Msaada: Napataje mafao yangu ya NSSF kama sina Certificate of Service na Kampuni niliyokuwa nafanyia kazi imefungwa?

ma twins

New Member
Joined
Sep 7, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Habari wakuu,

Naomba msaada na ushauri kutoka kwa mtu mwenye uzoefu na NSSF au aliyewahi kupitia hali kama yangu.

Nilikuwa nimeajiriwa katika kampuni fulani na nilikuwa nachangiwa NSSF. Kwa sasa kampuni hiyo imefungwa, hivyo siwezi kupata Certificate of Service kutoka kwa mwajiri wangu.

Nimekuwa nikifuatilia suala la kupata mafao yangu NSSF, lakini nimekwama kutokana na kutokuwa na Certificate of Service.

Swali langu ni hili: Je, mtu anaweza kupata mafao yake ya NSSF bila Certificate of Service endapo kampuni aliyokuwa akifanyia kazi imefungwa?

Kama inawezekana, ni nyaraka gani nyingine zinaweza kutumika kuthibitisha kwamba nilikuwa nimeajiriwa na kampuni hiyo?

NSSF wana utaratibu gani kwa mtu ambaye mwajiri wake amefunga kampuni na hayupo tena?

Je, kuna mtu aliyewahi kupitia hali kama hii na akafanikiwa kupata mafao yake? Naomba mnishirikishe uzoefu wenu.

Kama NSSF watakataa kwa sababu sina Certificate of Service, ni hatua gani ninapaswa kuchukua?

Naomba ushauri kutoka kwa mtu mwenye uzoefu wa moja kwa moja na NSSF, hasa wale waliowahi kushughulikia madai ya mafao katika mazingira kama haya.

Asanteni sana.
 
Peleka mkataba kam uliisha
 
Back
Top Bottom