Msaada: Nina 30,000 hapa, nahitaji kuanza biashara yoyote ile sasa hivi. Niko DSM

Msaada: Nina 30,000 hapa, nahitaji kuanza biashara yoyote ile sasa hivi. Niko DSM

Elfu 30! Huyu ametoka kwenye nyumba ya watu kama hausigali. Atalala wapi🤔? Hiyo biashara atafanya akiwa anatokea wapi? Hayo matunda atayalaza wapi ili atakapoamka aanze Tena safari ya kutembea. Sawa. Sasa Agnes,,,Daah!
House girls pia wanao ndugu
 
Nlifikishaga 11m nikaongezea hela kidogo nkauza gari yangu nikanunua gari ya fuel consumpion ndogo ili nipunguze ukali wa maisha saivi nna kama 1.5m kama kepitol nataka niende nayo mdogo mdogo sitaki tamaa.
Chagua na timu zako chache za kutembea nazo, timu ambazo zina consistency ya matokeo usizibadili tembea nazo mwanzo mwisho, hizo timu zako kila weekend huwezi kosa odds 2 stake, na stake iwe constant ukila mara2 ukapoteza moja bado unafaida mfano odds 2 kwa laki ukila Mara mbili ni nne ukipoteza Mara moja bado unabakiwa na laki tatu, kubadilibadili timu na kupoint kila ligi duniani lazima upoteze, mm ligi zangu ni saba tu, ujerumani, Czech,Netherlands, england, laliga tanzania na brazil kote huku Nina timu zisizozidi mbili, Brazil ni corners tu. Na option yangu mkubwa ni magoli mawili tu kwa individual wakiwa nyumbani au wote akiwa away.
 
Elf 30, kubwa hiyo inategemeana na uko maeneo gani Kuna dada anadamka mazizini na elf 10 yake ananunua nyama maana pale asubuh inakuwa bei rahisi anaenda kukatakata na kuuza supu kila siku anaingiza faida ya 5000 na mtaji wake uko pale pale
 
Chagua na timu zako chache za kutembea nazo, timu ambazo zina consistency ya matokeo usizibadili tembea nazo mwanzo mwisho, hizo timu zako kila weekend huwezi kosa odds 2 stake, na stake iwe constant ukila mara2 ukapoteza moja bado unafaida mfano odds 2 kwa laki ukila Mara mbili ni nne ukipoteza Mara moja bado unabakiwa na laki tatu, kubadilibadili timu na kupoint kila ligi duniani lazima upoteze, mm ligi zangu ni saba tu, ujerumani, Czech,Netherlands, england, laliga tanzania na brazil kote huku Nina timu zisizozidi mbili, Brazil ni corners tu. Na option yangu mkubwa ni magoli mawili tu kwa individual wakiwa nyumbani au wote akiwa away.
Okay sawa sawa masta nimekusoma ivi wikend wanarud ulingoni si ndio ?
 
Nilishawahi simulia kitu kwenye Uzi wangu mmoja hivi na moja ya kazi ambazo nilizisimulia nilizofanya ilikua ni hiii hapa chini 👇

JamiiForums


KUTEMBEZA MAJI NA SODA

Nakumbuka ndio miaka hiyo naingia Dar nikapata wana siwajui ila niliwaona tu ni wapambanaji nikawaelezea nia yangu,shida yangu wakaniambia, "imeisha hiyo wakwetu, twende ukachukue mzigo upge kazi." huyu jamaa yeye alikua anauza maji ya kutembeza, juice, soda za take away, biskut nk.
Nikamwambia mimi mtaji sina lakini, akasema usijali nakupeleka kwa boss wangu atakupa mzigo. Kweli tukatoka hao tukafika kwa muhindi mmoja hivi akanitambulisha, akamwambia "mimi iko letea wewe kijana ya kazi." Muhindi akauliza "hii hapana sumbua kama ile nyingine?" Jamaa akamwambia hii iko safi kabisa, basi baada ya hapo nikapewa kitrey Jamaa akanipakia mzigo wa kwenda kuzungusha.
Unachotakiwa ni unaenda na mzigo, unauza kwa bei ya reja reja ila wewe unachukua kwa bei ya jumla. Take away pale tulikua tunachukua kwa 800 wewe unauza 1000 na faida ni 200. Basi jioni mzigo utakaobaki unarudisha kwa muhindi, fresh maisha yanaenda.

Unapewa Vinywaji Free unaenda kuuza hiii ipo hadi Leo na watu ndio kazi inayowapa mtaji wa kuishi.

Mtaji si lazima pesa, Unaweza pata watu wakakuamini,connection kupitia kazi hiyo.
 
Najua hukosi Sufuria kwako, au vifaa kama huna basi jitose nunua bakuli 3 sahani 3,vijiko vitatu

Vifaa tumia 10k

CHUKUA 10,000 nenda kanunua utumbo Machinjioni utumbo wa bomba na taulo akuchanganyie. Njoo uza pika jioni uza.

Nunua Thermos ya 15,000

Tengeneza Uji wako Mweupe wa Mahindi, nunua blue band tu

na vikombe vyako Sambaza uza uji kikombe jero.

Dada hizi idea unapewa sio za kisista duu kuziingiza kwa practical inakubidi ujikatae kweli kweli.
 
Jaribu biashara za msimu ambazo ni matunda mbalimbali

Kwa elfu 30 unaweza kutafuta sehemu nzuri ukauza matunda kama machungwa, maparachichi, mitoo, misasati, maembe etc. na utabadilika taratibu kadri misimu inavyoenda

Mtaji ukikua unaweza kuendelea na biashara nyingine kama matikiti, n.k
 
Ingekuwa ni mwanaume anaomba ushauri huu angepewa kila aina ya kejeli na matusi..Ila kwa sababu mwanaume ni dhaifu kwa mwanamke, wanaume wengi wanatoa ushauri kwenye hili ili hali hawawazi kuhusu lililoulizwa ila wanatega ili kumpata huyu binti maana ashaonesha udhaifu tayari kujitangaza hadharani kabisa kwamba anahitaji mwanaume in indirect way..Wanaume wenzangu tuweni makini kwa hili..Hii ni biashara kabisa na yawezekana huyu akawa tapeli pia...pia uandishi wake unatia ukakasi ni kama mwanaume huyu kabisa 100%.
 
Hello JF Members,
I'm madam Agnes, leo tena humu Jukwaani. Nisiwachoshe, niko na 30k kwenye kipochi, nahitaji kuanza biashara yoyote ile itakayowezekana sasa hivi

Mazingira ni Dar es salaam. Siko na aibu, naeza fanya yoyote ile. Ilimradi tu itoshe kunipatia mlo pamoja na saving kidogo kwa ajili ya masuala ya baadae

Sihitaji kuajiliwa, maake naondoka hivyo kwenye nyumba ya watu nilipokuwa naishi as house girl, watu hawana shukhrani jamani

Mwenye wazo lolote lile ambalo limemsaidia kuendesha maisha, ama ameona limemsaidia somebody ku run his/her own life anipatie basi. Hata kama ni idea ya kiume, I'm ready

I'm waiting...
Fanya biashara ya kuuza matunda chukua dishi lako nenda kwenye masoko ya jumla nunua matunda pita barabarani ukiuza
 
Kuwa winga wa kkoo ila in difference way ambayo mawinga wengi wanafanya pale karikaoo.

1. Fungua akaunti Facebook & Instagram. make sure Instagram iko kwenye professional Mode.
2. Connect Instagram & Facebook Page.
3. Install whatsapp business then connect to Facebook Page.
4. Jifunze sponsored ads (Facebook & Instagram).
5. Nenda kariakoo duka la nguo za kike omba kuwa winga wao.
6. Jifunze ad copy.

Kama utafanikiwa hatua hizo 6 kwa ukamilifu , anza ku sponsor bidhaa kwenye instagram na facebook kwa kuweka $7 kwa siku 7 uku ukiongeza bei kwenye kila bidhaa, tafuata wateja ambao wako kwenye mwendokasi ili iwe rahisi kufanya delivery kwa haraka bila kuchelewa.

Unaweza tafuta duka la nguo za kike official ili udili na wateja wenye pesa na kuachana na wateja wasotea tumbo 🙂


"Success is a mindset game"
 
Kubali tu kuajiriwa kwa muda mfupi japo upate hela ya kuongezea maana hiyo 30,000 ni kidogo sana, ukiweza kupata mtaji wa kumiliki Genge la Matunda na Mbogamboga siyo mbaya.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
kanunue mzani unauzwa 30,000 ingia mtaani uwe unapima watu uzito kwa siku huwezi kosa 10k uzito utakuwa unapima kwa sh 200
 
Anzisha biashara ya kukatakata matunda mchanganyiko na kuuza sahani mia 5 hadi elfu 1 inategemea na ulipo, utanishukuru.
Na nikisema labda hizo plates nikazisambaze stand ama posta, nitapata wateja kweli!!!? Maake niliwahi kufanya hii biashara mwaka jana, lakini ndani ya siku tatu tu nilikata tamaa kutokana na wateja kuwa wachache

Sijui biashara yangu ilitupiwa mapepo!!🤔

Kingine kinachoniwazisha, nitafanya nini ili mchanganyiko huo ubaki kuwa wa baridi, na sina hata kijokofu kidogo?

Na je, hakuna malipo ta ziada ya kufanya biashara stendi?
 
Wazo zuri

Angekuwa maeneo ya Maswa ningemuuzia debe kwa moja kwa 40k

Pure,dry weed

Faida yake ni more than 100%

Sema Dar mbali
Oyaaa ya maswal siijui, ingekua ya Arusha tungefanya jambo untumie cyo ya biashara lkn
 
Back
Top Bottom