Msaada: Nimeuza nyumba, niliyemuuzia hataki kunimalizia fedha yangu mwezi wa nne huu, nikiuza tena kuna kosa?

nilicho gundua hii nchi tunaishi kishkaji na kijamaa sana

watu wanauziana kisheria, wanakiuka na wanamalizana kishkaji kwa kile kile kinacho itwa ujamaa na uswahili

alipe iyo 18% asilete uswahili
 
Kwasabab
nimemwambia afate mkataba unavyosema, alipe ASILIMIA 18% kama riba kwa kuchelewesha hela. Yeye hataki na anakuwa mkali ilhali Mimi nimekosa nyumba niliyotaka kununua kwa sababu yake. Pesa sijala ipo na alichonikera zaidi alipolipa awamu ya kwanza alienda kufukuza wapangaji wangu..Kuna walioondoka na Kuna waliobali. Kistaarabu alitakiwa amalize kulipa fedha kwanza nyumba iwe Mali yake ndipo kwa utaratibu wapangaji waondoke kwani wapangaji pia Wana haki zao. Sasa huoni huyu sio mstaarabu? Huoni ni muharobifu na Hana jema??. Mimi sikatai hela yake ila ailipe na Ile 18%. Na awe mstaarabu asinigombeze
 
Kama ana dhamira ya kukumalizia pesa zako chukua tu. Gharama utakayotumia kufuatilia madai ya ziada yanaweza kuvuka hata madai yenyewe pamoja na kupotezeana muda.

Kuna watu wameumbwa kuwa watata tu na kwa sheria za kipuuzi za nchi hii unaweza jikuta unapoteza haki yako hata kama upo sahihi.
 
Uza umrudishie hela yake.
 
Njooo ofsin ushauriwe kisheria na ulipe consultation fee
 
Unamaanisha, umeshakula Hela ya MTU, ila kwakua kachelewa kumalizia Hela, unataka Uiuze?.


Kwakua Kukuchelewesha ,hakujaharibu nyumba yako.

MRUDISHIE Hela yake, ubaki na nyumba yako uuze .


Bila hivo ACHA JEURI NA JANJA JANJA ZA SHERIA, sote tunajua. shería zetu ni mbovu japo ni Sheria



UTABAKWA AU KUFA MAPEMA endapo utafanya unachotaka kufanya.


Usiseme hujaambiwa.
 
Huyo mtu kabila gani? Tuanzie hapa.
 
Kwa kweli amrudishie tu pesa. Aendelee na mishe zingine. Watanzania si watu wa kuheshimu mikataba na sheria.
 
Tatizo linaanzia pale uliporuhusu mnunuaji kujipangia aina ya mkataba anaoutaka,hapo umekwama vibaya sana na ukisema ujitekenye kufanya kitu kuuvunja huo mkataba kesho mtakutana mahakamani na fidia umlipe wewe.

Kwanini ulikubali kitu cha hovyo kama hiki?huna washauri au huna hata mtu mnaekaa pamoja japo kwa dakika kadhaa mkashauriana siku yenu ilivyoisha au mipango yenu?
 
Chukua pesa iliyobaki Kisha uendelee na shughuli zako ,ogopa kitu kesi hata kama una uhakika wa kushinda ,lazima upigwe tarehe hadi kichwa kikukae sawa.hapo kuja kupata suruhu ukipeleka kesi kwenye mabaraza ya ardhi ni zaidi ya miaka mitatu.

endesha kesi pale panapokuwa hakuna suruhu,ila kama Kuna suruhu jaribu kufuata suruhu kwanza,

Nina kesi Baraza la ardhi wilaya ,huu ni mwaka wa nne tunajisomba Barazani,kula na kulala ni gest house,kesi yenyewe ni kumfukuza baba mdogo kwenye nyumba Ambayo ni ya baba yangu,baba mdogo anadai nyumba ni yake na amefoji barua za manunuzi, Mimi Nina Ofa na hati yenye kuonesha umiliki halali wa kiwanja hicho toka mwaka 1972,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…