Msaada: Nataka kuuza nyumba maana baba yangu mzazi anadai mimi sio mtoto wake

Watu kama ninyi ndio mnao sababisha urusi iendelee kumchapa ukren, maana Putin hataki kabisa ujinga wa aina hii...[emoji3525]

Alafu 41 years old unajiita kijana..!!
Hivi nyie wanaume wa Daslam mkoje...[emoji53]
Hahaha mkuu nimechukua umri wake nikagundua huyu sio kijana ila ni mvulana

Kijana anahama nyumbn akifikisha miaka 15 kama hayupo shule akiwa shule akimaliza form six huwa harudi nyumbn tena anaanza kutokea kwa marafiki mwisho anapanga chumba

Sasa huyu mvulana anajiita kijana kuna walakini hapa

Mali za wazazi ni zao wewe mtoto unapewa kwa hisani tu
 
Miaka 41 unajiita kijana ? Aise hawa bongo don wapigwe marufuku
 
Siyo wote wenye mvi ni wenye hekima....!!
 
Halafu ifikie wakati uache kucheza na akili zetu.

Hii mada umeshawahi kuiweka humu jukwaani.
Hii kitu kweli kama niliwahi kuisoma zamani. Halafu jitu la miaka 41 linagimbea nyumba ya babake
 
Pole Sana, kinachokusumbua Ni malezi mabovu, yaelekea ulidekezwa na mama yako, baba anakwambia nenda shule, badala yake unazunguka kwa mama yako unaomba pesa ya kula shuleni, ikibaki unavuta bange, matokeo yake ndo hayo..
Kwanza,, ki kawaida Mali ya mzazi huwa sio tegemeo la mtoto, wew ulipaswa kuwa na mambo yako binafsi, Sana Sana, kwa vile baba bado yupo, ungekuwa unamshauri jinsi ya kuishi vzr ili adumu zaidi,
Kuwa karibu na mzazi akuone rafiki yake, Kia's kwamba hata akiamua kugawa vitu akufikirie Mara 2.. kumbuka, ktk familia Kuna urafiki pia, mnaweza kuzaliwa watoto 6 lakini ukapata rafiki mmoja, au ukakosa kabisa, ukaja kupata rafiki wa nje ya familia,
Nakushauri, tafuta vyako, usitafte kaana ya mzazi, uking'ang'ania atakuambia subirini nikifa urithi nilishaandika mtaenda kuchukua maelekezo mahakama flani,,
Utaona anachalewa kufa, unamuwekea sumu ili afe mapema,ile kwenda mahakani unakuta URITHI wako, kakuandikia KOPO la chooni na PANGA,
So keep watching..
 
Sio sawa kumchukua baba mahakamani kisa nyumba yake mwenyewe. Kuuza nyumba bila baba kujua unatafuta LAANA.
 
Miaka 41 unakaa kwenu?huyo mzee ni fala ingekua mimi ningekupa kesi ukakae magereza ndio kunakufaa mtu wa hovyo kma wewe
 
Wewe jamaa utakuwa na tatizo la akili, kwanini unakomaaa na Mali ya baba yako , ushakuja hapa ukapewa ushauri ajabu zaidi wewe ni graduater mbona u adharirisha uwanaume wako acha utoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…