Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Inawezekana maana wala hakuna ugomvi wala tatizo lingine alivyoona anapoishi binti na kujua kipato chake akakimbia!

Labda amewahi kuonywa na watu wazima juu ya wanawake wenye fweza au amewahi shuhudia kidume akiwa humiliated kisa mali...ila binafsi nina mifano halisi mingi nyie bamtu yani mkipata gape hasira unazimalizia kwa mmeo nakwambia
 
Inawezekana maana wala hakuna ugomvi wala tatizo lingine alivyoona anapoishi binti na kujua kipato chake akakimbia!

C isije ikawa alikuwa anatafuta sababu tu ... au kitu cha msingi alipopata hakuona thamani tena ya kuwa nae au hakutimiza lengo ... hahah
 
kukimbia demu sababu anazo huyo jamaa atakua mtoto wa watu,mwanaume unakoleza gemu mpaka unapewa mamlaka ya uprezidaa wa nyumba until futher notice
Haa haa haa,
Dah mkuu hii yako nimeipenda sn,najua mwanaume ukijiamin utatafuta tu pa kumkoleza binti na unamilikishwa kila kitu kiulain!
 
mwanaume anafundishwa kuwa mwanaume from day one anapotoka kwa mama, wakati kizazi cha siku hizi mwanamke anafundishwa kuwa kama mwanaume ili aweze ku survive mfumo dume ... na kama binti anajiamini its obvious ni ngumu sana ku-bend over kuachia ego ya mwanaume iendelee ndani ya nyumba wakati yeye ndiye mwenye kipato kikubwa sana na ndiye anaye run show ya familia nzima, kuanzia bills, ada za watoto, magari, nyumba, na mendeleo yote ... hapa panakalika kweli?? na mara nyingi wanawake wa aina hii huwa wana kiburi, wajuaji sana, majivuno, kujiamini kupita kiasi, wasiojali, etc ... tabia hizo ni sumu kubwa kwa wanaume wengi (kimalezi) ... mume katika mazingira haya, ni lazima tu awe mpole, au gumegume tu! inawezekana huyo jamaa aliona huyo dada ana dalili hizo ndio maana akalianzisha mazima, sababu wanaume wengi wanapenda amani katika nyumba zao na hawapendi wanawake wenye magubu!

on the other side of it, mwanamke mwenye kipato kikubwa akiwa ni mwelewa, mwenye malezi mazuri, na mwenye staha kwa mumewe, hata awe billionea bado hutoona mumewe anakuwa inferior au na wasiwasi na kipato cha mumewe hata siku moja. na mara nyingi wamama hawa huwaachia waume zao wakimbize shoo za familia kiasi kwamba mtu baki wa nje ni ngumu sana kutambua kama mama ndio mwenye kipato kikubwa kuliko baba, mifano hai ipo, na maisha yao ni mazuri tu. wanawake wa namna hii ni lulu kwa wanaume, huwa hawatumii nguvu kupata wenzi wa kuwaoa kabisa, tofauti na aina nyingine tajwa hapo juu!
Mkuu you nailed it.
 
lack of confidence! Hela si zinatafutwa tu. Kwanini unamkimbia unayempenda sababu ya hela unless huna kichwa, mikono wala miguu ntaelewa. Vinginevyo ni kuchakarika tu
Wala hujakosea mkuu,
Wengi wanaokimbia wanakuwa hawajiamini ndio maana!
 
Nimekuelewa na hayo yapo mengi yanatokea,
Ila kwa ishu hii huyu dada hakuwahi kuonyesha tabia yoyote kati ya hizo ulizotaja,kiasi kwamba hata jamaa alishindwa kuamin alichokiona alipofika kwa huyo binti na ili kuthibitisha akataka kujua ana kipato gani,
Na ndo maana kabla ya jamaa kujua walikuwa wanapenda vizuri tu na binti alimheshimu jamaa kwa kiwango kikubwa,
Iweje yy kujua kipato tu,bila kuonyeshwa dharau au tabia yoyote ya kumshushia hadhi anaamua kukimbia?
Canta kwani wewe ndiyo huyo dada?? Adhawaizi umeyajuaje hayo??
 
Wala hujakosea mkuu,
Wengi wanaokimbia wanakuwa hawajiamini ndio maana!

simtetei kabisa nasema nachoamini lakini ningekuwa mimi nisingemkimbia mpaka ingeanza ile ya "unapigwa jicho kichwani mpaka mguun alafu unasonywa" hapo mwanakwetu nasepa kidogo kidogo
 
lack of confidence! Hela si zinatafutwa tu. Kwanini unamkimbia unayempenda sababu ya hela unless huna kichwa, mikono wala miguu ntaelewa. Vinginevyo ni kuchakarika tu
Wewe na huyu jamaa aliyesepa mnafanana tu tofauti ni kuwa wewe unaamini at some point utakuja kuwa na hela kama binti au kumzidi. Kwa hiyo in principle bado unaamini demu hatakiwi kukuzidi mkwanja.
 
C isije ikawa alikuwa anatafuta sababu tu ... au kitu cha msingi alipopata hakuona thamani tena ya kuwa nae au hakutimiza lengo ... hahah
Hata sijui labda,ila ingekuwa ishu ni kumpata huyo binti mboa alishaanza kula ni miezi sasa mbona km palikuwa pabaya aliendelea mpaka alipojua kipato cha mtoto wa watu!
 
Labda amewahi kuonywa na watu wazima juu ya wanawake wenye fweza au amewahi shuhudia kidume akiwa humiliated kisa mali...ila binafsi nina mifano halisi mingi nyie bamtu yani mkipata gape hasira unazimalizia kwa mmeo nakwambia
Labda ndio malezi aliyopewa,ila km angekuwa ameonyeshwa nyodo hata kabla ya kujua uwezo wa binti na akavumilia basi baada ya kujua na akaamua kukimbia hata mie nisingelaum!
Ila kwa hili mie nahisi tu ni kushindwa kujiamini!
 
Hata sijui labda,ila ingekuwa ishu ni kumpata huyo binti mboa alishaanza kula ni miezi sasa mbona km palikuwa pabaya aliendelea mpaka alipojua kipato cha mtoto wa watu!

hahaha haya ila itabidi ukamilishe kwa kumpata jamaa tupate upande wa pili , maan asije kuwa kaipiga buti bahati hahahaah unaweza kujikuta unakuwa mtu wa kati
 
hahaha haya ila itabidi ukamilishe kwa kumpata jamaa tupate upande wa pili , maan asije kuwa kaipiga buti bahati hahahaah unaweza kujikuta unakuwa mtu wa kati
Nitajitahidi,kwavile shost bado hajakata tamaa na amesema atatumia namna yoyote kumshawishi jamaa waendelee coz anampenda sn,najua nitaendelea kupata story zinavyoenda na mungu akijali wakarudiana jamaa ataniambia tu km kulikuwa na tatizo lingine.
 
Hata sijui labda,ila ingekuwa ishu ni kumpata huyo binti mboa alishaanza kula ni miezi sasa mbona km palikuwa pabaya aliendelea mpaka alipojua kipato cha mtoto wa watu!
Sasa Canta wewe mwenyewe mtazamo kuhusu mapenzi/ngono ndio huo hapo (wa mwanaume kuwa anafaidi) halafu unashangaa jamaa kuchapa mwendo............Trust me bado tuna safari ndefu ya kurekebisha mfumo wa watu kufikiri.
 
tatizo tunalokosea ni kwamba mabinti zetu tunawalea kwa kuwaambia wasome kwa bidii ili waje kuishi independent life wakidepend kwa mwanaume watanyanyaswa, na kwa upande wa vijana wetu tunawapa yale yale malezi yetu ya kizamani kwamba wao ni wanaume na hatutaki kuwaambia ukweli dunia imeshabadilika kitambo watu wanaishi kwa kuheshimiana na kusaidiana kama familia matokeo yake wakija kuwa wakubwa na kuoana kijana anaexpect mke amtii hata kama yeye kijana ni mpumbavu na mke anajua yeye amesoma na anaweza kufanya atakalo na pesa yake matokeo ndio broken families tuzionazo sasa

Unakuwa na vijana wawili binti na mwanaume hao wote unawapa malezi tofauti matokeo yake ndo hayo
 
Dunia ina mambo kwelikweli na tukiyazoea yanakuja mengine mapya kabisaa
 
Nitajitahidi,kwavile shost bado hajakata tamaa na amesema atatumia namna yoyote kumshawishi jamaa waendelee coz anampenda sn,najua nitaendelea kupata story zinavyoenda na mungu akijali wakarudiana jamaa ataniambia tu km kulikuwa na tatizo lingine.

haya kwa hiyo tukae mkao wa kuendelea kusubiri ...

wewe kama wewe ulimshauri vipi suala lake??
 
Back
Top Bottom