mim sina kazi mkuu kumbuka nmezaa mtoto njiti najiuguza na alinioa alisema hatak mwanamke afanye kaz asa nimeachwa sina pa kuanza nifanyaje?
1. Usimlaumu.
2. Usimtukane wala kujibizana naye Wakati unazungumza naye.
3. Kaa naye mzungumze kuhusu kulea mtoto wenu.
4. Mwambie hupendi unavyomsumbua kuhusu mtoto, ni vile hauna kazi. Mwambie akuwezeshe angalau mtaji ili ufungue biashara umlee mwanao. Ongea naye Kwa unyenyekevu, Akili na upendo.
Elewa kuwa Sisi wanaume Watoto kwetu sio lazima Sana hivyo huo uchungu unaousikia usidhani wanaume wanao. Ni wachache wanaoweza ku-feel hivyo.
5. Muombee Mzazi mwenzio, ili abadilike. Huyo ni kiumbe wa Mungu hivyo mwenye uwezo wa kumbadilisha ni Mungu mwenyewe.
Na ukimuomba Mungu usimshutumu huyo Baba Watoto,
6. Onyesha furaha muda wote, hata kama umetingwa, kitendo cha kuwa unamfuata fuata kila mara Kwa wanaume wengi wasio na Akili hukiona kama unamuabudu, hauna Njia mbadala, unamuona yeye ndiye kila kitu.
Lea mwanao Kwa uwezo wako kama atakuwa mkaidi.
7. Kama alikuzuia usiende kazini enzi hizo na unaushahidi, nenda Mahakamani kuomba akihudumie mpaka utakapopata kazi. Sheria zinaeleza kuwa kuna mazingira ambayo mwanaume anaweza kumhudumia Mtalaka wake hata kama wameachana, peleka hoja ya kuwa alikuzuia kufanya kazi na wewe uliichukulia positive lakini kumbe yeye Mpango wake ulikuwa kukufanya kuwa mtumwa wake, na hata siku akikuacha ukose muelekeo. Huo ni ukatili na uhuni, ambao haikubaliki.
Mwisho, kila Siku hapa ninawaambia Wanawake muache kutegemea Pesa za Wanaume, mfanye kazi, mjitegemee lakini ninaonekana Mbaya. Mimi ninajua nikisemacho, ninaona Wanawake wengi jinsi wanavyodhalilika, nyanyasika na kutumikishwa Kwa kutegemea jasho la mwanaume.
Tafuteni wanaume wenye Akili, wenye Haki, upendo na wakweli. Kama hataki kuzaa na wewe atakuambia toka siku ya Kwanza. Na kama hatakuhudumia atasema. Ukipata mwanaume WA hivi jua umekutana na Mwanaume mzuri. Lakini wengi hamtaki wanaume wa hivyo.