Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Mtoto anahitaji vitu vingi mnoo basi baba hana uwezo atunze kadri ya uwezo wake na sio kutafutwa kama mwizi ,kuna wababa wanatunza watoto na hawana pesa nyingi lakin wanashiriki malezi asilimia kubwa wabarikiwe sanaa
Ukiona hivyo wamama sio wasumbufu, baba akimtaka mtoto anamuona muda wowote, ana uhuru wa kuondoka naye weekend.

Kuna wamama wanajimilikisha watoto, hawataki baba awaguse, watu kama hao unawaacha wajijue wenyewe
 
Isimvunje moyo, watu hatufanani.
Mimi niliwahi kumtunza mama aliyetelekezwa kwa miezi 8.
Nilimuwekea bill ya maziwa fresh na mahitaji kila mwezi.
Na sijawahi hata kuingia kwake au hata kutamani anishukuru hata kwa mdomo.

Watu hatufanani usimdhihaki mwenzio
Sio kudhihaki ndo ukweli huo
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
kwa nini mlitengana????,mimi mwenyewe hapa nilimpa wife mtaji aanze biashara samaki jumla na rejareaja,matokeo yake akaanza kiburi na dharau za hali ya juu{baada ya biashara kuchanganya},,,basi bana alipoona kama nammbana akabeba vitu kibao vya ndani,na duka akahamishia anapopajua yeye na yeye kwenda kupanga anapopajua,,,,mimi sikuhangaika nae,na wakati anabeba vitu mimi nilikuwa grocery ya jirani namwagilia moyo baada ya kutoka kwa job,,,,,nilimpigia nikamwambia beba kila ki2 niachie vitambulisho vya kazi na bank ukimaliza huo uchafu unaofanya nipigie simu nije kulala,,,,ninavoandika hapa duka kafunga{kafilisika},,anauza pombe kali za kupima na tigo pesa yenye mtaji wa ukubwa wa sisimizi,,,watoto wako boarding ila mdogo aliondoka nae...sasa akaanza kunisumbua niwe namtumia pesa za amalezi,nimegoma nahawezi kwenda popote manake aliondoka kijambazi na mtaji wa milioni 8 nilizokopa kazini,ameacha nymba tuliyojrnga na shamba la kama hekari mbili nakwenda kupanga!!!!!!!hiyo akili au matope......??? mrudie mumeo
 
Kuna watu badaye hapa lazima watapandikizwa chuki

Ova



Wanafanya makosa makubwa sana.

Kama wanataka mtoto afanikiwe waepuke kunpandikiza chuki zidi ya bana yake.

Imeandikwa: waheshimu baba na mama ,

Hakuna provision ya kwamba kwa Baba alokulea na kukutunza tu bali Baba .
 
Haijalishi mkuu, kama umegombana na Mama wa Mtoto ndiyo usitoe hela ya matumizi?

Hapo huoni anayeumia ni Mtoto, imagine unamkuta Mtaani huyo mwanao akiwa Chokolaa, utapenda Mkuu?
Wamama wakorofi hujenga chuki kwa watoto
 
Umemzoesha hivyo, makosa ni yako. Watoto wana tabia moja in common, wanabeba kile unachowafundisha. Huenda wewe ndio unapenda choma na kaanga.

Sasa chipsi tukanunue vibandani jamani kila mara ?akaange ale na mayai yapo
Watoto wanapenda chips wewe na wali
Mi kwangu unga wa ugali huwa Upo tu hauishi
 
Haya sawa tumezaa mtoto, badae nakwambia nipe mwanangu nimlee mwenyewe hutaki unataka ubaki nae wewe utafikir mi ni mtu Baki. Pambana
 
Ni mume wako au? Wanapima DNA kama sio mume wako.

Na pili, inaweza hata isifike 50k kwa maana na yeye ana majukumu mengine.
Very straight!! On a serious note kumbe unaweza kuingia kwenye mahusiano ukaropoka kumbe mwenzio anachukua notes za salary slip yako
 
Kwa wanawake wenye akili wanahakikisha uhusiano wa bana na mwana unakuwa mzuri ili Mtoto azidi kubarikiwa haijalishi Hata kama bana hakumlea wala kumtunza.
 
Mtoto wangu hapendi vitu chukuchuku au mchesho ,samaki mbichi hali,lazima ukaange urosti
Ndizi za kukaanga na kachumbari hata bila nyama yeye anaridhika mno ilimradi tomato iwepo
Mi mtoto wangu anakula kila kilichopikwa kasoro vitunguu, nyanya utazikita pembeni
 
tatizo linaanzia baada ya wewe kufahamu mshahara kwa yeye kukwambia ama kwa wewe kuchunguza kisha unaanza mrushia manenoo kila mshahara ukaribiapoo
 
Ujeuri haufai ,kaa chini na baba watoto wako mujenge mustakabali wa watoto wenu , ukijifanya mjuaji ustawi utaenda kupewa afutatu kwa mwezi maana kwenye sheria inasema Ths 100 kwa siku....wewe unafikiri kati ya hiyo 2.8m inaingia yote bank? Akikwambia analipa Bodi , Bank ,Saccos ya Kazini ,Vikundi vyao na anabakiwa na laki mbili utakataa?
 
Sii jogoo tu hata simba dume halei watoto ni jukumu la simba jike! Hivi unajua hata simba jike akipata joto anataka dume bsasi kuwinda swala safi na kuohonga simba dume ili apate nguvu za kutosha kumshughulikia jike vizuri? Hata zamani mwanamme alikuwa anaoa wake watatu yeye anajenga tu nyumba na halafu wanawake wanalima chakula chao wenyewe na kuzaa watoto! Hii ndo asili! Sasa huyo baba hata ukumpeleka ustawi kama ana watoto wengine 10 unafikiria wewe utaambulia nini? Komaa tu tafuta riziki!
Hili somo ni muhim. Sijui tulisambaze kupitia siasa au dini!
 
Kama hana huo uwezo
Serikali ilitunga ikiwa inajitambua, na ukienda mahakamani mahakama kupitia ustawi wa jamii wataangalia hali zote na watatoa maamizi ambayo yanaweza gawanywa iwe 50/50
Ni sahihi Mkuu, ila sio jambo zuri kutelekeza watoto wako bila kuwahudumia.

Hata kama huna hela basi ujitahidi hata kidogo kinachopatikana kuwatumia.

Kuna wakati tunaweza kujivunia Nguvu za Ujana tulizonazo lakini kuna wakati utawahitaji hao watoto japo wakusaidie kutoka Nje ya nyumba kwaajili ya kuota Jua na Jioni kukurudisha ndani wakati ukisubiri kufa.
 
Back
Top Bottom