Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Huyu Dejane asimsingizie mtoto, hizo tabia zote za mtoto ni zake. Mfundishe mtoto nini ale, asichague chakula uone kama atakusumbua. Kwangu hakuna chakula cha baba wala mtoto(kuna nyumba baba anapikiwa separate, kwangu ni upuuzi mtupu), wote tunakula lilichopikwa na watoto wanafurahia sana tu.
Kwa hiyo kanirith 😂😂😂
 
Kwa wanawake wenye akili wanahakikisha uhusiano wa bana na mwana unakuwa mzuri ili Mtoto azidi kubarikiwa haijalishi Hata kama bana hakumlea wala kumtunza.
Asilimia kubwa ya wanawake ugomvi wao wanamhusisha mtoto pia
 
Mahusiano yamekua changamoto sana nowdays..very unpredictable. Ifike mahali mwanamke aliyepevuka kimwili na kiakili anapoamua kua na mtoto ajiridhishe kwamba ataweza kupambana na malezi ya mwanae with or without support ya baba mtoto...vinginevyo ni kujinyanyasa kisaikolojia mwisho wa siku mama atachukia hadi mtoto.
Binafsi mwanamke asinizalie kama hatukukubaliana, haya mambo ya kushtukizwa eti nina mimba wakati nimekutana na mwanamke anayejielewa kabisa ni upumbavu mkubwa, nitampeleka kwa pilato akajibu hoja kwa nini abebe mimba bila makubaliano!
 
Ulizaa mtoto Kwa kuhitaji uwe na mtoto au kumrishidha huyo mwanaume?

Lea mwanao! Angekufa ungeenda kulishtaki kaburi?

Fanya kama hayupo, Lea bila huzuni, ona mwanao ni baraka kuu.

Sali na mtegemee Mungu, atakupa riziki ya mtoto wako.

Ukianza habari za ustawi wa jamii, utapauka Kwa stress, huo muda angalia shughuli ya kufanya.

Mwanaume wa kweli na mtu mzima, hakumbushwi kulea damu yake.

Pambana lea mwanao, achana nae.

Ushawahi ona jogoo analea vifaranga? Wanaume hawaleagi, its nature....atahudumia mtoto Kama na wewe unamuhudumia, Kama uko tayari kufata matumizi ya mtoto guest endelea kumsumbua, Kama unajali utu wako pambana mwenyewe.....mlezi mkuu ni Mungu, mtoto atakua tu bila yeye.

Angalizo, akileta matumizi usikatae na usimlishe mtoto sumu kumuhusu.
well said
 
Ni sahihi Mkuu, ila sio jambo zuri kutelekeza watoto wako bila kuwahudumia.

Hata kama huna hela basi ujitahidi hata kidogo kinachopatikana kuwatumia.

Kuna wakati tunaweza kujivunia Nguvu za Ujana tulizonazo lakini kuna wakati utawahitaji hao watoto japo wakusaidie kutoka Nje ya nyumba kwaajili ya kuota Jua na Jioni kukurudisha ndani wakati ukisubiri kufa.
Mtoto hana kosa
Hata sisi hatukuwa na kosa, ila dhambi ya Adam na Hawa ndo imesababisha dunia nzima iibebe.
Vivo hivyo dhambi ya mama inaenda kwa mtoto kama mama ataamua kummiliki mtoto
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
 
Kama hutaki kuzaa na mwanamke unae furahishana nae tumia condom kwa wingi Sana acheni kuzalilisha wanawake watoto wakifankiwa mnaanza kujiliaza kutwa wengine mpaka mintandaoni kutaka huruma shit
Condom zipo unamtaka mwanamke njoo na Kinga zako uone Kama mwanamke atakataa kutumia Kinga na akikataa unamwacha kitandani unasepa zako sio lazima ushiriki nae tendo akikataa halafu sio sifa kukataa kulea mtoto maana mtoto hakwepo muda mnafanya starehe yenu mnaathiri Sana watoto kisaikojia kuweni makini kwenye starehe zenu.Ukipanda karanga utavuna karanga sio nju
 
Mpenzi achana na habari za kupelekana ustawi wa jamii, 50000 inatosha nini kwa maisha ya sasa hivi?? Ni mara mia ukamlea mwenyewe mtoto wako kama baba hana habari ya kulea mwanae hakuna haja ya kumlazimisha. Jishughulishe mwanamke mwenzangu umlee mwanao.

Mwanaume ambae halei damu yake ni MPUMBAVU kabisa, haijalishi mna situation gani na mama yake mtoto hahusiki kabisa wewe lea mwanao. Unakuta mwanaume anakambia mm nitatoa ada tuu ambayo ni 800k kwa mwaka means kwa mwezi ni kama anatoa 67,000 sasa si bora akae na hela zake tuu ni dharau sana hiyo.
Nyie kina baba leeni watoto wenu bila kushinikizwa
Hatulei kama wamama mmeamua kuwapa sumu.

Narudia hatulei na hakuna litalotokea
 
Sii jogoo tu hata simba dume halei watoto ni jukumu la simba jike! Hivi unajua hata simba jike akipata joto anataka dume bsasi kuwinda swala safi na kuohonga simba dume ili apate nguvu za kutosha kumshughulikia jike vizuri? Hata zamani mwanamme alikuwa anaoa wake watatu yeye anajenga tu nyumba na halafu wanawake wanalima chakula chao wenyewe na kuzaa watoto! Hii ndo asili! Sasa huyo baba hata ukumpeleka ustawi kama ana watoto wengine 10 unafikiria wewe utaambulia nini? Komaa tu tafuta riziki!
 
Naungana na wewe hapa
Hao viumbe ni pasua kichwa sana, kuna mmoja alimbana mshikaji kwamba amezaa mtoto wake na jamaa anaye mke tayari, basi jamaa akamwambia ili mambo yaende sawa waende ustawi wa jamaa ili wakaandikiwe vipimo vya DNA ili ifahamike kisheria kwamba huyo mtoto ni wake, mwanamke hataki anang'ang'ana tu apewe pesa za matumizi. Yaani ilikuwa mtifuano mkubwa hadi leo huyo mwanamke hajafuata utaratibu na jamaa kapotezea.

Halafu mwanamke kama huyo akianza kulalamika utafikiri kaonewa, kumbe yeye mwenyewe ndo kajifanya kichwa maji.​
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Pole classmate kwa haya unayopitia
 
Huyu mwanamke ana tamaa na pesa KUTOKANA na Hali ngumu ya maisha
 
Back
Top Bottom