Msaada: Nina aibu kupita kiasi, nifanyeje kuondokana na hali hii?

Mara ya mwisho nilitongoza live 2015. Nikaapa sitarudia tena niliaibika sana
 
In term of money I'm comfortable sir. Ila yaani aibu zipo tu, duuh yaani sijui nitakua baba wa namna gani mbele ya wanangu

Sina hakika mazingira unayokaa na kufanyia kazi yana interaction kubwa kiasi gani. Nakuelewa tatizo lako na naamini limechangiwa sana na malezi ambapo ulikua hauchanganyiki sana na inaelekea ulikua kwenye mazingira ambapo hahukua na watoto wenzio wa kucheza Bali watu wakubwa na kila mtu alikua busy na mambo yake.

Nimewahi pitia hiyo nikiwa primary mpaka olevo. Nimewahi kuruka dirisha ili niingie darasani kuepuka kupita mbele ya darasa kisa kulikua kumekaa wanafunzi wa kike na mmoja wapo nilikua nampenda sana na nilikua na aibu sana. Nimewahi kutumwa pahali,nikakuta mwenyeji yupo binti,nikapiga hodi na kujiitikia mwenyewe karibu!!!.

Ila sasa hivi naweza hutubia hata maelfu ya watu,naweza ingia mjadala wowote na niko very comfortable and relaxing.

I can feel your feelings, your stress, utakua sawa ila you need to work on it buddy.
 
Kwa maelezo haya, basi una tatizo kubwa. Lifanyie kazi haraka kablq halijaathiri mpangilo wako wa maisha.

Hatua ya kwaza ya kuishinda aibu ni kuangalia watu machoni bila kupepesa macho wakati unaongea nao.
Hili lifanye kwa kudhamiria!
 
Uko mkoa gani kwanza

Nilikua kama wewe mpaka namaliza advance naaibu kuongea kutongoza ilikua mtihani

Wahuni wa chuo wakaniadd friend request wakaniona huyu jamaa future yake akiwa hivi hatoboi

Nikaanza kupelekwa viwanja
Mdo mdo nikaanza na kuchangamka
Hapo sinywi kitu kikali

Baada ya muda nikaanza kufukuzia na warembo
Ah

One year later nikawa aibu imeisha naongea tu fresh

Sahivi najiona ni mstaarabu sehemu za ustaarabu ila ukinikuta mahali unaweza kataa sio mimi

Kuna workmate wa kike aliniona mahali usiku akakausha akapiga simu kuhakikisha ni mimi na mimi nikaitoa nikaiangalia nikakausha nikajua ana shida zake tu nikaweka eroplen mode

Kesho hanimalizi maana nilizungukwa na uumbaji kama wote😂

Labda uwe na sura ya mizengo antipass curve ndo watakuogopa ila wote wanaokushauri nenda club au viwanja vya usiku wasikilize

Ni nadra sana kukuta watu wamepoa club au bar afu bar watu wapo friendly sana hamna mtu ana kinyongo

Sehemu moja nzuri sana ya kujichanganya tena ukienda zinazojaa jaa hzi unaweza shangaa kila weekend unakutana na watu tofauti

Sio lazima unywe pombe
Ila sasa usiweke fanta orenj kwenye meza na ww
 
Nimekushauri uvute bangi ikupe kujiamini, mods wamepita nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…