Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,999
- 23,540
Nadhani kila jambo ukilitazama kwa upande m'moja hautaona sababu za upande wa pili.Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔
Pole kwa changamoto.
Kuna wanawaume ni unreasonable au hawana mashiko inapokuja swala la mke kufanya kazi. Sababu zao haviendani na uhalisia wa matendo yao kwa wake zao.
Mfano mleta uzi anasema mumewe amekataa kumpatia matunzo yeye na watoto,hivyo it means mwanaume ana matatizo wazi kabisa kwa maana anataka kumtesa na watoto.
Lakini wapo wanaume wanazo sababu za msingi na kiuhalisia unaona kabisa wana hoja. Anakataa mke kwenda kutafuta ajira ila anafungua biashara mkewe atakwenda kusimamia. Nyumbani anatoa matunzo na kusimamia bills zote na mkewe anampatia pesa za matumizi na kumshirikisha mipango muhimu kiasi hata ikatokea mume amesafiri mke anamudu kusimamia vitu vyote sababu ana details zote na anashiriki.
Ni vema kabla ya kudhania then upate muda wa kuelewa na kujua marefu na mapana ya kwanini mwanaume akatae wewe kama mkewe kufanya kazi.
Kuna mwanamke ukimtazama tu unajua huyu mwaka hautaisha huyu kazini watamchota akili na kumtoa kwenye ramani ya ndoa. Na mbaya zaidi ni kuna watoto,ukiwafikiria tu, unaona atulize tu makalio yake nyumbani life inaendelea utabeba bills zote.
Tunawajua wake zetu madhaifu yao hata kabla wao hawajaonyesha dalili yoyote.