Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

Mkuu Ni story. Ndefu nimeacha mengine nkajua ntayakuta kwenye maswli na ufafanuzi!! Mm kuaxhwa nimekubali mbali na huo msaad nliompa pia Kuna vingi tu nimemfanyia kwa huo muda mfupi nilikutana nae,! Kibaya aliniaminisha Hadi nkamtambulisha kwa wazazi na yeye akanitambulisha kwao kumbe alikua na lake moyoni!! Sijamkosea kitu na imekua gafla sana
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hapo sasa unakuja tatizo ni ule utambulisho
Sasa utatambulisha wangapi dunia yenyewe hii ya kudanganyana tuu
 
Hapo songa mbele na maisha yako . Kuhusu ghalama ulizotumia isikupe shida mapenzi ni ghalama. Kuna hasara nyingi umepata kwenye maisha na ulijipa moyo maisha yakaendelea. Litakushindaje hili?

Kwa kuwa wakati mko wote ulifurahia penzi lenu to the fullest na mpaka ukafeel kumpa chochote basi hujapoteza kitu.
 
Ahaaaaa usiwaze sana mkuu futa namba yake na picha zake kwenye simu tafuta mwanamke mwingine wa kukupa kampani,binadamu tumeumbwa kusahau,hakuna mtu hajawahi kuachwa
Ndilo napambana nalo , najua ntasahau lakini amejua kuniumiza huyu mwanamke Lol, yaani Kama Ni mechi nimepigwa hat trick first half
 
Mku mwanamke hawezi kumiliki wanaume wawili mkafahamiana. Achana na huo mzigo utakutoa roho.
Ndio maana nkasema acha nipate ushauri kwa watu wenye akili zao humu maana hiki nlichofanyiwa ni armery robbery ya mchana
 
Hapo songa mbele na maisha yako . Kuhusu ghalama ulizotumia isikupe shida mapenzi ni ghalama. Kuna hasara nyingi umepata kwenye maisha na ulijipa moyo maisha yakaendelea. Litakushindaje hili?

Kwa kuwa wakati mko wote ulifurahia penzi lenu to the fullest na mpaka ukafeel kumpa chochote basi hujapoteza kitu.
Sawa mkuu , japo itachukua muda maumivu kuisha lakini acha nipambane na hii Hali maana niliyataka mwenyewe!!
 
Wazee nakuja kwenu nikiomba ushauri,

Kama kichwa cha habari kinavyosema japo mimi sio mtaalamu sana wa kuandika nitajitahidi kuandika machache na ya muhimu, mwaka 2018 nikiwa kwenye safari zangu za kibiashara nilikutana na mwanamke mmoja tukiwa tumekaa siti moja kwenye bus tulilokua tunasafiria pamoja!!

Tulipofika kwenye kizuizi sehemu flan gari ikasimamishwa kwa ukaguzi, kumbe yule mwanamke alikua na mzigo wa magamu(magendo) na akatelemshwa hapo beria.

By then tulikua tushapeana namba za simu na nikataka kujua kulikoni ndipo aliponisimulia mkasa wake na akaniomba nifikishe taarifa kwa ndugu ambaye alinipa namba yake na maelekezo yote!!!

Hata nilipomtafuta yule bwana hakua tayari kuonyesha ushirikiano na yule mdada akawa Hana namna ila kuomba msaada wangu Kama naweza kumsaidia, baada ya michakato yote kufanyika ikawa inahitajika laki 5 ambayo alikua amepungukiwa ili amalize tatizo lake.

Mimi nkaamua kumsaidia kiroho Safi na akatoka ndani , mwanzonii mwa 2020 nkapata kesi ya uhujumu uchumi iliyoniweka gerezani mwaka mmoja na miezi Saba, yule dada nlimpa taarifa siku nakamatwa(alishakua rafiki yangu lakini sio kimapenzi) katika mwanzo wa kesi yangu Hadi natoka gerezani nlikua nae bega kwa bega na hakuna siku hata moja alikosa Kuja kunisalimia nkiwa gerezani (NB gerezani wanasalimiwa siku za wikend tu)

Mungu akasaidia kesi ikaisha na nkatoka, yule dada akanikaribisha nyumbani kwake na katika muda huo wote nlikua sijawahi kufika nyumbani kwake!! Nkakuta anaishi mwenyewe na akaniambia Ana miaka 2 hayuko kwenye mahusiano na pale anapoishi Ni nyumbani
kwake hajapanga

Basi nkatumia nafasi Ile kumuomba awe mwenzangu na akakubali !! Tumekaa kwa upendo na furaha nkiwa naenda kwake kila napohitaji hata Kama Ni usiku wa manane namkuta Yuko peke yake!!

Lakini alishaniambia huko nyuma alikua kwenye mahusiano na mtu japo waliachana sababu ya changamoto za maisha ya hapa na pale Basi kidume nkashika usukani

Yule X wake anasema waliishi pamoja miaka 10 lakini hawakua kwenye ndoa , waliishikimada tu, na walikua wameachana miaka imepita 2 Sasa Hadi mm nakutana nae kimapenzi

Siku moja yule X akapiga simu , akamwambia nasikia una mwanaume hapo nyumbani, Sasa Leo nakunywa KVANT nakuja kukufanyia fujo hapo kwako!! Nkamwambia yule mwanamke huyu X wako Kuna kitu anakudai hapa au alikusaidia kujenga hii nyumba?? akaniambia hajawahi hata kuninunulia glass hapa ndani, vitu vyote Ni jasho langu, Basi nkamwambia Kama Ni hivyo hawezi Kuja Ni mikwara tu!!

Ilipofika saa 5 usiku yule bwana akaja, kumbe alimaanisha, akafanya fujo anapiga madirisha na milango ikawa fujo kubwa wakati huo sisi tuko ndani tumefunga mlango

Asubuhi nkamtaka akaripot police akasema hawezi kumuweka ndani maana Kuna mazuri alimfamyia wakiwa pamoja Ila atamuonya asirudie! Jioni yake akanipigia simu akaniambia nimepata ushauri kwa watu wazima wamesema hapa kwangu nisilete mwanaume, kwa hiyo kuanzia leo usije hapa labda Kama Ni kukutana tukutane juu kwa juu!!

Nkasema sawa sitakuja Wala usiwe na Shaka kuhusu Hilo!!! Nkamuuliza au ndo unamrudisha x wako akasema yule siwezi kurudiana nae maana aliyonifanyia Ni makubwa!! Ntakua na wewe tu Ila nyumbani ndio usije maana namuogopa akisikia Tena uko hapa atakuja kunifamyia kitendo kibaya maana namfahamu Ni mkorofi.

Basi mm nkaamua kukaa kimya Ila Mara kwa mara akawa ananichokonoa kwa msg na simu akitaka tuonane, na mm nkajaa maana niwe mkweli nlijikuta nampenda Sana huyu mwanamke!! Juzi nkampigia simu hakupokea na sio kawaida yake , meseji hajibu nkasema huyu labda atakua na mwanaume ndani !

Nkaenda kwake kufika dirishani nkakuta anaongea na Yule x wake kwa simu ananisengenya na kuniongelea vibaya!! Nkamwambia fungua mlango na kweli akafungua tukiwa ndani nkamuhoji Kama anataka kuendelea na mm au anarudi kwa x wake akasema ananitaka Mimi!!

Basi ukatokea ugomvi Kati yangu na yeye na asubuhi akaita watu wazima tukasuluhisha , jioni hii Nimempigia simu kapokea yule x wake Ila kaongea kistaraabu tukamaliza , baadae nlipopiga Tena akapokea mwanamke akasema bwana yangu ameenda kazini ,namsubiria aje tulale Mimi nlikua na wewe sababu ya shida tu!

Nikihesabu garama na muda ambao nimeuwekeza kwake afu Leo anakuja kunilipa jeuri nakosa Raha kabisa hapa najiuliza nimfamye Nini huyu mwanamke?? Na nitoke vipi kwenye hii Hali niliyonayo maana roho Inaumia Sana , nahisi nlikutana nae naweza kufanya tukio baya maana amenifanyia usaliti mkubwa Sana.


Nawasilisha wakuu naombeni ushauri wenu
Mlikutana barabarani, achaneni barabarani kwisha!
 
Mtoa mada unatatizo mengi, ntaorodhesha Hapa KISHA ntakushauri

1.Unakutana na mwanamke humjui vizur in&out unajitosa mazima moyo wako wote kumpenda sana.
Ni kosa kubwa Sana.

2. Unasahau kwamba mwanamke akiwa na stress Anahitaji faraja, faraja anaweza kupata kwa mtu yeyote Alie around. Bahat nzur ulikuepo wewe.
Ila hilo haiondoi mapenz kwa wake anayempenda kwa dhati, ata Kama kamzingua sana. Anavumilia hivo hivo anaumia.

3. Kwenda kufanya mapenz kwny nyumba ya mwanamke Ni kosa kubwa Sana, ujatwambia kwann ulkua umpeleki kwako au hotel.
Nilikutahadharisha utakuja charangwa mapanga, na kweli jamaa akaja kukufanyia fujo.
(probably yeye Ndo sponsa wa hapo, stori ya Kila kitu chake Ulidanganywa)
Ndo Maana mwanamke akogopa kuachana nae Moja kwa moja, jamaa ni mshari Sana.

4. Jifunze kutofautisha huruma na upendo, uyo mwanamke alitulia kwako akiangalia Kama seriously jamaa atamove on, wewe uchukue nafas.
Bahat mbaya jamaa karudisha majeshi, huna chako Tena.

Cha kukushauri,
1.Kama kweli unampenda,
[emoji117]Vumilia mpk siku wavurugane ndo Wewe uchukue nafasi.
[emoji117]Wafanyie figisu wavurugane, mwanamke sana amchukie jamaa ww uchukue nafas.

2.Kama kwake umefata sex au uchumi
[emoji117]Kausha Kama hamna kilichotokea, weka ratiba zako vizur za kupewa Shea yako kisha ulale mbele.

YOTE NI MACHAGUO SAHII, CHOOSE WISELY[emoji4]
 
pole kwa yaliyokukuta

ila wanaume acheni kwenda kulala kwenye nyumba ambazo hamjui tofali zake zimetokea wapi

mtauwawa bure
 
Na mkiambiwa hajanifanyia kitu yote ni jasho langu ujue hapo anamaanisha hata kama alipewa chochote, imetokana na jasho la wakati wa kufirimbwa papuchi.

Ndo jasho lenyewe hilo wala sio la kushika jembe ukalima.
 
We kichaaa unapenda mbeba magendo?????serious????

Kuna tabia za kijinsia ukiona mwenye jinsia yake hana ujue unatatizo.

Mfano mwanaume hapendi kufanya kaziwaka biashara hapo moja kwa moja hiyo sio tabia ya kiume

Mwanamke anauza bangi too ambition hiyo sio tabia ya kike.
 
Ndugu yangu unajua nimeenda pale miezi 2 silali Ila nashinda pale naondoka jioni na nimekaa nae miezi 11 sikuwahi kuona mwanaume pale aje kugonga au apige simu yake
hujatujua vizuri.

Ukiwa jela bwana kuna kandege tulishagundua tukikabonyeza basi hapigi jini wala iblis ikaingia.

hukuona ka ndege kwenye simu?

Ndo uchawi wenyewe huo.
 
Usinunue magonjwa kwa bei rahisi, mshukuru Mungu una afya njema na Mwanamke amekueleza ukweli tofauti na hapo unaingia kweny shida achana naye kuna wanawake wazuri wengi sana hapa duniani
 
Mbio zako ndio zitazo kuokoa.Achana na wake zawa tu miaka10 unadanganywa wameachana??? Tafuta mwanamke uoemabinti wako lundo.
Mbona komenti yako imemaliza kila kitu bulaza, uyu alikuwa kaoa mke wa mtu hivi miaka 10 wanapika wanapakua kwel na ww unasema umepata mpenzi hatar sana
 
Back
Top Bottom