mwanaume anafundishwa kuwa mwanaume from day one anapotoka kwa mama, wakati kizazi cha siku hizi mwanamke anafundishwa kuwa kama mwanaume ili aweze ku survive mfumo dume ... na kama binti anajiamini its obvious ni ngumu sana ku-bend over kuachia ego ya mwanaume iendelee ndani ya nyumba wakati yeye ndiye mwenye kipato kikubwa sana na ndiye anaye run show ya familia nzima, kuanzia bills, ada za watoto, magari, nyumba, na mendeleo yote ... hapa panakalika kweli?? na mara nyingi wanawake wa aina hii huwa wana kiburi, wajuaji sana, majivuno, kujiamini kupita kiasi, wasiojali, etc ... tabia hizo ni sumu kubwa kwa wanaume wengi (kimalezi) ... mume katika mazingira haya, ni lazima tu awe mpole, au gumegume tu! inawezekana huyo jamaa aliona huyo dada ana dalili hizo ndio maana akalianzisha mazima, sababu wanaume wengi wanapenda amani katika nyumba zao na hawapendi wanawake wenye magubu!
on the other side of it, mwanamke mwenye kipato kikubwa akiwa ni mwelewa, mwenye malezi mazuri, na mwenye staha kwa mumewe, hata awe billionea bado hutoona mumewe anakuwa inferior au na wasiwasi na kipato cha mumewe hata siku moja. na mara nyingi wamama hawa huwaachia waume zao wakimbize shoo za familia kiasi kwamba mtu baki wa nje ni ngumu sana kutambua kama mama ndio mwenye kipato kikubwa kuliko baba, mifano hai ipo, na maisha yao ni mazuri tu. wanawake wa namna hii ni lulu kwa wanaume, huwa hawatumii nguvu kupata wenzi wa kuwaoa kabisa, tofauti na aina nyingine tajwa hapo juu!