Hipo
 
Mambo yamebadilika. Siku hizi watoto wote wanaomaliza elimu ya darasa la saba majina yao yanatakiwa kuonekana kwenye mfumo.

Kinyume na hapo, mtoto hawezi kupata usajili. Hata kama unampeleka private! Lazima jina lake lionekane kwenye huo mfumo.
Wewe ndiyo mtu unayejua unachoandika.Siku hizi hata uhamisho kwa shule binafsi lazima ufanywe kuanzia kata hadi halimashauri.
 
majeshini kinatakiwa Cha darasa la 7
Wala hakuna connection anaendelea Tu labda kama unataka apangiwe shule za serikali ndio arudie. Matokeo ya darasa la Saba KWA SASA HAKUNA YANAPOTUMIKA Almradi umemaliza
 
Jumla ni watoto 2200+
Labda wanafanya hivyo ili shule ziepuke huo mchezo
 
Kumbuka hawa watoto wamefutiwa namba zao, kutokana na vituo vyao kudanganya, hivyo watapewa namba upya ambazo zitaonesha mwaka tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…