Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Kwanza kabisa kabla hujaenda naomba kujua ulivyokutana na huyo mzee baba ulikua ukifanya kazi au alikukuta ukiwa huna moja wala 2 πŸ˜„ maana haki husimama kwa watu wote kama mmekorofiana kaeni chini muyajenge mulee wanenu
 
Kama hawezi kuwalea kwanini alazimishe kubaki nao?
Kama nitahitaji wanangu alafu ukawazuia bila sababu ya msingi, hakika utalea mwenyewe.

Tunasubiri tu hiyo fainali uzeeni ije vyovyote🀣
Uzee unatisha Mkuu, si uliona Baba yake Diamond alivyokuwa anaomba huruma ya Watanzania kuwa ametelekezwa na Mwanaye.

Na mbaya zaidi mtoto ambaye ulimtekeleza unakuta anafanikiwa maisha na wewe ndiyo unakuta hata ugali wa siku unashindwa kumudu kuupata.πŸ˜…
 
Yaàni ni maboss kwelikweli,mtu anapanga masharti Utasema yeye ndio mwenye hiyo nyumba,ukipika maharage anasema sitaki nataka nyama,ukipika nyama anasema nataka Chipsi,ukipika Chipsi anasema nataka samaki aaaaaah hakika hutu tuviumbe ni tusumbufu Sana....Nina kamoja hako kananimbiaga "mama,hii juice sijaipenda"yaàni hapo mie nimejipinda najua katafurahi ,naishia kuchokaa😁😁😁
 
Hii ni point kubwa kama siyo kuu. Lakini ieleweke kuna wanawake/mabinti ni zaidi ya shetani.
Ni vile wanaume wengi huwa hawazungumzi!
 
Sawa tu hayo ndio maisha. Lakini siwezi kukubali kupelekeshwa na mwanamke wakati huu kisa mtoto.

Yani nikupe maelekezo yanayohusu mtoto ukaidi alafu unategemea niendelee kukusapoti haiwezi kutokea.

Kwa sasa kila mtu ashinde mechi zake hata hivo kufa anaweza tangalia mtoto mwenyewe au mama.
 
Hayo ni malezi ya hovyo! Na hapo ndo umuhimu wa baba katika malezi unapokuja. Mtoto hawezi kukupangia nataka hiki, sitaki hiki.
Mnapokuwa na ka-uwezo kuwapa chakula,nguo na malazi mnadhani ndo kulea!
 
Piga pamba kali za kumtamanisha mwanaume yeyote, kisha muite mzazi mwenzio mmalize tofauti zenu. Hapo itakuwa 'case closed.'
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚nina talaka zangu zote 3 mkuu japo za matamshi
Talaka sio kitu, pigilia pamba shepu ionekane, akikuona apate kigugumizi, mambo yataenda sawa; sasa ukiwa unavaa kama mpika supu wa mnadani, ni nani atakuwa na hamu na wewe, lazima maisha uyaone magumu tu.
 
Haijalishi mnapitia sintofahamu gani na Mama mtoto, lakini swala la child support ni muhimu kutoa.

Mkishindwana kabisa, ni heri kumchukua mtoto na kumlea mwenyewe Baba, ingawa huwa ni risk sana iwapo utaoa Mwanamke asiyempenda huyo Mwanao, anaweza kumfanyia matendo mengi ya unyanyasaji ukiwa umeenda kazini
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Hesabu zako zinasema utapata ngapi,utapigwa kama hakimi , mi shahara tunakopea
 
Nadhani ni 50% na sio 40%.
 



Hapana,
Kwani kalenda ya uzazi Mungu kaiweka kwa nani kati ya Mwanaume na mwanamke?
Hivyo anayetakiwa kuchukua tahadhari Kwa kujijua zaidi ni nani ?

Ikitokea vinginevyo mhanga atakuwa nani?

Je huwa wanakubaliana kuzaa?
 
Naomba kukuuliza swali la kizushi. Hivi, huyu Mwanaume ulikutana nae mazingira gani??

Na mlipokutana ulikuwa na malengo gani au ulitegemea kuanzisha nae mahusiano ya namna gani?

Nauliza haya kwasababu nataka nifahamu mazingira gani mlianzia hadi leo muwe katika hali hii.

Nina wasi wasi huyu mwanaume ulianzisha nae mahusiano ili uweze kupata kutumia pesa zake. Uliona ana mshahara mkubwa ukajua ukizaa nae mtoto atakupa attention ya matumizi.

Kwa kifupi ninadhani huu ujauzito ni 90% your decision mwanaume haukumshirikisha hata kidogo. Wanaume wengi wasiolea vizuri watoto wao ukiwauliza mazingira ambayo wameletewa taarifa za ujauzito wengi watakwambia hawaelewi hata imekuwaje mabinti walijiachia hadi ujauzito ukaingia bila kuwashirikisha.

Wengi huwa wanastukia tu ujumbe "Nina ujauzito wako". Halafu kimachofuata hapo ni straight kuanza kutaka matumizi jambo ambalo wanaume huhisi ni mtego walitegewa kitambo sana.

Aiseee.
 
Vipi mtoto akiwa na maisha ya hovyo na baba yake akapata watoto sehemu nyingine akalea vizuri wakawa na mafanikio wakamsaidia. Hapo itakuwaje kwenye hii story yako?! [emoji23][emoji23][emoji23]
 

kakuta kazini nilikuwa nafanya tigopesa enzi izo kariakoo akanipenda akanitongoza akanioa nadhani nmejibu ipasavyo na watoto wamezaliwa ndan ya ndoa
 
Haya usitufokee sasa hiki ni kikao cha familia dada, kuna wazee hapa , wajomba, wapwa, mabinamu, hebu tafadhali tuliza hasira na jazba tumalize kikao salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…