Wakuu, nilitangaza kuuza nyumba yangu na nikaletewa na dalali mteja. Mteja huyo akaomba kulipia nyumba hiyo kwa installment mara tatu. Awamu ya kwanza ilikuwa tarehe 23/12/2023. Awamu ya pili ilikuwa iwe mwezi wa tatu lakini alichelewa akanilipa mwezi wa tano. Na malipo ya mwisho alitakiwa kunilipa tarehe 25/6/2024.
Ilipofika hiyo tarehe nilisafiri kutoka mji naoishi kwenda huo mkoa nilipouza nyumba. Siku moja kabla nikampigia simu kwamba kesho tunakutana saa ngapi kwa mwanasheria wake ambae alituandikisha mkataba akasema yupo safari atanipigia jioni.
Jioni hakupiga na siku ya malipo hakutokea. Mwanasheria wake alimpigia akasema ana wageni atapiga simu lakini hakupiga. Baada ya week ikanibidi niondoke nirudi mji naoishi huko mikoani.
Mteja yule alikuja kunitafuta mwezi BAADAE na nikamweleza jinsi alivyonisababishia hasara kwani NAMI nilikuwa NAENDA kununua nyumba nyingine na nimekosa. Matokeo akawa mkali sana na hakuonyesha ushirikiano. Nikamwambia basi kwakuwa umevunja mkataba na mkataba unasema ukichelewesha fedha ulipe 18%ya ziada naomba tufate mkataba, kwani Mimi nilitumia gharama kusafiri na pia nimekosa nilichopanga kufanya na hela hiyo. Alikuwa mkali na akasema anataka nimrudishie hela yake yote na yeye HAYUPO tayari kuongezea hela yoyote Ile hata kama alivunja mkataba.
Leo hii amenipigia simu ananiambia kwamba amepata hela na anataka alipe hela bila kujali hasara na bila kufata mkataba kama unavyosema. KUMBUKA alitakiwa kulipa hela tarehe 25/6, Leo ni mwezi wa kumi. Na anasema ule mkataba kwasababu ilishapita miezi mitatu hautumiki Tena. Wakuu hii ni sawa?
Sasa wakuu naombeni ushauri nifanyeje?? Nyumba yangu sio mbaya na nilikuwa naiuza Ili ninunue nyingine Dar, nae kachelewa kunilipa hivyo sijaweza kununua... Nikiiuza kwa mtu mwingine nitakuwa nimetenda kosa??
Je huyu mteja SI anatakiwa afate mkataba kama unavyosema??
Mkataba huo ulitengenezwa na mwanasheria wake mwenyewe. Je anapaswa Kuongezea hela ama asubiri niuze niirudishe pesa yake.
Naombeni maoni na ushauri