Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Mpenzi achana na habari za kupelekana ustawi wa jamii, 50000 inatosha nini kwa maisha ya sasa hivi?? Ni mara mia ukamlea mwenyewe mtoto wako kama baba hana habari ya kulea mwanae hakuna haja ya kumlazimisha. Jishughulishe mwanamke mwenzangu umlee mwanao.

Mwanaume ambae halei damu yake ni MPUMBAVU kabisa, haijalishi mna situation gani na mama yake mtoto hahusiki kabisa wewe lea mwanao. Unakuta mwanaume anakambia mm nitatoa ada tuu ambayo ni 800k kwa mwaka means kwa mwezi ni kama anatoa 67,000 sasa si bora akae na hela zake tuu ni dharau sana hiyo.
Nyie kina baba leeni watoto wenu bila kushinikizwa
 
Umemzoesha hivyo, makosa ni yako. Watoto wana tabia moja in common, wanabeba kile unachowafundisha. Huenda wewe ndio unapenda choma na kaanga.
Mtoto hapaswi chagua chochote maana hajui kesho itakuwaje na hana uwezo wa kutafuta.
Mi kitachopikwa atakula hivyo hivyo.

Huwa anajifanya kutaka tapika namwambia ukitapika utakula matapishi, akisikia hivyo anakula anamaliza ananionesha Baba ona nimemaliza
 
Halaf wapo hivi mwanamke kama humpi uchi baba mtoto hatoi matumizi Yaan akili za hawa watu sijui zipoje na unakuta kaoa yeye ila mda anaotaka apewe madikteta kweli
Sio wote mi sinaga time na nyuchi, ila ukizingua hata mia hupewi
 
Pambana lea mwanao, achana nae.

Ushawahi ona jogoo analea vifaranga? Wanaume hawaleagi, its nature....atahudumia mtoto Kama na wewe unamuhudumia, Kama uko tayari kufata matumizi ya mtoto guest endelea kumsumbua, Kama unajali utu wako pambana mwenyewe.....mlezi mkuu ni Mungu, mtoto atakua tu bila yeye.

Angalizo, akileta matumizi usikatae na usimlishe mtoto sumu kumuhusu.

Kwa huo ujasiri ulioutapika hapo[emoji122][emoji122]inatosha ujengewe sanamu kwenye makao ya ustawi[emoji28]
 
Tatizo hapo sio malezi ya mtoto ni iyo 2.8 million. Kwamba anakula pekeyake kweli? Hv angekua kafaliki baba yake n uyo mtoto. Ni 100% uyo mme wa mtu.Dawa zimeisha nguvu karudi nyumbani
 
Mahusiano yamekua changamoto sana nowdays..very unpredictable. Ifike mahali mwanamke aliyepevuka kimwili na kiakili anapoamua kua na mtoto ajiridhishe kwamba ataweza kupambana na malezi ya mwanae with or without support ya baba mtoto...vinginevyo ni kujinyanyasa kisaikolojia mwisho wa siku mama atachukia hadi mtoto.
 
Mtoto hapaswi chagua chochote maana hajui kesho itakuwaje na hana uwezo wa kutafuta.
Mi kitachopikwa atakula hivyo hivyo.

Huwa anajifanya kutaka tapika namwambia ukitapika utakula matapishi, akisikia hivyo anakula anamaliza ananionesha Baba ona nimemaliza
Ni kweli lakin si unajua kuwa kuna vyakula mtoto wako anavipenda kwanin kila mara asipikiwe akala na ambavyo havipendi ale mara moja moja si mbaya
 
kwa nini mlitengana????,mimi mwenyewe hapa nilimpa wife mtaji aanze biashara samaki jumla na rejareaja,matokeo yake akaanza kiburi na dharau za hali ya juu{baada ya biashara kuchanganya},,,basi bana alipoona kama nammbana akabeba vitu kibao vya ndani,na duka akahamishia anapopajua yeye na yeye kwenda kupanga anapopajua,,,,mimi sikuhangaika nae,na wakati anabeba vitu mimi nilikuwa grocery ya jirani namwagilia moyo baada ya kutoka kwa job,,,,,nilimpigia nikamwambia beba kila ki2 niachie vitambulisho vya kazi na bank ukimaliza huo uchafu unaofanya nipigie simu nije kulala,,,,ninavoandika hapa duka kafunga{kafilisika},,anauza pombe kali za kupima na tigo pesa yenye mtaji wa ukubwa wa sisimizi,,,watoto wako boarding ila mdogo aliondoka nae...sasa akaanza kunisumbua niwe namtumia pesa za amalezi,nimegoma nahawezi kwenda popote manake aliondoka kijambazi na mtaji wa milioni 8 nilizokopa kazini,ameacha nymba tuliyojrnga na shamba la kama hekari mbili nakwenda kupanga!!!!!!!hiyo akili au matope......??? mrudie mumeo
Watu kama hao unawaacha ma ujeuri wao.
Tatizo la wanawake wakishapata kakipato wanajiona wanajiweza na kutaka panda watu vichwani
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Ila ilikuaje ukaamua kuzaa naye? Haya mambo sometime mnayataka wenyewe. Mtu hajaamua kuwa na mtoto unaona ujikamatishe mimba. Mwanaume huwa suala la kulea anajua ni lake na ukiona hataki hilo achana naye. Pambana wakati mnakatikiana viuno mlipaswa mjue hili nalo lipo. Mnaanza kusumbua watu wawalipe pesa za matunzo. Hao watoto msitumie kama kitega uchumi. Wewe angalia unapataje pesa fanya shughuli flani mtoto apate mahitaji yake. Achana na huyo mwanaume
 
Mtoto hapaswi chagua chochote maana hajui kesho itakuwaje na hana uwezo wa kutafuta.
Mi kitachopikwa atakula hivyo hivyo.

Huwa anajifanya kutaka tapika namwambia ukitapika utakula matapishi, akisikia hivyo anakula anamaliza ananionesha Baba ona nimemaliza
Huyu Dejane asimsingizie mtoto, hizo tabia zote za mtoto ni zake. Mfundishe mtoto nini ale, asichague chakula uone kama atakusumbua. Kwangu hakuna chakula cha baba wala mtoto(kuna nyumba baba anapikiwa separate, kwangu ni upuuzi mtupu), wote tunakula lilichopikwa na watoto wanafurahia sana tu.
 
Ni sahihi Mkuu, ila sio jambo zuri kutelekeza watoto wako bila kuwahudumia.

Hata kama huna hela basi ujitahidi hata kidogo kinachopatikana kuwatumia.

Kuna wakati tunaweza kujivunia Nguvu za Ujana tulizonazo lakini kuna wakati utawahitaji hao watoto japo wakusaidie kutoka Nje ya nyumba kwaajili ya kuota Jua na Jioni kukurudisha ndani wakati ukisubiri kufa.
Na wazee wanavyojua kuugua sasa kupelekwa hospital sijui nin Halaf unazeeka peke yako wee
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Uwiano wa 50k ni ndogo sana kulingana na kipato chake maana sidhani kama itatosha na maisha yalivyo juu kwa sasa ..... kama una hakika utapata walau 250k au 300k nenda otherwise pambana kama MUNGU amekujalia afya njema na uhai ..
 
Sasa chipsi tukanunue vibandani jamani kila mara ?akaange ale na mayai yapo
Watoto wanapenda chips wewe na wali
Mi kwangu unga wa ugali huwa Upo tu hauishi
Unawazoesha vibaya watakuwa obese
 
Back
Top Bottom