Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Kuna wakati huwa nashindwa kuwaelewa Wanaume wenzangu, hivi inakuwaje unashindwa kulea damu yako?

Imagine huyo Dada yupo tayari kupokea hata shilingi 50,000 kwa mwezi. Hiyo elfu 50 inatosha Kula, mavazi au mtoto akiugua kweli? Kwa hiyo elfu 50 huyo Mtoto atapata Sare za shule au hata Kalamu na Daftari akianza shule?

Tuweni na huruma wakati mwingine, wewe usingehudumiwa na Baba yako ungefika hapo ulipo kweli?

Kama hauko tayari kulea Mtoto, niwasihi Wanaume wenzangu ni bora kutumia Kondomu au mtumie uzazi wa mpango. Tutakuja kupata dhambi na laana za Uzeeni kwa kutelekeza damu zetu.
Una uhakika wote tumelelewa na Baba zetu.. vingine ni kama kurithi.. mwanamme aliyekulia mazingira ya kutelekekezwa na Baba na akakua kwa malezi ya Mama kuna uwezekano mkubwa naye akikua akawa katili na kutelekeza watoto.. haoni shida.
 
Masikini umeandika kwa huruma hadi nimejisikia vibaya. Pole sana kama una roho ndogo Jf sio sehemu ya kuomba ushauri mpenzi.
Siku hizi JF imekuwa ya ovyo sio sehemu serious kabisa. Wanaume wa Jamii forum 90% ni wa ovyo wana roho mbaya na chuki kwa kila mwanamke. Wanapenda kuwatukana na kujudge wanawake bila hata kujua uhalisia.
Wanaume wa JF wao ishu za ndoa na watoto wanaona wanawake ndio wakosaji kiasi cha kuwatukana ni malaya na wafwata mali/hela kwa wanaume au umejibebesha mimba.

mama cutest nilichotaka kukwambia ni usiumie na comment za wapumbavu hawa na wala zisikupe shida na usijibizane nao wengi wana stress za maisha na tatizo la afya ya akili. Watatukana ila ndio ukweli huo.

Wewe kama ni mke wa ndoa na una cheti swala lako kaanzie bakwata huko utapata msaada na mwisho ugua pole ukishapona jishighulishe ulee wanao kwamwe usikubali kuambiwa uache kazi eti kaa nyumbani unaona madhara yake ndio hayo.
Kipofu unamuelekeza kipofu mwenzako
 
Ukisema Ndoa sio priority yako mbona unataka benefits za ndoa sasa?

Ukipata watoto malezi sahihi ni ndani ya Ndoa, ukiwa nje ya Ndoa hapo ni wewe na nafsi yako na sio wewe watoto na mume wako.

Dada nahisi unachangamoto zako. Huyu mwanaume anaweza kuwa mkorofi ila wewe una part yako kubwa katika kuvunja hii ndoa. Huwa nakutana na visa vya namna hii, ukitumia hisia utajikuta umetetea mwanamke na kumbe yeye ndie mkorofi.

Mimi nadhani fanya kujitathimini kwa kina hili eneo.
sijataka benefict za ndoa ningezitaka si ningeenda bakwata na cheti na talaka ningemwambia aandike maan aliitamka?? niliishi maisha yangu sikuwa na tamaa na mali zake mkuu nawez toa mfano alikuwa ana usafiri na nmekaa naye miaka 4 alinipeleka mpaka shule ya driving nikikwambia nilikataa mpk leo sijui lolote kuhusu ku drive coz sikuwa na tamaa laiti ningekuwa na tamaa ningefanya usafiri wangu ningetamba nao mpaka kwetu ila sikuwa na pigo za show off
 
Kama hawezi kuwalea kwanini alazimishe kubaki nao?
Kama nitahitaji wanangu alafu ukawazuia bila sababu ya msingi, hakika utalea mwenyewe.
Siyo kutuletea "vitisho ooh fainali uzeeni" kama vile nyie ndiyo Mungu

Tunasubiri tu hiyo fainali uzeeni ije vyovyote[emoji1787]
Achana na hao wataka utelezi wa bure
 
Ukisema Ndoa sio priority yako mbona unataka benefits za ndoa sasa?

Ukipata watoto malezi sahihi ni ndani ya Ndoa, ukiwa nje ya Ndoa hapo ni wewe na nafsi yako na sio wewe watoto na mume wako.

Dada nahisi unachangamoto zako. Huyu mwanaume anaweza kuwa mkorofi ila wewe una part yako kubwa katika kuvunja hii ndoa. Huwa nakutana na visa vya namna hii, ukitumia hisia utajikuta umetetea mwanamke na kumbe yeye ndie mkorofi.

Mimi nadhani fanya kujitathimini kwa kina hili eneo.
kamwe usikae ukamsikiliza mwanamke na kutoa maamuzi!! asilimia tisin wao ni vivuruge na yakishavurugika wanakimbilia kwenye jamiii kutafuta huruma na support coz wao machoz na kulialia na kuongea sana ni jadi yao..

Be warned na wanawake!!!!
 
Kumbe hadi kwenye ndoa mnapangiana!!
Jukumu la kubeba mimba analo mwanamke, yeye ndio anajua lini na saa ngapi mimba itaingia, yeye ndio anapanga akupe leo au kesho.

Sio lazima ndom, kuna njia nyingi za uzazi wa mpango. Anapojisahahu na kuleta habari za mimba wakati haukuwa mpango wetu ninaweza kumshtaki mahakamani kwa kuniongezea majukumu sikuyahitaji.
 
Uzee unatisha Mkuu, si uliona Baba yake Diamond alivyokuwa anaomba huruma ya Watanzania kuwa ametelekezwa na Mwanaye.

Na mbaya zaidi mtoto ambaye ulimtekeleza unakuta anafanikiwa maisha na wewe ndiyo unakuta hata ugali wa siku unashindwa kumudu kuupata.[emoji28]
Waliotelekezwa na kufanikiwa ni wangapi?
 
mim sina kazi mkuu kumbuka nmezaa mtoto njiti najiuguza na alinioa alisema hatak mwanamke afanye kaz asa nimeachwa sina pa kuanza nifanyaje?

1. Usimlaumu.
2. Usimtukane wala kujibizana naye Wakati unazungumza naye.
3. Kaa naye mzungumze kuhusu kulea mtoto wenu.
4. Mwambie hupendi unavyomsumbua kuhusu mtoto, ni vile hauna kazi. Mwambie akuwezeshe angalau mtaji ili ufungue biashara umlee mwanao. Ongea naye Kwa unyenyekevu, Akili na upendo.
Elewa kuwa Sisi wanaume Watoto kwetu sio lazima Sana hivyo huo uchungu unaousikia usidhani wanaume wanao. Ni wachache wanaoweza ku-feel hivyo.

5. Muombee Mzazi mwenzio, ili abadilike. Huyo ni kiumbe wa Mungu hivyo mwenye uwezo wa kumbadilisha ni Mungu mwenyewe.
Na ukimuomba Mungu usimshutumu huyo Baba Watoto,

6. Onyesha furaha muda wote, hata kama umetingwa, kitendo cha kuwa unamfuata fuata kila mara Kwa wanaume wengi wasio na Akili hukiona kama unamuabudu, hauna Njia mbadala, unamuona yeye ndiye kila kitu.
Lea mwanao Kwa uwezo wako kama atakuwa mkaidi.

7. Kama alikuzuia usiende kazini enzi hizo na unaushahidi, nenda Mahakamani kuomba akihudumie mpaka utakapopata kazi. Sheria zinaeleza kuwa kuna mazingira ambayo mwanaume anaweza kumhudumia Mtalaka wake hata kama wameachana, peleka hoja ya kuwa alikuzuia kufanya kazi na wewe uliichukulia positive lakini kumbe yeye Mpango wake ulikuwa kukufanya kuwa mtumwa wake, na hata siku akikuacha ukose muelekeo. Huo ni ukatili na uhuni, ambao haikubaliki.

Mwisho, kila Siku hapa ninawaambia Wanawake muache kutegemea Pesa za Wanaume, mfanye kazi, mjitegemee lakini ninaonekana Mbaya. Mimi ninajua nikisemacho, ninaona Wanawake wengi jinsi wanavyodhalilika, nyanyasika na kutumikishwa Kwa kutegemea jasho la mwanaume.

Tafuteni wanaume wenye Akili, wenye Haki, upendo na wakweli. Kama hataki kuzaa na wewe atakuambia toka siku ya Kwanza. Na kama hatakuhudumia atasema. Ukipata mwanaume WA hivi jua umekutana na Mwanaume mzuri. Lakini wengi hamtaki wanaume wa hivyo.
 
Labda anawatoto wengine sehemu zingine.
Hoja hapo yaangaliwe mahitaji ya mtoto ya lazima, kisha gharama alafu yagawanywe Kwa Mbili yaani Baba na Mama. Full stop.
Hakuna sheria inayosema utapigiwa hesabu ya Mama na mtoto, haipo.. huyo Mama wa mtoto ni mtu mzima na ana wazazi wake na yeye, mkishafika Ustawi. Wanaangalia umri wa mtoto na mahitaji yake ya msingi. Wataangalia kama anakunwa uji kwa mwezi unga na sukari ni sh ngapi, nguo, sabuni, mafuta, nauli ya kwenda clinic mara moja, kama Jamaa ni mtumishi mtoto ana bima tayari hapo kwenye matibabu halambi hata 100 mbovu.. ikipigwa hesabu haiwezi kufika Tsh 100,000 kwa mwezi, hata kama ana mshahara wa milioni 10 haihusiani.. ndo maana wenye Akili huwa wanajishusha tu na kuwa wapole kuna wakati Baba anaweza kutoa pesa kuliko hiyo.. ila ukimpeleka ustawi ndo umemtibua kabisa.. ingekuwa ulaya huko sawa lakini kibongo bongo sijui hata kama ipo sheria ya kumfunga jela mwanamme aliyekataa kuhudumia mtoto..
 
Masikini umeandika kwa huruma hadi nimejisikia vibaya. Pole sana kama una roho ndogo Jf sio sehemu ya kuomba ushauri mpenzi.
Siku hizi JF imekuwa ya ovyo sio sehemu serious kabisa. Wanaume wa Jamii forum 90% ni wa ovyo wana roho mbaya na chuki kwa kila mwanamke. Wanapenda kuwatukana na kujudge wanawake bila hata kujua uhalisia.
Wanaume wa JF wao ishu za ndoa na watoto wanaona wanawake ndio wakosaji kiasi cha kuwatukana ni malaya na wafwata mali/hela kwa wanaume au umejibebesha mimba.

mama cutest nilichotaka kukwambia ni usiumie na comment za wapumbavu hawa na wala zisikupe shida na usijibizane nao wengi wana stress za maisha na tatizo la afya ya akili. Watatukana ila ndio ukweli huo.

Wewe kama ni mke wa ndoa na una cheti swala lako kaanzie bakwata huko utapata msaada na mwisho ugua pole ukishapona jishighulishe ulee wanao kwamwe usikubali kuambiwa uache kazi eti kaa nyumbani unaona madhara yake ndio hayo.
Wewe sasa ndio wale wapotoshaji tunaowaongelea hapa kila siku. Hapo akisemwa baba mtoto wa huyo mwanamke ndicho unachotaka kukisikia. Ila anapohojiwa mwanamke basi sisi ni roho mbaya, wakorofi, hatujielewi, tunatukana.

Hii mentality ya kuamini mwanamke always yupo right ilijengwa na kizazi cha wanaume waliokuwa wanakumbatiwa sana na mabibi na mama zao maisha yao ya utotoni muda mwingi. Wanaume hawa wakabeba vinasaba vya kike wakiona mwanamke anasemwa kwa mabaya na uzembe wake na wao wanajikuta automatically wanajiskia kama wanashambuliwa na kutukanwa yote hii ni matokeo ya kubeba akili ya kike.

Sasa wanaume wa miaka hii wamekuzwa kitofuti na wanaweza kutambua mipaka ya haki ndio maana unaona hata mtu aje na story kuwa mwanaume alimkatakata mapanga watataka kujua huyo mwanaume ulimfanya nini hadi afikie hatua hiyo kabla hawajaanza kukuonea huruma na kuleta hisia za kutetea mwanamke kwasababu ya kutambulishwa kama kiumbe dhaifu kwenye jamii ile hali kuwa si kweli.

Nadhani ifike wakati tuanze kujua na kutambua haki yako inapoishia ndipo ya mwenzako inaanzia so its very important kujua mipaka. Wanawake hamna mipaka na haki zenu ndio maana mnajikuta mara nyingi sana mpo katika eneo la mwanaume na hapo mwanaume akiwasha moto mnasema ni mkorofi sababu unahaki ya kuingia katika haki za mwanaume na kuchukua unachotaka.

Nitakupa mfano, wewe unaweza kutana na mwanaume ana muonekano mzuri na ana uwezo wa kifedha. Ikatokea ukaanza kujijengea fikra kuwa ukiweza kumrubuni kimahaba akakukubalia wewe kuingia himaya yake na kutumia mali zake kujinufaisha wewe binafsi then hapo unakuwa umeshaanza kuvuka mipaka ya haki. Kwann uanzishe mahusiano kwa misingi ya tamaa za mali?

Ukijastukia ni baadae umejitegesha ujauzito, mnapata mtoto unaanza sasa kuwa direct kudai kwa kulazimisha kutumia mali za mwanaume kulea mtoto ambaye wewe kwa tamaa zako ndie ulisababisha kutengenezwa na mwanaume kakushitukia sasa ndio maana unaona balaa linakuwakia.

Mabinti/wanawake wa sasa tamaa zenu ndio mtaji wa maisha na hiki ndicho kinawaliza kila siku sio wanaume. Someni vitabu vya MUNGU kila wasaa mnaopata sio kusoma post za kidangaji huko mitandaoni ili akili zenu ziwe safi muweze kuamua kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU sio kwa uwezo wa UROHO MTAKATIFU.
 
Amri ya Tano, Waheshimu Baba na Mama yako ilo upate heri na baraka
AMRI KUMI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana MUNGU wako usiabudu miungu wengine
2. Usitaje bure jina la MUNGU wako
3. Shika kitakatifu siku ya MUNGU
4. Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani
5. Usiue
6. Usizini
7. Usiibe
8. Usiseme uongo
9. Usitamaman mwanamke/mwanaume asie mke/mme wako
10. Usitamani mali za watu
 
Pambana lea mwanao, achana nae.

Ushawahi ona jogoo analea vifaranga? Wanaume hawaleagi, its nature....atahudumia mtoto Kama na wewe unamuhudumia.

Kama uko tayari kufata matumizi ya mtoto guest endelea kumsumbua, Kama unajali utu wako pambana mwenyewe.....mlezi mkuu ni Mungu, mtoto atakua tu bila yeye.

Angalizo, akileta matumizi usikatae na usimlishe mtoto sumu kumuhusu.
Nakazia hapa📌🔨
 
mi sihitaji pesa yake naomba alete mahitaji ya watoto kila mwezi tu maan kuhusu pesa naonekana huku sijui nataka pesa no nataka mahitahi niweze msaidia mama majukumu apa maaan nimeletea familia na mamaangu hajaajiriwa anabangaiza tu
So dada wakati unaolewa na huyu jamaa ni kweli ulimpenda yeye damuni, au ndio ilikuwa ni "Yule kaka ni engineer wa tanesco ana hela balaa lazima nimpate nimlie vihela vyake". Watoto wa kike mnatabia ya kusonga ugali kabla hamjaangalia unga upo kiasi gani mwisho wa siku ugali hauivi maana maji yanazidi unga.
 
1. Usimlaumu.
2. Usimtukane wala kujibizana naye Wakati unazungumza naye.
3. Kaa naye mzungumze kuhusu kulea mtoto wenu.
4. Mwambie hupendi unavyomsumbua kuhusu mtoto, ni vile hauna kazi. Mwambie akuwezeshe angalau mtaji ili ufungue biashara umlee mwanao. Ongea naye Kwa unyenyekevu, Akili na upendo.
Elewa kuwa Sisi wanaume Watoto kwetu sio lazima Sana hivyo huo uchungu unaousikia usidhani wanaume wanao. Ni wachache wanaoweza ku-feel hivyo.

5. Muombee Mzazi mwenzio, ili abadilike. Huyo ni kiumbe wa Mungu hivyo mwenye uwezo wa kumbadilisha ni Mungu mwenyewe.
Na ukimuomba Mungu usimshutumu huyo Baba Watoto,

6. Onyesha furaha muda wote, hata kama umetingwa, kitendo cha kuwa unamfuata fuata kila mara Kwa wanaume wengi wasio na Akili hukiona kama unamuabudu, hauna Njia mbadala, unamuona yeye ndiye kila kitu.
Lea mwanao Kwa uwezo wako kama atakuwa mkaidi.

7. Kama alikuzuia usiende kazini enzi hizo na unaushahidi, nenda Mahakamani kuomba akihudumie mpaka utakapopata kazi. Sheria zinaeleza kuwa kuna mazingira ambayo mwanaume anaweza kumhudumia Mtalaka wake hata kama wameachana, peleka hoja ya kuwa alikuzuia kufanya kazi na wewe uliichukulia positive lakini kumbe yeye Mpango wake ulikuwa kukufanya kuwa mtumwa wake, na hata siku akikuacha ukose muelekeo. Huo ni ukatili na uhuni, ambao haikubaliki.

Mwisho, kila Siku hapa ninawaambia Wanawake muache kutegemea Pesa za Wanaume, mfanye kazi, mjitegemee lakini ninaonekana Mbaya. Mimi ninajua nikisemacho, ninaona Wanawake wengi jinsi wanavyodhalilika, nyanyasika na kutumikishwa Kwa kutegemea jasho la mwanaume.

Tafuteni wanaume wenye Akili, wenye Haki, upendo na wakweli. Kama hataki kuzaa na wewe atakuambia toka siku ya Kwanza. Na kama hatakuhudumia atasema. Ukipata mwanaume WA hivi jua umekutana na Mwanaume mzuri. Lakini wengi hamtaki wanaume wa hivyo.
asante member barikiwa
 
iko hivi mimi nmeolewa na tuna miaka 4 na nusu ya ndoa now nina miaka 24 ex husband ako na 31 ...ye ni engneer tanesco kipindi tunaowana sikukaa sana naona ni saba ile nikabeba mimba nikajifungua mtoto wa kwanza ..nikaja beba mimba nikajifungua wa pili siwezi sema mimi ndo nina matatizo au yeye maan nitakuwa nakosea pengine mimi nilikosea au yeye pia alinikosea maan nikisema alinifanya hivi sijui vile ntakuwa pengine namponda yeye kumbe shida ninayo mm ila mimi ndiye nikawa naumia kila nikijitahid kurekebisha ilishindikana basi tukawa tunaishi ndan kama watu hawajuani chuki yule baba kwangu ndo ilizidi maan nahis alinichoka zaidi kutokana na kuwa kinyume nae baadhi ya mambo yake ambayo sikuona sahihi au kutokana na tofaut zetu ukimwambia hiki tunaishia kulumbana kutokana na pengine tuliyopitia tulichokana ila mimi kama mm nilivumilia sababu ya mtoto apo nina mimba miez 7 ikafikia hatua mbaya mpaka napigiwa simu na manzi za nje zinanitukana nilipata pressure ya mimba nikajifungua siku ambazo sio makadirio nilijifungua week 29 mtoto njiti na siku najifungua hakuwa nyumban alilala kwa manzi zake alipigiwa simu na nesi alete vifaa hosptal kwa maan kabla ya kuingia theatre niliandika namba za wadhamin wawili na sikwenda kwa nia ya kujifungua ila nilikwenda kama clinic ndo pressure ikanishika ikabidi nikimbizwe op fasta basi nilipozinduka nilimuona hosp na mama yang na baadhu ya ndug zake apo mtoto alikuwa yupo kwenye incubeta ile ya kupumulia tulikaa sana hosp bas baada ya kuruhusiwa nilikaa week mbili alinipa talaka kwamba hanitaki ye anataka kuoa niende kwetu nikawasiliana na kwao tulikaa kikao ila alionekana mkorofi sana bas mpaka hivi navoongea mamaangu kajitoa kabisa kwenye maswala ya kesi yetu nipo napambana mwenyew ila kinachonifanya nipambane naye kwa sasa hali yangu haijaimarika sana kutokana na op nilifanyiwa mbili ya mtoto na ya hernia ya kitovu ambapo huko nyuma nilipata op ya nje ya kizazi na ya mtoto wa kwanza jumla ninayo mishono 4 kwa muda mfupi kwahiy sikukava sana hivo mamaangu analalamika anaelemewa sababu mamaangu ni kibarua tu hana biashara ya ajira ila yeye tulivyoachana alinitamkia sitapata chochote sikuhangaika maan tulijenga tukifanya maendeleo tukiwa wote sikutak kusumbuana nae kwenye mali maan niliamini ipo siku ningepata mali zangu na mimi je (nyie mnaosema nimefwata mali je ningeshindwa enda bakwata kudai mali zang?? msipende mtukan mtu hamjui nachopitia maan cheti ninacho na kuhus msharah alikuwa ananambia mpk siku anapandishwa cheo alinionyesha karatas kabisa ya ofisi mmenitukana san

cha mwisho nilitak kupambania haki za watoto tu ndo naan niliomba msaad wapi nipitie niwez pata haki yangu
Pole, sikuzote mimi nasemaga jf sio sehemu ya kuomba ushauri, humu kuna watu wajuaji wa kiwango cha lami, at least ukiwa humu jitahidi kunotice mtu mmoja unayeona ana akili ukijiridhisha mwendee hata pm kaombe ushauri huko lakini si hapa public utaishia kuumia nafsi yako, hapa ni mada za kuchakata mbususu basi na utapata wachangiaji positive page 15+
 
Back
Top Bottom